Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,896
- 4,058
Nimeuangalia mchezo wa Kil Stars toka dk ya 12 ya mchezo. Pamoja na mapungufu ya mchezaji mmoja mmoja lakn kocha kaonyesha mapungufu mengi na makubwa ya kimbinu.
1. Timu ilimshinda kuipanga
2.Wachezaji walikua wanafanya makosa mengi yanayojirudia lakn akawa kimya tu. Sikumuona akiwakumbusha wachezaji majukumu yao km ilivyokua kwa kocha wa Kenya. Kuna muda Stars walikua wamerundikana upande wa kushoto( kpnd cha 2) na kila wakijaribu kupiga pasi Wakenya wanapola mpira. Lakn upande wa kulia ulikua mtupu, nilitegemea kocha aone hilo kosa lakn wapi! Stars waliendelea kurudia kosa hilo zaidi ya mara 4 au 5.
3. Alikua anafanya mabadiliko bila mkakati. Timu iliendelea kucheza vile vile licha ya kufanya mabadilio. Hakujua timu iko weak sehemu gani. Yeye alifanya sub.ili akomboe goli tu basi bila mbinu inayoeleweka.
4. Mpira ulipoisha eti anasema bila aibu kuwa timu ilitengeneza nafasi nyingi,Nafasi zipi? Hapo ndo nkajua hatuna kocha kabsa.Ukiwaangali Kenya walikua wanaonekana kujua wanachokifanya.
Baada ya kupata goli tu Kenya walianza kucheza kimkakati kulinda goli lao huku wakishambulia kwa kushitukiza na kuuficha mpira pindi wanapoupata,na walifanikiwa. Wapo watakaosingizia timu yetu ni mpya lakn hata kenya timu yao ni mpya kabsa. Ni wacheza 3 tu ndio waliokuwepo mwaka 2017 walipochukua kombe. Kwangu Matola na Zuberi wangetosha kupewa timu kuliko huyu mjanja mjanja. Ngoja mtaona.