Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Nani msafi?slaa?mbowe?zitto?acheni kujidanganya "we nyumba yako ya kioo afu unataka vita ya mawe"aya mfuatilie slaa nae kiundani uchafu anaoufanya baada ya mikutano yake ya M4C?ninaposema umfuatilie haimaanishi umfuatilie jf but in real life!huku kunduchi nyumba anayoijenga??sijui ela kapata wapi??huyo mbowe bora nisiseme??mkamilifu hakuna aliyekuwepo nitajie huko chadema!
 
Viongozi wetu wenye utajiri mkubwa sharti tuwahoji pesa walizipataje. Wasitukoge na pesa walizotuibia

Mteteeni Lowassa ila NI MWIZI MKUBWA KABISA, and we know it!
 
na Danson Kaijage | Tanzania Daima

WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amesema hana fedha wala si tajiri bali ushawishi mkubwa alionao na wafuasi wengi wanaomuunga mkono katika shughuli za kimaendeleo ndivyo vinavyomng'arisha.

Kauli hiyo aliitoa jana wakati wa uzinduzi wa Jumuiya ya Akiba, Mikopo na Maendeleo Dodoma (Jamimado) katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Lowassa anayetajwa kuwa miongoni mwa wagombea urais mwaka 2015 kupitia CCM, ambaye amekuwa akiandamwa kwa kufanya siasa kwenye makanisa, alisema amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuchangia masuala ya maendeleo katika vikundi mbalimbali kwa lengo la kuwakwamua katika umasikini.

"Najua mmenipa heshima ya kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Jumuiya ya Jumimado kwa kuwa mnajua ninachokifanya kwingine. Sina fedha, lakini nina ushawishi mkubwa kwa watu na wengi wananiunga mkono," alisema.

Aliwataka wanajumuiya hiyo kujipanga ili wafanye harambee waweze kupata fedha zaidi ya sh milioni 500 na kwamba hilo linawezekana.

"Nataka tukifanya harambee iwe babu kubwa ili kila mtu ajue tumefanya nini, na nilitamani tufanye harambee hiyo kabla ya mwisho wa mwaka huu. Unajua ukiwawezesha akina mama umeliwezesha taifa na utakuwa umeondoa umasikini," alisema.

Lowassa alisema ameamua kutoa sh milioni 10 kwa ajili ya maandalizi ya harambee itakayokuwa na tija pamoja na kuutunisha mfuko wa jumuiya hiyo.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Aksa Lemwayi katika risala yake alimmwagia sifa lukuki Lowassa kuwa wanamtambua ni baba wa kupinga umasikini katika maeno mbalimbali hapa nchini.

"Tunatambua jinsi anavyosimamia na kutekeleza maamuzi yake katika shughuli za kimaendeleo, amekuwa ni kiongozi wa aina yake katika kutambua na kuthamini shughuli za maendeleo katika jamii," alisema.

Aliongeza kuwa Lowassa amekuwa ni kiongozi anayepigana kufa au kupona kuhakikisha jamii inaondoka kwenye lindi la umasikini.

Lemwayi alisema wanajisikia furaha na ufahari kumualika Lowassa kwenye uzinduzi wa jumuiya hiyo.

Alisema kuwa jumuiya hiyo kwa sasa inakabiliwa na changamoto za kukosekana kwa usafiri kwa wanachama wanaotoka maeneo mbalimbali nje ya mji.

Alibainisha kukosekana kwa usafiri kunafanya shughuli za jumuiya hiyo ikiwemo vikao vya mara kwa mara kushindwa kutofanyika au kufanyika kwa wakati usiostahili.

Lemwanyi aliziomba taasisi za kifedha zipanue mitandao katika kutoa mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha Watanzania wengi kujikwamua katika dimbwi la umasikini ambao kwa sasa ni kilio kikubwa kwa wananchi wengi.
 
Ni vizuri Lowassa ukawa mkweli. Sema "Nina pesa na watu" Hivi mtu asiyekuwa na pesa anaweza akawa anatoa mamilioni yote hayo katika harambee mbali mbali? Kwa maisha ya kitanzania unahadhi ya kuitwa Milionea. Hivi kama una pesa na ni halali kwanini unakwepa kusema nina pesa na watu wanaoniunga mkono? Be honest EL!
 
Wanasiasa kwa uongo wamekubuhu! Kama hana hela hizo milion kumi kapata wapi? Na sio hizo tu sehemu nyingi ikiwemo makanisani huwa anatoa pesa. Hata hao watu wanajua atachangia ndo maana wanamualika mara kwa mara, sjui ndo anatakatisha pesa ya Richmond atajua mwenyewe ila pesa anayo sana asituongopee
 
Maisha yanakwenda kasi sana ndani ya CCM nguvu ya lowasa haizuiliki kwa kweli huyu jamaa pamoja na kuchafuliwa anazidi kung'ara na ukweli wa wanazuoni kuwa mti wenye matunda ndio hupigwa mawe unadhiirka ata ZUMA alibambikiziwa kashfa na ZUMA the same na LOWASA alivyofanyiwa na KIKWETE lakini umma wa Afrca ya Kusini uliamua na leo ZUMA ni Rais Lowasa CCM si baba yako wala mama yako leo KANU ya Mzee Kenyata ipo wapi wanaokutaka uwaongoze na kuwatoa katika ili Ombwe la uongozi ambalo familia inaifanya ikulu kuwa kijiwe kama alivyosema silaha....usijutie ulichokifanya ulivyoita wafuasi wako na kumuunga kikwete mkono kufanya kosa si kosa kosani kurudia kosa..simama imara kwa pamoja tutashnda
 
Maisha yanakwenda kasi sana ndani ya CCM nguvu ya lowasa haizuiliki kwa kweli huyu jamaa pamoja na kuchafuliwa anazidi kung'ara na ukweli wa wanazuoni kuwa mti wenye matunda ndio hupigwa mawe unadhiirka ata ZUMA alibambikiziwa kashfa na MBEKI the same na LOWASA alivyofanyiwa na KIKWETE lakini umma wa Afrca ya Kusini uliamua na leo ZUMA ni Rais.

Lowasa CCM si baba yako wala mama yako leo KANU ya Mzee Kenyata ipo wapi wanaokutaka uwaongoze na kuwatoa katika ili Ombwe la uongozi ambalo familia inaifanya ikulu kuwa kijiwe kama alivyosema silaha....usijutie ulichokifanya ulivyoita wafuasi wako na kumuunga kikwete mkono kufanya kosa si kosa kosani kurudia kosa..simama imara kwa pamoja tutashnda
 
Huwa si mkweli na hili ni sehemu tu ya matatizo makubwa aliyonayo EL na hii kwa wenye akili timamu tusiohitaji kutumia masabuli kufikiri na kutenda tunafahamu kuwa hafai kuwa Raisi wetu hata siku moja. Ila kwa wenzetu wengi tu na mtawasikia muda mfupi wakichangia humu JF wanamfagilia sana bila ya kutambua kuwa wanatuongezea umasikini waTZ kwa kuwa na sampuli hii ya watu wanaotumia fedha kuutaka uongozi kwa manufaa ya matumbo yao bila kujali maskini mamilioni wa Tanzania.

Mifano ni mingi tu ya ushiriki wake katika kupora rasilimali za nchi hii na kuwaacha waTZ maskini lakini wanaomtetea hawataki kuona wala kusikia. Mfano ni suala la Richmond na Dowans yeye ni sehemu ya wamiliki pamoja na rafiki yake Rostam.

Wamekwapua toka TANESCO zaidi ya mabilioni na hatimaye bado wanatakiwa walipwe tena mabilioni ya watanzania ambao hawana huduma bora za afya, elimu, maji na umeme vijijini. Lakini yote haya wenzetu hawa hawaoni wala kusikia.
 
KUMBUKENI HAYA....Huyo mtu hakuanza kuhusishwa na kashfa za ufisadi leo wala jana,... wewe kama unapenda sura yake nenda kanywe nae chai. ANA LAANA YA MWALIMU NYERERE, NO WONDER HIZI RECENT CAMPAIGNS ZA KUMDISCREDIT MWALIMU ZINA LENGO MAHSUSI LA KUMSAFISHIA NJIA HUYU MTU MAANA WANAJUA, LAANA YA MWALIMU NYERERE HAINA EXPIRY DATE. Tujikumbushe simulizi za watu(Mzee Kasori) waliokua wanamjua vizuri na ni wazalendo wa kweli wenye uchungu na Tanzania.SALAAM KWA MH. EDWARD LOWASA NA WENZAKE KUHUSU KUSEMA UKWELI (TRUTH) NA SUALA ZIMA LA UADILIFU NA UWAJIBIKAJI WA VIONGOZI TANZANIA (Sehemu ya makala yake)

Naam, tazama ahadi ya 8 ya mwanachama wa CCM, inasema, " NITASEMA KWELI DAIMA, FITINA KWANGU MWIKO" mwisho wa kunukuu.

Ndugu zangu waheshimiwa wote waliotajwa katika sakata la Richmond napenda wasome kwa kurudia mara kadhaa nukuu hiyo niliyoanza nayo hapo juu katika mstakabali mzima wa kutukuza kwa unyenyekevu kitu kinaitwa kusema UKWELI (TRUTH). Wahenga walisema UKWELI UNAUMA. Ni vizuri tu wote tukakubaliana hivyo. Huo ndio ustaarabu. Ndio utu kusema ukweli. Tuhuma hizo nzito zinazowakabili wakizijibu pasipo kukiri kitu kinaitwa UKWELI na badala yake wakaendekeza majigambo , uwongo na tukafanya hivyo mahali pasipo husika hawalitakii Taifa letu la Tanzania mema. Katika hili hawatakiwi kutumia jaziba au hasira.

Tena wakumbuke kuwa Mh. Edward Lowasa, na Karamagi na Msabaha walipewa nafasi halali Bungeni. Pale walichokifanya kwa bahati mbaya walitawaliwa na jazba na hasira " ANGER ".

Ndugu zangu, kuhusu hasira naomba niwaase kama mtaalam mmoja kwa jina SENECA alivyosema kuwa ukikumbwa na hasira (samahani kwa kunukuu kwa kiingereza)"there is no other way but to meditate and ruminate well upon the effects of anger, how it troubles man's life. The best time to do this is to look back upon anger when the fit is thoroughly over. Anger is like ruin, which breaks itself upon that, it falls. The scripture teaches us to possess our souls in patience. Whosoever is out of patience is out of possession of his soul. Men must not turn bees" Mwisho wa kunukuu.

Katika makala yangu iliyopita Salaam kwa Mawaziri wa Mhe. J.Kikwete kuhusu uadilifu na uwajibikaji kwa sehemu kubwa nilizungumzia juu ya mawaziri bila kumtaja Mheshimiwa Edward Lowasa. Mb wa Monduli. Kwa haya aliyoyafanya baada ya kuomba kwa Spika Bungeni na kupewa nafasi ya kwanza ajieleze kuhusu ufisadi wa Richmond, namtafadhalisha asome na kurudia mara kadhaa nukuu niliyoanza nayo hapo juu sambamba na hiyo ya mtaalamu SENECA. Napenda niseme kuwa kwa yale aliyosema Bungeni na Monduli na katika mahijioano ya TVT, bwana Lowasa nasema "si mkweli hata chembe moja".

Waandishi wa habari wengu tu wamekwisha mchambua kwa usahihi jinsi asivyokuwa mkweli, asivyo muadilifu anavyopenda kusifiwa kwa gharama yoyotena asivyolitakia mema Taifa letu. Narudia, asome kwa utulivu nukuu zote mbili nilizoanza nazo hapo juu. Kama Mwanasheria Mkuu, Mwanyika na wenzake Lowassa hakuridhika na ushauri wao juu ya Richmond na kuona kuwa ulikuwa na madhara kitaifa, kwanini hakutafuta ushauri wa ziada? Je? Hizo ndizo rasilimali watu pekee nchini katika ushauri wa kiserikali? Je, Vyuo Vikuu na Mahakama Kuu hakuna wataalam wa kisheria wa kuisaidia serikali? Did he leave any stone un-turned?

Kwa mapenzi mema na nchi yetu na mwana (CCM) napenda niwape mfano hai wa Bwana Lowasa asivyo muadilifu na asivyopenda kuwajibika kichama CCM na kiserikali.

Tanzania nzima mtakumbuka kuwa huyu mheshimiwa Edward Lowasa alikuwa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais mwaka 1995 na akaenguliwa kwa hoja nzito ya kutokuwa muadilifu na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, kwa ukweli (wala sio tuhuma) kuwa alikuwa amejilimbikizia mali nyingi kwa kipindi kifupi ndani ya CCM na Serikali.Muda mfupi alikuwa ni mtumishi wa CCM, muda mfupi kama Mkurugenzi wa kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha. Mfano hai wenyewe uko hivi; tufuatane kwa kuusoma tafadhali:-

Mara baada ya kurudi Butiama, 1995, baada ya kuenguliwa kugombea nafasi ya urais, siku moja mapema asubuhi Bwana Lowasa alonipigia simu na kusema yafuatayo: "Bwana Kasori, naomba uende kumwambia Baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, aende Monduli kusaidia kusafisha jina langu ili nisikose ubunge kutokana na yale aliyonisema Dodoma".

Nilishikilia mkono wa simu (TTCL) kwa zaidi ya nusu saa tukiwa tunazungumza na hatimaye mimi nilipata ujasiri wa kumwambia Bwana Lowasa kuwa siwezi kwenda kusema maneno hayo kwa Baba wa taifa na kwamba akitaka aje Butiama na nitamruhusu waongee ana kwa ana. Nikanyamaza na hatimaye yeye akawa wa kwanza kukata simu. Hiyo ikawa itifaki njema kwangu!

Kesho yake tena asubuhi nilipokea simu, safari hii akawa ni mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa maneno yake alisema "Bwana Kasori,jana ulizungumza na Edward Lowasa; naomba ufikishe ombi lake kwa Baba wa taifa tafadhali". Kutokana na heshima ya Mheshimiwa Mzee Kawawa, nilikubali na nikaenda na kabla ya hapo nilimuomba Mzee Kawawa akae karibu na simu ili nimpe jibu muda si mrefu. Nilimueleza Baba wa Taifa kuwa "Mheshimiwa Edward Lowasa kupitia kwa Mhe. Mzee Rashidi Mfaume Kawawa anaomba usaidie kusafisha jina lake kule jimboni kwake Monduli ili asikose ubunge kutokana na yale uliyomsema katika Kamati Kuu ya CCM Dodoma".

Jibu la Baba wa Taifa alilonipa ni kuwa "Nenda umwambie Mzee Rashidi Mfaume Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa"!Watanzania wote, leo March19, 2008, nawaomba radhi kuwa jibu hilo kwa uzito wa maneno hayo kuwa "Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa" kweli kwa kuzingatia heshima kati ya wazee hao wawili; "Kawawa sikumwambia hivyo"! Badala yake nilimdanganya (nawaomba radhi tena watanzania) jibu nililompa Mzee Kawawa ni kuwa juma lililokuwa linafuata tungekuwa Dar es Salaam na kwamba aje Msasani aongee na Baba wa Taifa. Mhe. Kawawa alikubali. Nikarudi kwa Baba wa taifa kusema uongo (naomba radhi tena) kuwa "Mzee Kawawa ameomba mzungumze tatizo la Lowasa tutakapofika Dar es Salaam".

Baba wa taifa alikubali na akaagiza nimuombe Mhe. mzee Kawawa kuwa Lowasa na Guninita na wapambe wengine wa Lowasa wote wafike Msasani.Siku ya siku ikafika. Tukawepo Msasani na Mhe.mzee Kawawa akaja. Lowasa hakuwepo! Sababu anazijua mwenyewe.(muulizeni maana nasema ukweli). Mkutano ulipoanza mzungumzaji wa kwanza nikawa mimi, kueleza lengo la mkutano. Mzungumzaji wa pili alikuwa Baba wa Taifa na swali la kwanza ni kuuliza Lowasa yuko wapi?. Bila kupoteza wakati Mwalimu alisema "Rashidi , huyu Kasori ananiambai eti niende Monduli nikasafishe jina la Mhe. Lowasa eti asikose ubunge kwamba nilimchafulia Dodoma katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM. Kutokana na ombi lako nilimtuma akuambie usiwe mjinga kama Lowasa. Kasori alikuambia eh?"

Oneni , huko nyuma tayari nilishasema uongo kwa kutosema maneno hayo kwa Mhe. mzee Kawawa. Kweli hilo kurudiwa na Baba wa Taifa kwa Mzee Kawawa mbele yangu lilisababisha kalamu yangu kuanguka, nikatetemeka na nikatokwa na jasho jingi mbele ya hao wazee!!! Bila kutegemea na kwa mshangao mkubwa Mhe. mzee Kawawa alikubali kwa kuitikia "NDIO ALINIAMBIA". Mwalimu akacheka sana!!!! Sababu sijui hadi leo kwa nini alicheka sana.Kwa kuendelea, Mwalimu alimwambia Mzee Kawawa kuwa "Kasori ana umri mkubwa kuliko Lowasa. Kasori alipata taabu sana kufikisha kwangu ombi la Lowasa na aliniambia kuwa jana yake alikuwa amekataa ombi la Lowasa. Sasa nasema kuwa kwa umri wangu mimi mzee, Lowasa ni mtoto wangu tena mdogo sana. Kwa heshima mliyonayo kwangu na kwa chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina Bwana Lowasa asikose ubunge.

Kweli Lowasa ni jasiri sana kusema maneno hayo. Hayo ningeambiwa na Kasori tu ningesita kumuamini. Lakini kwamba hata wewe Rashidi ulitumiwa kusema maneno hayo! Huyu Lowasa ni jasiri sana!!. Lakini kwa nini hajatuambia ukweli kuhusu mali hizo ambazo ni nyingi kuliko mimi ambaye nimekuwa Rais wenu kwa kipindi kirefu? Sasa Bwana Rashidi, nakuomba hivi, kamwambie mwenyekiti wa CCM Mhe. Mwinyi aitishe wajumbe wote wa Kamati Kuu, chagueni tarehe na mahali popote Tanzania, mimi nitakuja kumsafisha Bwana Lowasa na nitagharamia mkutano huo kwa hela zangu. Kamwe msitumie hela za chama wala serikali. Monduli sitokwenda,umesikia eh?" Mkutano ukaisha hapo Msasani.

Hadi uchaguzi 1995, unafanyika na kumalizika Baba wa Taifa hakwenda Monduli. Alichukia sana tabia za Lowasa na alimfahamu kama mtu muongo na mwenye kiburi. Hadi Baba wa Taifa anafariki,sikuwahi na hata niandikapo makala hiisijasikia wala kusoma popote ambapo Lowasa anakanusha alivyolombikiza mali akiwa mtumishi wa CCM na serikali kwa muda mfupi kiasi cha kumzidi Rais wa Kwanza !!! Sasa anatuhumiwa na vyombo vya habari kununua sehemu ya Ranchi za Taifa kwa kuandika majina ya wanafamilia! Kama hilo nalo ni kweli, ningekuwa mimi nisingeota tena kugombea URAIS n.k Tanzania. Bora kuendelea na biashara kwa uwazi kuliko kupitia mgongo au wa serikali au wa chama ( CCM). Huo ndio ushauri wangu kama mwana CCM kwa Lowassa.

Angalia tunavyofanya "total transgression of CCM regulations and ethics." Kamati kuu 1995 ilimwona Mhe. Lowassa hana uadilifu. Mhe. Mkapa baada ya kuingia madarakani baada ya muda si mrefu sijui ni kwa kikao gain cha CCM na taasisi ipi ya serikali akamwona Lowassa ni safi na akamweka katika safu yake ya baraza la mawaziri. Huyu bwana akaendelea na huo usafi hadi akaukwaa uwaziri mkuu 2005. Yote haya yanatia shaka kama kweli ndani ya CCM na Serikali tuna benki sahihi za takwimu za mienendo kitabia ya wanachama na watumishi wetu kama si kubebana kwa majina tu!

Nilinunua gazeti la mzalendo nikampa Baba wa Taifa na aliposoma kuwa Lowassa ni Waziri alimaka AHH!! Katika hili nabaki nimeduwaa hasa tunapopeana madaraka makubwa ya kuendesha nchi kimzaha tu. Tukumbuke kuwa kwa kila kitu na kwa dini yoyote Mungu huweka wazi mambo mahali na kwa muda atakao yeye.( Time and space) ya Mwalimu J.K Nyerere juu ya Lowassa tuliyapuuza. Sasa Mungu kayaanika! Basi tuone hizi tuhuma za RICHMOND n.k, Mikataba ya Madini, EPA zitakavyoshughulikiwa.

Ni huyu Lowasa leo anasema kanyimwa "Natural Justice" hakuulizwa na kamati , kaonewa, kamati ya Mwakyembe inauonea wivu uwaziri mkuu wake na ni mahiri wa kuchukizwa mikataba mibovu na kudhalilika! Oh kweli? Hivi Lowassa amewahi kusoma wasifu wa kila mmoja wa hao? Bila kupima uzito, busara na hekima ya maneno yake anasema ameachia ngazi kama alivyofanya Mhe.Alli Hassan Mwinyi, Peter Kisumo, Peter Siyovelwa n.k. Hivi CCM yetu hawa ndiyo viongozi tulio nao ngazi za juu? Wasio sema ukweli? Tukumbuke na kukiri kwa dhati wajibu wa wanachama wa CCM , katika katiba (ccm) inasema 15 (7) " kuwa tayari kujikosoa na kukosolewa…Watanzania wenzangu haya anayosema Lowasa yanafanana na nukuu niliyoanza nayo?

Fikiria nairudia tena "For those winding and crooked courses, are the goings of the serpent, which goes basely upon the belly and not upon the feet! There is no vile that does cover a man with shame as to be found false and pertifidious" Niharakishe kusema hapa kuwa viumbe vyote ambavyo havikupenda kusema ukweli Mungu aliviadhibu kwa kuvifanya vitembelee matumbo yao milele nyoka wakiwemo! Lowasa, Mwanyika, Hosea na wenzake naomba kama nilivyoanza, tafadhali wasome hiyo nukuu mara kadhaa na waielewe na kuizingatia.

Watanzania wanawashangaa, wanadharau na kuchukizwa na viongozi wasiopenda kusema ukweli kwa maisha magumu waliyo nayo ambayo wao wanawazomea kwa dharau kuwa ni wavivu na wachovu wa kufikiri. Wanasahau kuwa hawa watu wa kawaida ndio wanaozalisha kile kinacholipa mishahara na marupurupu yao. Kama viongozi wakuu wa CCM, katika hili daima kumbukeni wajibu wenu kwa mujibu wa katiba ya CCM, ibara ya 15 (4) kuwa wakati wote mkweli, mwaminifu na raia mwema wa Tanzania. Onekaneni hivyo kwa vitendo tafadhali. Utaratibu huu wa kusema uongo unadhoofisha amani na utulivu Tanzania.Hayo niliyasema niko tayari kuyasema bungeni akiwepo Lowasa ikibidi.

Hatuwezi kukubali nchi hii kuendelea kuwa na viongozi wa aina hii. WAWE WAKWELI, WASEME UKWELI TU. WANAPOKOSEA HARAKA NA KWA UKWELI NA UNYENYEKEVU WAOMBE RADHI KWENYE VYAMA VYAO, SERIKALINI NA KWA WANANCHI. NI UPUUZI WA HALI YA JUU KUJITETEA OVYO NA KUINGIZA UKABILA ( LOWASSA NA OLE NAIKO) HATA KWA MAKOSA YALIYO DHAHIRI.Katika mahojiano na TVT Lowassa alikiri kuwa alishindwa kuvunja mkataba wa RICHMOND. Sababu alizitaja. Sawa.

Waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa Serikali, kwa mujibu wa kanuni za kudumu za utumishi wa umma ( Toleo 1994), kifungu F33, makosa yake kiserikali ni haya yafuatayo; 33( xi) omission which is against public interest. 33(xiii) negligence occasioning loss to the employer ( yaani serikali na taifa kwa ujumla). 33( xiv) gross negligence in the performance of duty. Kama mtendaji mkuu wa shughuli zote nzito za serikali bwana Lowassa hana namna ya kujitetea kwa makosa hayo yaliyodhahiri ambayo TANESCO imeendelea kudhoofishwa na RICHMOND kwa yeye kuogopa kutumia utaalam nje ya wale aliowaamini. Mbona tuna vyuo vikuu, je, aalivitumia kikamilifu? Mbona kwa maswala yasiyo na maslahi ya maana tumezoea sasa kukodi wataalam wa nje? Kwanini hakujiridhisha katika maeneo yote hayo?

Tatizo hili ni kubwa sana maana watanzania sasa wanatozwa viwango vikubwa sana kulipia umeme ikiwa ni pamoja na sehemu za uzalishaji zenye kutumia umeme achilia mbali malipo ya capacity charges? Nani anabisha kuwa kwa huu mkataba wa RICHMOND n.k Bwana Lowassa na Wenzake waliweka sahihi za kifo siyo kwa TANESCO tu bali pia cha kuvuruga maendeleo ya nchi yetu na kuendeleza umasikini?

Katika yote haya ambayo yamesemwa, Bwana Lowassa na wenzake wajue kuwa kama watanzania, we have a compelling moral case for complaining against him. There is also a compelling case that is in Tanzania's self interest. Recently many trade agreements already have made the poorest countries worse off. Such agreement already have condemned to death thousands of our people . Corporations of whatever name do strip Tanzania of its natural resources leaving behind a trail of environmental devastation etc. This is done through very poor legal frameworks. Nimuhimu tukawa na viongozi waaminifu, waadilifu na wasema ukweli.

Kwa haya yanayotendeka, something is fundamentally wrong with our government. Kwa kila maamuzi tunayoyafanya mara zote tuzingatie ni kwa maslahi ya nani; yale ya Taifa ni kipaumbele cha kwanza. Tuzingatie matumizi mazuri ya rasilimali zetu daima. Duniani ziko serikali nyingi tu ambazo zimevunja mikataba mibovu. Kwa ziara nyingi ambazo viongozi wetu wanafanya na baada ya wanahabari kupigia kelele RICHMOND, kwanini Lowassa huko nje hakutaka kujifunza namna ya kuvunja mikataba mibovu? Yaani umahiri wake uliishia mkataba wa maji Dar es salaam na kiwanja cha Mnazi Mmoja? Mikakati yetu ya maendeleo imekuwa haileti tija iliyokusudiwa moja ya sababu ikiwa a flawed vision of development. Successful countries have a broader vision of what development entails and a more comprehensive strategy for bringing it about. It is very unfortunate that in the majority of developing countries Tanzania included the nation – state has been weakened thoroughly! Haya maamuzi yanayofanywa na viongozi kama Lowassa ndiyo matokeo ya kutojua namna ya kuthibiti na kutumia kwa uangalifu fursa za kitu kinaitwa UTANDAWAZI.

Government that attempt to control capital flows find themselves unable to do so, as individuals find ways of circumventing the regulations. A county may want to raise the minimum wage, but discovers it can't, because foreign companies operating there will decide to move to a county with lower wages. Situmeona jinsi waziri Chiligati ( waziri wa kazi wa wakati huo) alivyohenyeshwa na wakubwa – wawekezaji kukataa kulipa kima cha chini hapa Tanzania? Wengine wamepunguza kazi ndugu zetu na sasa ni katika kundi la Machinga! Waziri mkuu wa wakati huo Lowassa alisaidiaje? KIMYA! Dhahiri kinachoonekana hapo ni sense of powerlessness.

Kwa kukumbatia matajiri na wakubwa wa nje, kupitia utanzawazi, baadhi ya viongozi wetu kama inavyojidhihirisha kupitia RICHMOND n.k. find their ability to act eroded. These days it is the order of the day for the electorate to see its government bending before foreigners wenye (mitaji). Day in day out democracy is being systematically undermined. When the electorate shouts through the media etc, no body listens! Wanataka sifa tu. The electorate feels being thoroughly betrayed. Whether we like it or not, it is perceived, quite rightly, I think the way globalization is currently managed is not consistent with democratic principles. Little weight is given to the concerns and voices of ordinary people and the poor! Kwa kiburi cha wakubwa kutosikia, kutopenda kukosolewa Tanzania inaendelea kubaki masikini.

Lowassa na wenzake wangekuwa makini na mahiri katika kusikiliza waandishi wa habari mapema RICHMOND n.k isingetufikisha tulipo sasa ambapo kila siku tunapoteza fedha nyingi. Tusingekuwa na tume juu ya tume ambazo baadhi tunazibeza kwa kejeli hata kwa kutumia chama (CCM). CCM kweli tunasoma na kuzingatia kwa vitendo wajibu wa mwanachama wa CCM kifungu 15(3) na 15 (4) na 15(7) pamoja na ahadi za mwanachama wa CCM (3) na (4), na (8). Hivi CCM sasa ni mali na jina la mtu; kwamba hivyo mtu akikosolewa hamtaki kuona kakosa na mko tayari chama kife kwa ajili ya mtu mmoja au kundi dogo tu la watu? Nendeni Butiama mtupe majibu tafadhali. Uwezo, busara na nia vyote mnavyo.

Ningekuwa Lowassa Butiama nisingeenda. Yeye kwenda huko ni kejeli kwa Baba wa Taifa.BADO TUTAENDELEA KUWASEMA WENZAO KUHUSU MIKATABA YA HOVYO NA UKWAPUAJI WA RASILIMALI ZA NCHI HII. HOJA YA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR BWANA IDD PANDU HASSAN- " Lowasa kutostahili kuitwa Waziri mkuu Mstaafu" ni muhimu ikazingatiwa sambamba na utata wa stahili za mafao. Haitoshi kuimba utawala wa sheria na kumbe inapofika kwa wakubwa tunakunja na kunyonga sheria zetu. Sheria ni Msumeno. Someni Pensions Ordinance cap 371 sambamba na kanuni za kudumu za utumishi wa umma toleo la (1994) kifungu F53 (d) na (e).

Tusiwe na kigugumizi katika hili. Tujifunze yaliyojiri hapo jirani Kenya hivi majuzi.

Namalizia kwa kusema "Tuheshimu na kudumisha kitu UKWELI". Kwa viongozi, zingatieni na kwa unyenyekevu heshimuni viapo vyenumnapokabidhiwa madaraka. Baba wa Taifa daima katika mkoba wake alibeba Bibilia na Azimio La Arusha. Nyinyi kwa kipindi hiki kigumu cha ufisadi na kukithiri kwa rushwa na mikataba mibovu; bebeni daima photo-copy za viapo vyenu pamoja na Bibilia au Koran pamoja na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mnazo dini zenu. Sikusikia yeyote akiapa kwa dini za asili kwa Rais au kwa Spika wa Bunge.

Nawashukuru watanzania, Mhe. Spika na Waandishi wa habari ambao wamekemea maneno ya Lowasa na wenzake baada ya kikao cha Bunge.

Namshukuru sana Mhe. William H. Shelukindo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji na Biashara kwa kuwasilisha hoja ya kuundwa kwa kamati ya kuchunguza Richmond na shukran maalum nazitoa kwa Dr. Mwakyembe na wajumbe wote walioshughulikia suala la Richmond na kuwasilisha taarifa Bungeni kwa uadilifu mkubwa sana.

Mwisho nawashukuru Watanzania wote na nchi za nje walionipongeza na kunipa moyo kuhusu makala zangu za kukemea ukwepuaji rasilimali za nchi BoT. yenye kichwa cha habari "Salaam kwa Mawaziri" Namshukuru Rais Kikwete. Namshukuru pia Mhariri gazeti la Rai namba 748 na 749.Halmashauri kuu ya CCM inayokutana Butiama naitakia mafanikio makubwa katika maazimio watakayofikia . baada ya hapo muonekane mmedhamiria kutenda kwa kuleta maendeleo yenye kuzingatia uadilifu na uwajibikaji .

Viongozi wabovu wawajibishwe tu. Watanzania wengi leo bado wanamlilia Mwalimu J.K. Nyerere hasa kwa matatizo kama haya ya mikataba mibovu ya Madini, RICHMOND n.k. Wanasema sorry Mwalimu lived ahead of his time. Alituangazia kwa mengi, hakuna wa kutu tetea leo kwa matatizo yote haya.

Mungu Ibariki Tanzania. Mungu Ibariki Africa.

Samwel. H. Kasori

Katibu mstaafu wa J.K.Nyerere

0754 372141
 
Maisha yanakwenda kasi sana ndani ya CCM nguvu ya lowasa haizuiliki kwa kweli huyu jamaa pamoja na kuchafuliwa anazidi kung'ara na ukweli wa wanazuoni kuwa mti wenye matunda ndio hupigwa mawe unadhiirka ata ZUMA alibambikiziwa kashfa na MBEKI the same na LOWASA alivyofanyiwa na KIKWETE lakini umma wa Afrca ya Kusini uliamua na leo ZUMA ni Rais Lowasa CCM si baba yako wala mama yako leo KANU ya Mzee Kenyata ipo wapi wanaokutaka uwaongoze na kuwatoa katika ili Ombwe la uongozi ambalo familia inaifanya ikulu kuwa kijiwe kama alivyosema silaha....usijutie ulichokifanya ulivyoita wafuasi wako na kumuunga kikwete mkono kufanya kosa si kosa kosani kurudia kosa..simama imara kwa pamoja tutashnda
 
Du hata jana nilikuwa kwenye kampeni za udiwani Elerai Lema akawa anamsema huyu mzee ni mnafiki na anatafuta kura makanisani. Huo ni udini anataka siku akigombea urais viongazi wa dini aliowachangia wamuombee kura kwa waumini. Sahame on him. Anasema hana pesa atuambie ndani ya mwaka mmoja tu amechanga karibia bilion kazitoa wapi?
 
huyu KASORI naonaga ni kichefuchefu huwa simuelewi anajiita katbu wa mwalimu hivi mwalimu ni MUNGU....TIME WILL TELL LOWASA NI ZUMA WA TANZANIA....
 
mkuu amenena ila hoja yake haina mashiko amepata wapi watu kama si pesa zilizopata watu ,tunachohoji hapa ni pesa na si watu kila mtu ana watu wake ila linapokuja suala la pesa ujibu hoja umepataje hizo hela ni mishahara tu au kuna nyingine zisizo eleweka .pesa hasa ndio zinatakiwa zitolewe sababu na sio watu ,hata mimi nina watu sina pesa
 
Tena mtu wake wa kwanza na wa kufa na kuzikana ni Pasco wa JF...
 
HAKUNA WAZIRI ALIYEKUWA MTENDAJI KAMA LOWASA KATIKA BARAZA LA MKAPA....HOFU YA LOWASA KUUKWAA URAIS NDIO ILIMFANYA JK AWATUME MARAFKI ZAKE KUMUOMBA LOWASA ASIGOMBEE URAIS ATAMPA UWAZRI MKUU NA BAADA YA MIAKA MITANO LOWASA ATAKABIZIWA NCHI NA AHADI HIYO AKAWA AMEPEWA SAMWELI SITA NA JK NDIO UGOMVI ULIPOANZIA BAADA YA SITA KUPEWA USPKA AMBAO HAKURDHKA NAO AMBAPO UNAYEJIITA MWAMBA USEMAO UKWELI NI MWAKILISHI WAKE APA JAMVINI... NITAWALETEA THREAD YA KIKAO CHA LOWASA BAADA YA BUNGE LA BAJETI 2002/2003 Ambapo aliwaita wakuu wa mikoa 14 na viongozi mashuhuri kuwambia hatagombea urais wamuunge JK ambapo wengine walikataa katakata kumuunga mkono JK akiwemo mama Makinda na Kinana wakiamini JK si mwanasiasa imara ni mtu wa siasa nyepesi...Lowasa anaujua udhaifu wa JK na ndio anaoutumia kuingia magogoni
 
NAOMBA MSOME NAMNA JK ALIVYOINGIA IKULU

Huyu anajua ‘machungu' ya Rostam




Na Mwandishi Maalum - Imechapwa 20 July 2011

Gumzo la Wiki



HATIMAYE Rostam Adulrasul Aziz ameandika historia. Ni kwa kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hii ni baada ya miezi mitatu ya malumbano kati yake na baadhi ya wajumbe wapya wa sekretarieti ya CCM.

Kwa wale tuliobahatika kuwa ndani ya sakata zima la kupanda na kushuka kwa Rostam, hatutakuwa tumetenda haki tusipoeleza kilichojiri mpaka kuanguka kwake.

Ni vema tukaeleza haya ili kuipa historia nafasi yake; lengo likiwa kufanya umma uelewe nini kilijiri.

Rostam alikuwa rafiki wa muda mrefu wa Edward Lowassa. Ni wazi pia alikuwa rafiki wa Rais Jakaya Kikwete. Sina uhakika ni nini kilimfanya Rostam awe karibu na Kikwete kuliko Lowassa katika miaka ya 2002 hadi 2005.

Rostam alikuwa na mapenzi ya kweli na Kikwete; alidhihirisha mapenzi yake hayo mwaka 2002 pale palipotokea mivutano ndani ya mtandao iliyohusu nani hasa awanie nafasi ya urais kati ya Kikwete na Lowassa.

Wakati huo ilikuwa ikinong'onwa na kuripotiwa kuwa Lowassa alikuwa na nguvu kubwa ndani ya chama kuliko Kikwete.

Wengi walimuona Kikwete kuwa mtu wa matukio mepesi kama vile kukaa na wazee na kula nao, ili kujionyesha kuwa yeye ni "mtu wa watu" mwenye uwezo wa kuishi maisha kama yao.

Hatimaye baada ya ushawishi mkubwa wa Rostam, wakati wa mkutano wa bunge la bajeti mwaka 2003, ndipo Lowasa alipokubaliana na matakwa la Rostam.

Aliwaita wazee nyumbani kwake, wakuu wa mikoa 14 na watu wengine maarufu waliokuwa wanamuunga mkono na kuwatangazia rasmi kuwa hatogombea tena urais. Aliekeza wafuasi wake kuhamishia nguvu zao kwa Kikwete.

Hili halikuwa jambo rahisi. Baadhi ya wafuasi wake waligoma hadi kufikia wengine kuamua kukaa pembeni.

Miongoni mwa waliokaa pembeni ni Anne Makinda na Abdulrahman Kinana. Ila Kinana inadaiwa alijiondoa baada ya kuona wenzake ndani ya mtandao wanachafua wagombea urais wengine.

Kilichofuata ikawa kutafuta uungwaji mkono ndani ya chama. Kwa nguvu ya Rostam na Lowassa hili lilifanikiwa, huku Umoja wa Vijana (UV-CCM) ukiwa ndiyo nguzo kuu ya kusimamia kampeni za Kikwete.

Vijana waliotapakaa nchi nzima walianza kazi ya kumwita Kikwete kwenye matamasha mbalimbali kwa lengo la kumjenga kisiasa.

Baada ya hilo kukamilika, likaingia zoezi Na. 2 ambalo ni Rostam kutafuta njia ya kujipenyeza katika maeneo nyeti ya dola ili kuwaaminisha kuwa Kikwete anafaa.

Hilo lilifuatiwa na kampeni ya chinichini na wazi na upikaji taarifa, nyingine za "kiintelijensia" ili kuonyesha Kikwete ana nguvu isiyoweza kuzuilika.
Hatimaye, hata Rais Benjamin Mkapa akashawishika kumuunga mkono Kikwete.

Rostam alipiga hesabu za haraka na kugundua kitendo cha kupiga kura tatu kwa mgombea mmoja kilikuwa hatari kwa Kikwete.

Ni baada ya kubaini Frederick Sumaye, Profesa Mark Mwandosya, Dk. Abdallah Kigoda na Dk. Salim Ahmed Salim kuungana ili wafuasi wao wapigiane kura.

Kitendo cha wafuasi wa Kikwete kumpigia kura yeyote kwa kupitia utaratibu wa kura tatu, kama ulivyoelezwa kwenye kanuni za uchaguzi za CCM, kilikuwa kinakamilisha safari ya kushindwa kwake maana angekuwa anaongezea wenzake ushindi, huku yeye akibaki na kura chache.

Katika uchaguzi huo, kati ya kura zaidi ya 215 zilizopigwa, Kikwete alipata kura 76 tu.

Kwa maana nyingine, ilibidi kumshawishi Mkapa kupindisha kanuni za uchaguzi. Ghafla Mkapa akatangaza mtu "mmoja kura moja."

Huu ukawa ushindi mwingine wa Kikwete uliotengenezwa, kurabatiwa na kuandaliwa na au kwa msaada wa Rostam.

Uchaguzi mkuu ulikuwa mwepesi kwa kuwa kazi zote za chini zilifanywa na Rostam ambaye aliongoza timu kubwa ya wapiga kampeni waliotapakaa nchi nzima.

Mathalani, mimi nilikuwa nikiongoza kundi la watu tuliokuwa tukipokea maelekezo kutoka kwa Rostam moja kwa moja.

Baada ya ushindi wa Kikwete ndipo hasa tatizo la umoja ndani ya kundi kubwa la wanamtandao lilipojitokeza.

Katika kuhakikisha kila mwanamtandao anapata stahiki yake, Rostam akajikuta anatengeneza uadui na "vyombo" vya dola na viongozi wa chama, jambo lililochangia anguko lake la juzi.

Kosa la kwanza lilikuwa ni kusimamia Lowassa kupewa uwaziri mkuu. Baadaye "akamuumba" Samwel Sitta kwa kumpa nafasi ya spika – mtu ambaye alikuwa na matumaini makubwa ya kuwa waziri mkuu.

Katika kuhakikisha mpango wake wa kumweka Sitta katika kiti cha uspika unafanikiwa, Rostam aliwaomba wagombea wengine walioonekana wenye nguvu, akiwamo Philip Marmo kujitoa katika kinyang'anyiro hicho.

Inaaminika Rostam alifanya yote haya kwa baraka za Kikwete mwenyewe. Bali hapa ndiko ilikuwa tamati ya ndoa ya wanamtandao….

Mtandao uliobaki ukawa ule wa wote walioamini kuwa ni marafiki wa Kikwete, wakati ukweli ulikuwa Kikwete hakuwa tena na upande, bali aliunga mkono upande ulioonekana kushinda.

Kwa upande wa pili, ilianza kuonekana kuwa Kikwete amepoteza hamu na Rostam na ushawishi wake.

Ghafla Kikwete alimteua Pius Msekwa kuwa makamu mwenyekiti wa CCM, ilhali akijua Msekwa ni mhanga wa uspika uliochukuliwa na Sitta chini ya maelekezo thabiti ya Rostam.

Shughuli zote za kuendesha chama sasa zikawa chini ya Msekwa huku yeye akiwa nyuma akitazama minyukano yao.

Kama vile haitoshi, Kikwete akamteua George Mkuchika kuwa naibu katibu mkuu wa CCM, Tanzania Bara. Mkuchika alikuwa mhanga wa Rostam katika kinyang'anyiro cha nafasi ya katibu wa wabunge wa CCM.

Alipambana na Ali Ameir Mohammed. Ushindi wake huu haukuja hivihivi. Ilikuwa kama kumlipizia kisasi hasa baada ya Mkuchika, aliyekuwa rafiki wa Kikwete, kumgeuka wakati wa kampeni. Mkuchika alimuunga mkono Mwandosya.

Matokeo yake, Rostam akawa tayari amezungukwa na maadui wa kisiasa ndani ya chama, ndani ya bunge na ndani ya serikali.

Ripoti ya Bunge ya Richmond ilikuwa eneo mojawapo ambalo bunge chini ya Spika Sitta, CCM na serikali viliungana kuwashambulia Rostam na Lowassa, jambo lililobadili mwelekeo kutoka kilichoitwa na Kikwete, "ajali ya kisiasa" na kuwa tuhuma na hatimaye kuachia ngazi.

Bado wale viongozi waliokuwa wakituambia ubaya wake wamenyamaza kimya.

Ni wazi kabisa kumfanya Dk. Harisson Mwakyembe kuwa mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza sakata la Richmond hakukuwa kwa bahati mbaya.

Huyu alikuwa meneja wa kampeni wa Mkuchika katika kinyang'anyiro cha ukatibu wa wabunge wa CCM.

Matokeo ya uchaguzi uliopita ndiyo yaliyoleta taharuki ndani ya CCM, huku yakitafutwa majibu mepesi ya kufanya vibaya kwa chama hicho.

Mathalani hakuna aliyetayari kusema chama kiliwekwa pembeni katika uchaguzi mkuu uliopita na hata mwenyekiti wa kampeni, Kinana, alikuwa hajui kinachofanyika zaidi ya kuongea na vyombo vya habari.

Kazi zote za Umoja wa Wanawake (UWT) zilihamishwa kwenye chama zikakabidhiwa kwa mke wa rais, Mama Salma, huku zile za UV-CCM zikikabidiwa kwa watoto wa rais, Ridhiwani na Miraji Kikwete.

Kuna taarifa kuwa baadhi ya maeneo kama Iringa, msafara wa Ridhiwani ulikuwa na magari mengi zaidi kuliko aliyokuwa nayo mgombea mwenza, Dk. Mohammed Gharib Bilal.

Akiwa Iringa, Ridhiwani alivishwa uchifu, huku Dk. Bilal akiachwa bila kufanyiwa chochote, jambo lililosababisha chuki kwa wananchi, serikali na katika chama. Wenye chama walijitenga na shughuli za kampeni na kuiacha familia na marafiki zao.

Rostam hajajiuzulu kwa kuogopa matambo ya Nape Nnauye na wapambe wake. La hasha. Ni kwa kujua kwa dhati kuwa siyo kwamba Nape anawakilisha maazimio ya NEC, ukweli anawakilisha mawazo na maelekezo ya Kikwete.

Kwa kutambua hawezi kupambana na Kikwete anayepigana naye chini kwa chini, akaamua kufanya uamuzi wa busara wa kujiuzulu.

Rostam ameondoka. Lakini bado ana machungu na kinyongo.
 
Ningekuwa naamua nani awe rais wa nchi hii
jk ningeshamuondosha cku nyingi nakumpa lawasa
mana ili huyu mzee aishi baada ya 2015 ni lazima apate huo uraisi
bla hvo? tujiandae kumzika. kwa mana hyo watanzania wote
tutakuwa tumecomit crime kwa kushindwa kumpa uraisi mtu
ambaye tunajua anautaka kwa gharama yoyote ile

......................ANGALIZO....................................
Kwa kutambua hilo mimi nimejiandaa kumpigia kura huyu jamaa
sitaki kutenda dhambi ya kuua
 
Hivi nyny wachangiaji kwa nn mnakuja na hotuba ndefu kiasi hiki unasoma mpaka kizunguzungu bwana
 
Ni vizuri Lowassa ukawa mkweli. Sema "Nina pesa na watu" Hivi mtu asiyekuwa na pesa anaweza akawa anatoa mamilioni yote hayo katika harambee mbali mbali? Kwa maisha ya kitanzania unahadhi ya kuitwa Milionea. Hivi kama una pesa na ni halali kwanini unakwepa kusema nina pesa na watu wanaoniunga mkono? Be honest EL!
Umempa ukweli wenyewe, ubarikiwe sana.
 
Back
Top Bottom