Job K
JF-Expert Member
- Oct 4, 2010
- 9,314
- 7,149
Nimekuwa na tatizo la kusumbuliwa na mguu wa kushoto leo yapata miezi mi-3, kiasi nashindwa hata kukaa kwenye kiti kwa ajili ya kufanya kazi kwenye computer. Ukikaa tu misuli inakaza siyo kawaida unatamani kuakaa chini (sakafuni). Hapa ninapoandika nimepiga magoti utafikiri nasali rozari takatifu. Shida ilianza kama maumivu tu ya kawaida baada ya kukaa muda mrefu kwenye computer sasa imekuwa kinyume maumivu ni makali mno.
Nimepewa madawa hospitalini sasa yapata mwezi nayameza lakini siponi tu. Maumivu yanaanzia kwenye T.A.K.O la kushoto yanashuka na hiyo misuli ya nyuma hadi kwenye kisigino, utafikiri kuna mtu anazivuta hizo muscles. Dawa zote za kuchua nimetumia mpaka nimekata tamaa, vidonge aina ya neuroton nimetumia hakuna kitu. Sasa kama kuna ma-DR waliobobea kwenye matatizo ya muscles hapa JF naomba msaada wenu!!!