Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

ushauri wako ni mzuri sana lakini ccm ni sikio la kufa

tatizo ccm inaongozwa na mambumbu unless otherwise kuna baadhi ya watu kule mi mwenyewe nawaaminia,chama kinahitaji kupata dereva mzuri amabacho kwa sasa hivi hakiwezekani kupata dereva huyo kutokana na kukithiri kwa rushwa
 
Mi yangu macho, vijana wanasubiri kwa hamu kuandikishwa ili waweze kupiga kura, nitapigia cdm kura mpaka siku ya kufa
 
Ndugu Lowasa hebu aone aibu,hizo fedha anazo gawa kila siku zingekuwa zake,anajisikiaje akifika jimboni kwake anakuta wapiga kura wake hawana maji zahanati hakuna nk,jamani toka ameanza kugawa fedha Monduli si ingekuwa zaidi ya DUBAI,tuache unafiki kuna jambo.
 
Hii nchi bado ni kichwa cha mwenda wazimu. Hata jambazi lowasa na makamba eti wanataka wawe marais......na tatizo mitanzania mingi bado haina akili wa naweza kuwapigia kura.
Kazi yetu sisi kunyolewa na kila mwenye fedha. Jamani ya kikwete yametutosha sasa tunataka MTU Majibu sio misifamisifa

vijana wengi tumeaminishwa lowasa anafaa na wengi tumeamini hivyo ni vijana wachache wanaoujua ukweli ambao wanapenda kudadisi ndo wanaweza kumjua lowasa ni nani hasi,otherwise tufanye juhudi za makusudi kuelezea upande wa pili wa huyu mmwaga hela,kuanzia kusign mikataba ya kifisadi,kuelezea alivyotumika na kutumia nafasi ya uwaziri mkuu vibaya kumnufaisha yy
 
Nafikiri chama kita lipatia ufumbuzi ili swala kupitia vikao vya ndani.
CCM sio kama CDM mgogoro kidongo ndani ya chama wao wanapayuka hadi dunia nzima inajua.
Kwa kuhakikisha viongozi nao wanapatiwa fungu lao ili hao kina january wapitishwe. .. Teh eeh.
 
Nawapongeza CDM kwa kuliona hilo mapema na kuwafukuza MM na wenzake!CCM magamba yamukua magumu kutoka!
 
Kwa mzee Lowasa sina 'comment' lakini kwa huyu dogo labda anatumia nafasi yake ya uwaziri maana pana makampuni mengi tu ya simu hapa nchini.
 
Acha wafu wazikane wenyewe.Ila wenye akili timamu watatumia macho matatu kwenye box la kura 2015
 
Jana Makamba kagawa pikipiki 1700×300000=510,000,000 million mia tano na kumi. Hizi pesa ametoa Lowassa.Makamba hana ubavu wa urais hapa anataka kugawa tu kura ktk kinyang'anyiro cha uteuzi wa urais kwenye chama cha majambazi. KIKWETE hawezi kusema kitu kwa Lowassa kwani njia hii ya rushwa ndio iliyomweka madarakani 2005. Na takururu polisi wamewekwa na Lowassa na Kikwete.

Hapa ni vijana wenyewe kuamka, pokea pikipiki, simu chochote kile atacholeta Lowassa na Makamba kwani hatawafanya chochote kuwafunga au kuwapeleka mahakamani hawezi. Kikubwa kadi yako ya upigaji kura USIUZE KWA BODABODA KWANI ITAKUCHUKUA MIAKA 10 UKITESEKA WAKATI BODABODA itakufia baada ya miezi miwili au siku io io uwezi jua.

WATANZANIA THIS TIME HAMKENI MSIKUBALI KUDANGANYWA NA WENYE FEDHA. MWAKA 2015 WAJUE KUWA WATANZANIA WAMEAMKA. WAMECHOKA KUGEUZWA VICHWA VYA WENDAWAZIMU.

Kula ccm kura yako .................
 
Makamba sure anamaono nashawishika kusema hivyo kama yupo anabisha aniulize kwa nini makamba tupo nyuma yako.
 
Lowassa na Makamba Jr, ni timu moja kwa nyie ambao hamtambui. Lowassa anamkubali sana huyo dogo and visevesa.
 
Tulimuani sana mh.raisi aliopo tukamchagua kwa asilimia mia,kwamba angeweza kufukua ufisadi na uozo wote ndani ya serekali ya chama chake na kukisafisha kabisa,lakini ameshindwa kabisa kufanya hivyo,kila akigusa mahali anajikuta hata yeye alishiriki kwa namna moja au nyingine alivyokuaga ni waziri.
Alivyoanza kashkash mwanzoni,watu wengi wakasema hizo ni nguvu za soda,hata pia wengi walitabiri huo ni mwanzo tu huwa unamwisho wake,na kweli tumeona mwisho wake.
Mimi kwa maoni yangu,sasa tuwe makini sana kuchagua raisi ajayo,tusikubali tena kudanganyika kwa ahadi nyingi,pia nasema kuwa kama tulimuamini huyu kuwa angeweza kufuata nyayo za baba wa taifa na hakufanya hivyo,basi hakuna raisi yeyote ajao kutoka c.c.m atafanya mabadiliko katika nchi hii,tuchague raisi ajayo kutoka chama kingine tuangalie,kama hatatufaa naye tutamtoa,hawa wanaozunguka kwa kumwaga pesa,waacheni waangaike lakini tusichague hata mmoja,tukifabya mdhaha tena tutapigwa miaka kumi tena tukiangalia mfisadi wakipeta.
 
Wewe ni CCM na UNAULIZA? Haukusoma HABARI ya kuwa Waziri wa Madini Dr. Muhongo Amekwapua SH. Million 400 Unadhani zinakwenda kwa Wananchi???
Ni prof sio Dr.
 
Kuna mtafaruku mkubwa kati ya EL na JM. JM ameshastuka kwamba ngamia hawezi kuingia kwenye tundu la sindano hivyo basi JM ameamua aende solo kuponya mkate wake. Kosa la JM ni kutumia mbinu za boda boda na kugawa ela, mbinu hizi zitamgharimu.
 
wanawekeza kwenye vichwa vya wapuuzi, na baadaye watarejeshesha wanachokiwekeza kupitia wapuuzi hao hao

-Siyo siri kwamba wasaka urais wawili wakubwa ndani ya CCM, January Makamba na Edward Lowassa, wamekuwa wakizunguka nchi wakigawa mamillioni ya fedha kwa wananchi ili waungwe mkono katika mbio zao za urais 2015

-Siyo siri kwamba Bw. Makamba Jr. Alikuwa mtumishi wa umma wa kawaida, lakini baada ya muda mfupi, huyu kijana amatokea kuwa na ukwasi mkubwa wa kifedha kiasi kwamba anadhamini vijana, na makundi mengi huku akigawa rushwa za waziwazi. Zanzibar aligawa simu aina za Samsung Galaxy S3 ambazo zinagharimu zaidi ya Tsh 700,000 kwa zaidi ya vijana 200 wa UVCCM. Kwa mahesabu ya juu juu, thamani ya simu 200 ni million 140. Hizi fedha amezitoa wapi January Makamba?
attachment.php


-Naye mzee Lowassa licha ya kwamba jimboni kwake ni masikini wa kutupwa, amekuwa akizunguka nchi nzima akigawa mabillioni makanisani na kwenye misikiti. Hizi fedha naye kazitoa wapi? Hawa watu wanatafuta nini Ikulu? Kwa nini CCM inyamazie tabia za hawa watu? January akumbuke kwamba ubunge wake aliupata kwa hila baada ya babake Mzee Yusuf Makamba kumfanyia hila Mzee. Shelukindo

-Naitahadharisha chama changu CCM kwamba, ikiwa itafanya makosa ya kuwapitisha hawa watu wawili ambao wanazunguka nchi wakigawa rushwa hadharani bila vyombo vya dola kuwahoji, nitafanya maamuzi magumu ya kuongoza uasi ndani ya CCM ili tuwape wananchi njia mbadala ya uongozi, hata kama itamaanisha kuwaunga mkono viongozi safi wa upinzani. Hawa vinara wawili siyo tu wanakiuka miiko na maadili ndani ya CCM, kwa maana kwamba muda wa kampeni bado, kadhalika wanavunja sheria za nchi kwa kugawa rushwa.

-January hajawahi kuchaguliwa kwenye cheo chochote kile hata ubunge, lakini badala ya kufuata njia halali, yeye anaendekeza rushwa huku akimpiga majungu waziri wake pale wizara ya Sayansi na Teknolojia. Natokea jimboni Bumbuli, lakini cha ajabu, Mzee Makamba na Mwanaye wanatangaza jimboni kwamba January Akiwa Rais Tanga itakuwa kama Singapore? Really? Tutafika kweli kwa mwendo huu? Hawa jamaa wanakimbilia ikulu kufata nini?
 
kaka kama ungalikuwa na akili kidogo tu hata kama ya kuku ungalimfahamu zito na tabia zake. Unangia kwa kuchemka kama mafuta ukidhani unawasilisha uhalisia kumbe you are very negative about who is real zitto. Zito ana sura zaidi ya kumi na ni kigeugeu, msalili, mnafiki, muongo, mwenye ucho wa madaraka, mwenye hila mpaka kufikia njama za kuuwa huku akisingizia ni yeye anawinda na uchafu mwingi ambao hauelezeki kwa kuwa hapa is too public. Zito ni hatari kuliko anavyokuaminisha, unavyosoma maandiko/ matamshi yake na anavyojipambanua. Anajijua yeye mwenyewe, baadhi ya washirika wake wanaoshirikia kutekeleza uovu na ushirikina wake.
wewe upo kundi gani kati ya hayo uliyoyainisha
 
Kikwete ameshindwa kumpa hata uwaziri leo anataka kua raisi..
 
Back
Top Bottom