Mgunda hawezi kuifikisha popote Kil Stars

Mgunda hawezi kuifikisha popote Kil Stars

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Nimeuangalia mchezo wa Kil Stars toka dk ya 12 ya mchezo. Pamoja na mapungufu ya mchezaji mmoja mmoja lakn kocha kaonyesha mapungufu mengi na makubwa ya kimbinu.

1. Timu ilimshinda kuipanga

2.Wachezaji walikua wanafanya makosa mengi yanayojirudia lakn akawa kimya tu. Sikumuona akiwakumbusha wachezaji majukumu yao km ilivyokua kwa kocha wa Kenya. Kuna muda Stars walikua wamerundikana upande wa kushoto( kpnd cha 2) na kila wakijaribu kupiga pasi Wakenya wanapola mpira. Lakn upande wa kulia ulikua mtupu, nilitegemea kocha aone hilo kosa lakn wapi! Stars waliendelea kurudia kosa hilo zaidi ya mara 4 au 5.

3. Alikua anafanya mabadiliko bila mkakati. Timu iliendelea kucheza vile vile licha ya kufanya mabadilio. Hakujua timu iko weak sehemu gani. Yeye alifanya sub.ili akomboe goli tu basi bila mbinu inayoeleweka.

4. Mpira ulipoisha eti anasema bila aibu kuwa timu ilitengeneza nafasi nyingi,Nafasi zipi? Hapo ndo nkajua hatuna kocha kabsa.Ukiwaangali Kenya walikua wanaonekana kujua wanachokifanya.

Baada ya kupata goli tu Kenya walianza kucheza kimkakati kulinda goli lao huku wakishambulia kwa kushitukiza na kuuficha mpira pindi wanapoupata,na walifanikiwa. Wapo watakaosingizia timu yetu ni mpya lakn hata kenya timu yao ni mpya kabsa. Ni wacheza 3 tu ndio waliokuwepo mwaka 2017 walipochukua kombe. Kwangu Matola na Zuberi wangetosha kupewa timu kuliko huyu mjanja mjanja. Ngoja mtaona.
 
Hivi mfumo alioutumia kocha katika timu yetu aniambie mana sikuona mfumo wowote ule yani kila mchezaji anacheza kama ndondo vile
 
Kilimanjaro stars wangepewa Zuberi Katwila na Meck Mexime......!
 
Na hasipo jirekebisha tutapoteza mechi zote katika kundi letu.
 
Mgunda kocha mpuuzi, timu yake tu coast Union tia maji tia maji
 
Wote hawa ni matokeo ya soka la bongo lisilokuwa na mipango tuendelee kuajiri wageni tu hadi hapo hiki kizazi cha kina Mbape na wengine wanaokuja watakapokomaa na kuja na mbinu mbadala
Kilimanjaro stars wangepewa Zuberi Katwila na Meck Mexime......!
 
Ndiyo tushangae kapewa timu kwa vigezo vipi zaidi ya urafiki na Karia na kujua kuwalamba miguu vigogo wa TFF.
Si wote wa mkoa wa Tanga ,tatizo media zetu nazo hovyo, walitakiwa walianzishie mjadala hili vigezo gani vimetumika kumteua kocha kill stars


Kuna siku nilijiuliza prison hainapoteza mechi hata moja ,mpk sasa lkn kocha wake hajawahi kuwa hata kocha bora wa mwezi
 
Hilo nalo neno
Si wote wa mkoa wa Tanga ,tatizo media zetu nazo hovyo, walitakiwa walianzishie mjadala hili vigezo gani vimetumika kumteua kocha kill stars


Kuna siku nilijiuliza prison hainapoteza mechi hata moja ,mpk sasa lkn kocha wake hajawahi kuwa hata kocha bora wa mwezi
 
Mgunda kafanya maajabu yapi kwenye ukocha mpaka wakampa timu?
 
Back
Top Bottom