Mguu wa mbele wa gari

Mguu wa mbele wa gari

BRO SANTANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2015
Posts
1,845
Reaction score
2,248
Kwema ndugu zangu?

Gari yangu ni runx inagonga sana mguu wa kulia wa mbele nikiingia rough road. Nimepeleka kwa fundi akasema nibadilishe shockup lkn bado inapiga kelele yani inagonga sana.

Msaada tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna vitu vingi hapo. Yangu ilikuwa inagongagonga sana. Tukabadili shock absorbers, stabilizer links na bushes, wishbone bushes, rack end pia zilikuwa zimechoka. Sasa hivi kimyaaa hadi unaipenda ukipita rough road.

Aangalie ile rubber iliyo kwenye makutano ya spring na 'plate' ya shock absorber. Kama imeisha ile, ina maana chuma kwa chuma vinakutana, lazima utaisikia inagonga ukiingia kwenye mashimo.

Pia aangalie engine mountings, zile rubbers zinazoshikilia injini kama zimeisha, kunakuwa na udhaifu pale unapopita kwenye rough road na kusababisha mtikisiko wa injini kusikika kwenye body ya gari.

Hivyo vyote nilivi experience kwenye usafiri wangu, jaribu kukagua humo.
 
Back
Top Bottom