Kuna vitu vingi hapo. Yangu ilikuwa inagongagonga sana. Tukabadili shock absorbers, stabilizer links na bushes, wishbone bushes, rack end pia zilikuwa zimechoka. Sasa hivi kimyaaa hadi unaipenda ukipita rough road.
Aangalie ile rubber iliyo kwenye makutano ya spring na 'plate' ya shock absorber. Kama imeisha ile, ina maana chuma kwa chuma vinakutana, lazima utaisikia inagonga ukiingia kwenye mashimo.
Pia aangalie engine mountings, zile rubbers zinazoshikilia injini kama zimeisha, kunakuwa na udhaifu pale unapopita kwenye rough road na kusababisha mtikisiko wa injini kusikika kwenye body ya gari.
Hivyo vyote nilivi experience kwenye usafiri wangu, jaribu kukagua humo.