Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Nafikiri chama kita lipatia ufumbuzi ili swala kupitia vikao vya ndani.
CCM sio kama CDM mgogoro kidongo ndani ya chama wao wanapayuka hadi dunia nzima inajua.

Tatizo la rushwa na ufisadi linatatuliwa na vikao vya ndani ??? Baada ya zoezi la kuvuana magamba kushindwa au vipi Shame on
 
-Siyo siri kwamba wasaka urais wawili wakubwa ndani ya CCM, January Makamba na Edward Lowassa, wamekuwa wakizunguka nchi wakigawa mamillioni ya fedha kwa wananchi ili waungwe mkono katika mbio zao za urais 2015

-Siyo siri kwamba Bw. Makamba Jr. Alikuwa mtumishi wa umma wa kawaida, lakini baada ya muda mfupi, huyu kijana amatokea kuwa na ukwasi mkubwa wa kifedha kiasi kwamba anadhamini vijana, na makundi mengi huku akigawa rushwa za waziwazi. Zanzibar aligawa simu aina za Samsung Galaxy S3 ambazo zinagharimu zaidi ya Tsh 700,000 kwa zaidi ya vijana 200 wa UVCCM. Kwa mahesabu ya juu juu, thamani ya simu 200 ni million 140. Hizi fedha amezitoa wapi January Makamba?

-Naye mzee Lowassa licha ya kwamba jimboni kwake ni masikini wa kutupwa, amekuwa akizunguka nchi nzima akigawa mabillioni makanisani na kwenye misikiti. Hizi fedha naye kazitoa wapi? Hawa watu wanatafuta nini Ikulu? Kwa nini CCM inyamazie tabia za hawa watu? January akumbuke kwamba ubunge wake aliupata kwa hila baada ya babake Mzee Yusuf Makamba kumfanyia hila Mzee. Shelukindo

-Naitahadharisha chama changu CCM kwamba, ikiwa itafanya makosa ya kuwapitisha hawa watu wawili ambao wanazunguka nchi wakigawa rushwa hadharani bila vyombo vya dola kuwahoji, nitafanya maamuzi magumu ya kuongoza uasi ndani ya CCM ili tuwape wananchi njia mbadala ya uongozi, hata kama itamaanisha kuwaunga mkono viongozi safi wa upinzani. Hawa vinara wawili siyo tu wanakiuka miiko na maadili ndani ya CCM, kwa maana kwamba muda wa kampeni bado, kadhalika wanavunja sheria za nchi kwa kugawa rushwa.

-January hajawahi kuchaguliwa kwenye cheo chochote kile hata ubunge, lakini badala ya kufuata njia halali, yeye anaendekeza rushwa huku akimpiga majungu waziri wake pale wizara ya Sayansi na Teknolojia. Natokea jimboni Bumbuli, lakini cha ajabu, Mzee Makamba na Mwanaye wanatangaza jimboni kwamba January Akiwa Rais Tanga itakuwa kama Singapore? Really? Tutafika kweli kwa mwendo huu? Hawa jamaa wanakimbilia ikulu kufata nini?

Weka ushahidi hatutaki umbea umbea hapa
 
Una chuk kama mtoto wa kondoo,ona aibu nan kasema anatafta urais?unaujua umri wa JM? Je kufkia hyo 2015 atakuwa amefikisha umri wa miaka 45?acha chuki za kibwabwa mkuu ukiwa GT pambanua mambo kwa kina,,,,,,,,,afu kama wanagawa rushwa ww kama raia mwema mtaka haki na usawa kawariport takukuru basi ulete uzi hapa na kesi uliowafungulia
 
Mkuu miaka 45 ya nini? Kama hujui miaka siamini kama unajua kwamba hawautaki Urais!!
 
Mkuu Moscow kwa jinsi ya makundi yalivyo kwa hivi sasa ndani ya CCM, CCM isipomeguka mapande mapande kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 basi itadumu daima.

Naona mwanza kuna kura nyingi kwa kuwa wawania Urais wengi ndani ya CCM wamekula xmass jijini Mwanza wakiwa na lundo la wafuasi wao.
 
Last edited by a moderator:
Hii nchi bado ni kichwa cha mwenda wazimu. Hata jambazi lowasa na makamba eti wanataka wawe marais......na tatizo mitanzania mingi bado haina akili wa naweza kuwapigia kura.
Kazi yetu sisi kunyolewa na kila mwenye fedha. Jamani ya kikwete yametutosha sasa tunataka MTU Majibu sio misifamisifa
 
Dogo acha bange. Kama mbege na gongo vinakuyumbisha mpaka akili yako inakosa mwelekeo kakojoe uende kulala.

Makamba na Zitto wapi na wapi?? Ni matahira kama wewe tu ndio wenye kulinganisha Makamba na Zitto.

Mtu yeyote makini anayepambanua siasa za nchi hii kwa kina na weledi wa kiwango kinachokubalika, anafahamu kabisa kuwa Makamba na ZZK they are incomparable!!!

Ukijidanganya kulinganisha Makamba na Zitto ni sawa kwamba unalinganisha mwendo wa basikeli ya miti na jumbo jet airline. Sasa kams siyo bange, gongo, mbege na viroba vinavyokusumbua kichwani ni nini????

Lakini vilevile ni misukule na vibaraka wa dj baba freelady na mzee slaa pekee, ndio wanaoona kwamba ZZK mwanademokrasia anayedai demokrasia harisi kuanzia ndani ya chama mpaka nje ya chama kuwa ana uchu wa madaraka!

Dogo acha kuwa mvivu wa kufikili, ZZK ndio jembe la mkulima, mtanzani masikini anayepuuzwa na CCm vilevile ZZK ndio jembe la kumkomboa mtanzania anayeendelea kudanganywa na wahafidhina, mafisadi wa cdm,watafuna ruzuku, wahuni wapenda wake za watu, wasiojali jasho la mlipa kodi na kuamua kurudisha wapenzi wao kutoka ktk vikao na ziara za kamati kwenda Dubai kula maisha na hawara yake!!!!!!

Dogo,Una akili timamu kweli!!!! Bado haya yote huyaoni? Dogo acha kubwabwaja ungea vitu vya maaana ueleweke -----!!!!!!
Agrrrrrrrrrrrrr mbafu.

Kaka kama ungalikuwa na akili kidogo tu hata kama ya kuku ungalimfahamu zito na tabia zake. Unangia kwa kuchemka kama mafuta ukidhani unawasilisha uhalisia kumbe you are very negative about who is real Zitto. Zito ana sura zaidi ya kumi na ni kigeugeu, msalili, mnafiki, muongo, mwenye ucho wa madaraka, mwenye hila mpaka kufikia njama za kuuwa huku akisingizia ni yeye anawinda na uchafu mwingi ambao hauelezeki kwa kuwa hapa is too public. Zito ni hatari kuliko anavyokuaminisha, unavyosoma maandiko/ matamshi yake na anavyojipambanua. Anajijua yeye mwenyewe, baadhi ya washirika wake wanaoshirikia kutekeleza uovu na ushirikina wake.
 
Hawa wanaohonga wananchi kwa sasa waachwe waendelee na honga hizi ili angalao fedha zinazokwapuliwa kwa wananchi ziwarudie na at the end in mmoja tu ndo atakayechaguliwa. Tusiwakatisj=he tamaa tena tuwapongeze ili ari ya hongo iendelee na maskini wa kijijini wapate nao haki
 
mpaka sasa ina mapande mengi, hawa jamaa -cccccmmmm kutoka 2015 na kushika ikulu kazi sana, naona ule mchezo wa kheri tukose wote unakuja ktk hiki chama, hapa ni suala la muda tu. Wamefikia pabaya sana, hawaaminiani, wanazungukana, wanaangamizana, utu hakuna, kila mtu ana lake. Angalia hata pale bungeni jinsi wabunge wake wanavyoongea ni aibu tupu. Wamesahau kabisa ilani yao ya uchaguzi badala ya kutekeleza ilani wanalumbana ni aibu tupu kwa watu wazima
Mkuu Moscow kwa jinsi ya makundi yalivyo kwa hivi sasa ndani ya CCM, CCM isipomeguka mapande mapande kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 basi itadumu daima.

Naona mwanza kuna kura nyingi kwa kuwa wawania Urais wengi ndani ya CCM wamekula xmass jijini Mwanza wakiwa na lundo la wafuasi wao.
 
Mkuu miaka 45 ya nini? Kama hujui miaka siamini kama unajua kwamba hawautaki Urais!!

Miaka 41 najua kwa mujbu wa katka ya JMT swal langu n je atakuwa kafka hapo?jib n hapana hvo basi nkianza na ww shobo kali waambie wenzio waache chuk za kikondoo wafanye yanayowahusu,tukiendekeza chuk hz TZ itakuwa nchi ya mapoyoyo tuuuu
 
hili ni balaa aisee,makamba nae anataka urais?kwa uzoefu upi alionao kisiasa? haya bwana kila la heri bwana makamba jr
 
Mh.Lowassa na January Makamba wote hawa walikuwa kambi moja ndani CCM na walifanikisha kwa njia zozote zile kumweka Jakaya Kikwete Madarakani mpaka wa Leo.

Sasa wote wawili wanapita huku na kule kujitengenezea makundi ndani na nje ya chama.

Makanisani na Misikitini wameingia nakutoka na wameacha ushawishi pamoja na Minoti kibao.

Boda Boda nao tayari wamefikiwa na kila mmoja wao na kuwamwagia ahadi kabambe.

Ila Nitumie nafasi hii kuwaonya madriver Boda Boda wasije wakageuzwa kuwa Double Double badala ya kubakia Boda Boda na wakatuletea Machafuko na Umwagaji wa Damu Usio wa Lazima Ndani Ya Tanzania Yetu.

Nataka kusema wazi January Makamba kuanza mbio za kuusaka Urais mapema hili sio jambo la Bahati mbaya.

Ni mkakati uliosukwa kwa ustadi sana wasio makini wanatoka kavu ukoko bila mchuzi.

Nitawaonyesha kwa kuwabomolea chumba kidogo tu.

Hii ndio kazi ya Makamba Jr :-

1.Kumdhoofisha nguvu Lowassa popote pale alipojijenga ndani na nje ya chama.

2.Kuwagawa wanachama na wapambe wa Eddo ili iwe kazi rahisi kumtengenezea njia Mteule ajaye ndani ya CCM hasa kwenye uchaguzi wao wa kumpata mpeperusha Bendera ya CCM bila ya kutumia Jasho jingi sana.

Kwanini wamefanya hivi.
Wanahofia Lowassa akivuka kuwa mteule wa chama na akafanikiwa kuupata Urais watakuja kushughulikia mmoja baada ya mwingine.

Pia Mahesabu yao yanasimama zaidi kwenye Umri.

Wanaona Makamba bado ana umri mdogo ukimlinganisha na Lowassa,yeye ni Kijana Mwororo hata akikosa kuteuliwa ndani ya chama cha mapinduzi 2014 kwake hakuna madhara kama kwa Mh.Lowassa.

Wanajua wazi Lowassa hana Ujanja wa kwenda na kiu ya kuutaka Urais kwa mwendo wa Miaka Ishirini (20) Ijayo,

Wakifanikiwa kumharibia 2014 ndio basi.

Kama mnazifutilia siasa za jirani zetu Kenya Utagundua Uhuru na Ruto Wamejipanga kuachiana Madaraka umri pia umezingatiwa.

Inavyoonekana Ndani ya CCM mpango ni huu Mh.Lowasaa na J.Makamba Jr 2014 wakose wote atawekwa ambaye hakutarajiwa sanana wengi ili kupambana na CHADEMA.

Endapo atahimili mikiki mikiki ya CHADEMA Mgombea wao na Kushinda Basi akifanikiwa kumaliza miaka kumi (10) Ndiposa J.Makamba Gamba liliokomaa kwa wakati huo naye Ashike Dola.

Huu ni mkakati wao Makamba na wenzake Mwenye kupuuza na apuuze.

Mh.Lowassa kama kweli uko makini hapa ndipo Pakuangalia. Uliwahi Kusikika unasema WAKIMWAGA UGALI WEWE UTAMWAGA MBOGA

Hapo ndipo tutakapojua MBIVU na MBICHI ndani ya CHAMA CHA MAPINDUZI. Na Msisahau wote kuwa, HASIRA YA MKIZI NI FURAHA YA MVUVI.

Nashauri Mh.Lowassa achangamke mapema 2014 kumwaga mboga.

Ukifanikiwa kuingia mwaka mpya wa 2014 Usijivune maana sio kwa nguvu wala kwa uwezo wako,WEWE JIFUNZE KUWA NA SHUKRANI KWA MUNGU.
 
Inawezekana ukawa sahihi kwani sion kama makamba kwss ana sifa/uzoefu za kuwa rais,yawezezekana ikawa nai maandalizi( long term plan )
 
Nafikiri chama kita lipatia ufumbuzi ili swala kupitia vikao vya ndani.
CCM sio kama CDM mgogoro kidongo ndani ya chama wao wanapayuka hadi dunia nzima inajua.
Ccm hamna ujasiri wa kuwajibishana ,acha longolongo yako.Chadema hawaangalii sura ya mtu.Paka shume wewe,nenda Lumumba kachukue buku 4 sasa.
 
Dogo acha bange. Kama mbege na gongo vinakuyumbisha mpaka akili yako inamkosa mwelekeo kakojoe uende kulala.

Makamba na Zitto wapi na wapi?? Ni matahira kama wewe tu ndio wenye kulinganisha Makamba na Zitto.

Mtu yeyote makini anayepambanua siasa za nchi hii kwa kina na weledi wa kiwango kinachokubalika, anafahamu kabisa kuwa Makamba na ZZK they are incomparable!!!

Ukijidanganya kulinganisha Makamba na Zitto ni sawa kwamba unalinganisha mwendo wa basikeli ya miti na jumbo jet airline. Sasa kams siyo bange, gongo, mbege na viroba vinavyokusumbua kichwani ni nini????

Lakini vilevile ni misukule na vibaraka wa dj baba freelady na mzee slaa pekee, ndio wanaoona kwamba ZZK mwanademokrasia anayedai demokrasia harisi kuanzia ndani ya chama mpaka nje ya chama kuwa ana uchu wa madaraka!

Dogo acha kuwa mvivu wa kufikili, ZZK ndio jembe la mkulima, mtanzani masikini anayepuuzwa na CCm vilevile ZZK ndio jembe la kumkomboa mtanzania anayeendelea kudanganywa na wahafidhina, mafisadi wa cdm,watafuna ruzuku, wahuni wapenda wake za watu, wasiojali jasho la mlipa kodi na kuamua kurudisha wapenzi wao kutoka ktk vikao na ziara za kamati kwenda Dubai kula maisha na hawara yake!!!!!!

Dogo,Una akili timamu kweli!!!! Bado haya yote huyaoni? Dogo acha kubwabwaja ungea vitu vya maaana ueleweke -----!!!!!!
Agrrrrrrrrrrrrr mbafu.[OTE]let me just reserve my comments.....fool
 
Back
Top Bottom