Mguu unataka kunitoa roho, msaada wakuu!!!

Mguu unataka kunitoa roho, msaada wakuu!!!

Job K

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Posts
9,314
Reaction score
7,149
Nimekuwa na tatizo la kusumbuliwa na mguu wa kushoto leo yapata miezi mi-3, kiasi nashindwa hata kukaa kwenye kiti kwa ajili ya kufanya kazi kwenye computer. Ukikaa tu misuli inakaza siyo kawaida unatamani kuakaa chini (sakafuni). Hapa ninapoandika nimepiga magoti utafikiri nasali rozari takatifu. Shida ilianza kama maumivu tu ya kawaida baada ya kukaa muda mrefu kwenye computer sasa imekuwa kinyume maumivu ni makali mno.

Nimepewa madawa hospitalini sasa yapata mwezi nayameza lakini siponi tu. Maumivu yanaanzia kwenye T.A.K.O la kushoto yanashuka na hiyo misuli ya nyuma hadi kwenye kisigino, utafikiri kuna mtu anazivuta hizo muscles. Dawa zote za kuchua nimetumia mpaka nimekata tamaa, vidonge aina ya neuroton nimetumia hakuna kitu. Sasa kama kuna ma-DR waliobobea kwenye matatizo ya muscles hapa JF naomba msaada wenu!!!
 
Hii tunaita Sciatica na sababu kubwa ni kukaa kwa muda mrefu au kuweka pochi kubwa sana mfuko wa nyuma. Hivi vyote husababisha compression ya Sciatic nerve as a result unapata maumivu makali. Sasa nenda hospital iliyo karibu nawe kitengo cha mazoezi hawa wanaweza shughulikia tatizo lako vema. Au kama vp fika Peramiho hospital kwa huduma bora zaidi yupo Dr mzuri pale anaitwa Dr Mdede au Dr Thaday au Sr Amana.
 
Asante Mkuu kwa ushauri!

Nitapitia hapa hospitali ya mkoa kama hicho kitengo kinafanya kazi vizuri, si unajua tena hospital za M'kwere X-ray yenyewe mpaka uende hospital za mission "AIBU". Ningekuwa karibu na Peramiho ningekimbia huko sasa ndugu yangu kutoka kanda ya ziwa mpaka kusini ni shughuli pevu!!

Asante sana mkuu na ubarikiwe!!

Nitashukuru pia kama kuna ma-physiotherapists humu ndani wakanishauri namna ya kufanya hayo mazoezi on my own!!
 
Back
Top Bottom