Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Nafikiri chama kita lipatia ufumbuzi ili swala kupitia vikao vya ndani.
CCM sio kama CDM mgogoro kidongo ndani ya chama wao wanapayuka hadi dunia nzima inajua.

Kweli wewe ni mvivu wa kufikiri kama avatar yako inavyoonyesha.
Pole kwa fikra mgando!
 
Si siri tena kwamba bwana Lowassa anausaka urais kwa udi na uvumba. Anamwaga millions of money makanisani na misikitini. Ukija kwa Makamba, ukamcheki vizuri unagundua kuwa kijana ana kiu kuu ya urais na mahali alipofikia, yuko tayari kunywa hata mkojo(rushwa) ili afikie malengo. Juzi amemwaga simu za gharama kwa vijana huko Zanzibar wakati Mwanza ameahidi pikipiki za millions of money kwa vijana. Style zao wote wawili hazitofautiani. Ni watu wenye lengo moja hawa na kamwe ccm msijiloge kuamini kwamba E.L na J.M ni mahasimu. Ninachokiona mimi ni formation ya game ambayo imesukwa kiufundi. Lowassa alichofanya ni kumtumia J.M kwakuwa ni kijana makini na ana ushawishi kwa vijana. Kitakachotokea Mwishoni J.M atampisha Lowassa na kama Lowassa upepo hautamwendea vizuri basi awe amempachika Rais wake J.M. Kwa ccm hiyo ni game hatari msipochukua hatua hao jamaa wanawaulieni chama asubuhiasubuhi. Ni ushauri tu nimeutoa bure kwenu!. Mnaweza kuupuuza ama kuufanyia kazi. CCM oyeeeee+peoplesssss poweeeeeeeeer+hakiiiiiiiiiiiiiii!

CCM kikifa si ndio afadhali kwenu?
 
Wenye samsung humu ndani wengi!
2015 CDM itashinda uchaguzi walie tu.Sanduku za kura zitalindwa hadi kieleweke.
 
jamani watanzania wa sasa sio wajinga wanajua kila kinachoendelea kula rushwa zao sio tatizo si wanazileta wenyewe bhana tunakula tu ila fainali 2015 wanajikaanga wenyewe imekula kwao:cool2::crazy:
 
Nimepata tetesi kwamba January anafadhiliwa na shemeji yake Rostam Azizi?
Kama kweli basi tunalo. Ifike hawa jamaa mafisadi waanze kupigwa mawe
mwanza wananchi wame thubutu huko dar ambako mnalala nao mnaishia kuwapisha na ving'ola vyao
 
-Siyo siri kwamba wasaka urais wawili wakubwa ndani ya CCM, January Makamba na Edward Lowassa, wamekuwa wakizunguka nchi wakigawa mamillioni ya fedha kwa wananchi ili waungwe mkono katika mbio zao za urais 2015

-Siyo siri kwamba Bw. Makamba Jr. Alikuwa mtumishi wa umma wa kawaida, lakini baada ya muda mfupi, huyu kijana amatokea kuwa na ukwasi mkubwa wa kifedha kiasi kwamba anadhamini vijana, na makundi mengi huku akigawa rushwa za waziwazi. Zanzibar aligawa simu aina za Samsung Galaxy S3 ambazo zinagharimu zaidi ya Tsh 700,000 kwa zaidi ya vijana 200 wa UVCCM. Kwa mahesabu ya juu juu, thamani ya simu 200 ni million 140. Hizi fedha amezitoa wapi January Makamba?
attachment.php


-Naye mzee Lowassa licha ya kwamba jimboni kwake ni masikini wa kutupwa, amekuwa akizunguka nchi nzima akigawa mabillioni makanisani na kwenye misikiti. Hizi fedha naye kazitoa wapi? Hawa watu wanatafuta nini Ikulu? Kwa nini CCM inyamazie tabia za hawa watu? January akumbuke kwamba ubunge wake aliupata kwa hila baada ya babake Mzee Yusuf Makamba kumfanyia hila Mzee. Shelukindo

-Naitahadharisha chama changu CCM kwamba, ikiwa itafanya makosa ya kuwapitisha hawa watu wawili ambao wanazunguka nchi wakigawa rushwa hadharani bila vyombo vya dola kuwahoji, nitafanya maamuzi magumu ya kuongoza uasi ndani ya CCM ili tuwape wananchi njia mbadala ya uongozi, hata kama itamaanisha kuwaunga mkono viongozi safi wa upinzani. Hawa vinara wawili siyo tu wanakiuka miiko na maadili ndani ya CCM, kwa maana kwamba muda wa kampeni bado, kadhalika wanavunja sheria za nchi kwa kugawa rushwa.

-January hajawahi kuchaguliwa kwenye cheo chochote kile hata ubunge, lakini badala ya kufuata njia halali, yeye anaendekeza rushwa huku akimpiga majungu waziri wake pale wizara ya Sayansi na Teknolojia. Natokea jimboni Bumbuli, lakini cha ajabu, Mzee Makamba na Mwanaye wanatangaza jimboni kwamba January Akiwa Rais Tanga itakuwa kama Singapore? Really? Tutafika kweli kwa mwendo huu? Hawa jamaa wanakimbilia ikulu kufata nini?

Lowasa anafaa achana na mawazo mgando jamani mnataka kila m2 awe masikini kama nyinyi? acheni roho za kwa nini ni kambi gani isiyo na mafisadi? msiongee vi2 hakuna data nyinyi mambo ya kusikia si ya kutemea nayo mtaani nyny wanafiki
 
Kuna mtafaruku mkubwa kati ya EL na JM. JM ameshastuka kwamba ngamia hawezi kuingia kwenye tundu la sindano hivyo basi JM ameamua aende solo kuponya mkate wake. Kosa la JM ni kutumia mbinu za boda boda na kugawa ela, mbinu hizi zitamgharimu.

Mkuu, hii siyo kweli. Makamba Jr. Ni pandikizi la mafisadi, RA na EL. Wao ndio wafadhili. nimepata report kali sana na punde ntaimwaga jukwaani
 
Haka kadogo kwanza niweke wazi ,mpaka leo sijawahi kumuona Makamba kama mtu anayefaha kuwa katika hiyo nafasi ukiachia kubebwa bebwa na jina la familia,lakini pili huyu dogo ni mzigo uliobaki CCM na atawasumbua kwasababu ana tabia kama za Zitto,wote ni watu wa uchu na wako radhi kufanya lolote na ndo walivyokuwa wakijiimarisha kwa pamoja sema sasa mwenzie CDM wameshtuka na kumshughurikia ..nawapeni pole CCM kwani majanga mnayo mengi na hizi pesa zitawagharimu na siku si nyingi mjiandae kumpokea na Zitto

Makamba na Lowassa majina yao yatakatwa raound ya kwanza. Waacheni waendelee kugawa pikipiki. Vijana wana shida nazo sana
 
Hivi mtu kama makamba aje awe raisi? hahahaaaaaaaaaaaaa! it will be a shame to all tanzanias! haingiii akilini mtu aliyefeli hadi sec. leo anawania uraisi? Mh! Mh! Rostam anawadanganya mno mno!
 
Lowasa anafaa achana na mawazo mgando jamani mnataka kila m2 awe masikini kama nyinyi? acheni roho za kwa nini ni kambi gani isiyo na mafisadi? msiongee vi2 hakuna data nyinyi mambo ya kusikia si ya kutemea nayo mtaani nyny wanafiki

Kwa mtazamo wangu binafsi tuachanae na UNAFIKI sioni Rais bora ajaye ZAIDI ya Lowasa otherwise mna lenu jambo
 
KWANINI LOWASSA ANATUMIA FEDHA NYINGI KWENDA IKULU;

"Mkimuona mtu anaitafuta Ikulu kwa pesa muogopeni kama Ukoma. Mimi nimekaa Ikulu miaka 25, ikulu sio mahali pa kukimbilia" Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Nimeitafakari kauli hiyo siku nyingi sana, lakini leo nimeona niizungumzie kwa kirefu kutokana na mambo yanayoendelea hivi sasa Nchini kwetu. Leo nataka nimzungumzie kidogo Mwanasiasa NGULI na mwenye roho ya Chuma, Mtuhumiwa namba moja wa Ufisadi ndani ya Chama cha Mapinduzi, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa Kashfa ya Ufisadi ya Richmond na Mwanasiasa Kinara wa kumwaga pesa ili aende Ikulu, Ndugu Edward Ngoyai Lowassa.

Nimeskia habari kuwa bwana huyu Mwenye Utajiri wa kutisha usiojulikana chanzo chake (Hii ni kwa mujibu wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere) amegawa Shilingi Laki mbili mbili (200,000/=) kwa kila Katibu wa CCM wa Wilaya na Mkoa katika wakati huu ambao Mkutano maalum wa Mafunzo kwa Makatibu wa Chama hiki unaendelea huko Mkoani Dodoma. Ukipiga hesabu ya idadi ya Makatibu hao kwa Mikoa na Wilaya zote Nchini utagundua kuwa "Mzee huyu wa Mvua za Kutengeneza za Thailand" ametoa jumla ya pesa za Kitanzania Shilingi Milioni Thelasini na Tano na Laki nane (35,800,000=).


Katika harakati hizo za kutangaza nia mtu huyu aliyena ukwasi usiojulikana chanzo katika jamii na piga Black Deal maarufu ametenga kiasi cha shs 78 Billion kuwa ajili ya Nia hiyo, katika fedha hizo ambazo hivi karibuni alikodisha vijana wengi kwenda Dodoma huku wakiongoza na kada mpanga mikakati wake na raia wa kisomalia anaitambulika kwa jina la HUSSEIN BASHE ambaye ndio alikuwa na fungu hilo mathubuti na pia alikuwa anagaw fedha kwa vijana wake kiasi cha posho sh.100,000 hadi 300,000 kutokana na umbea au habari ambazo mtu analeta dhidi ya wahasimu wake wa kisiasa ktk Nia ya kuwa Raisi wa Awamu ya TANO wa Jamuhuri wa Tanzania.

Pia hayo yote yalifanyika huku baraza kuu la vijana likiendelea hapo mjini Dodoma.

Pia LOWASSA kupitia kada wake maarufu raia wa kisomalia Ambaye ndie mkurungezi mkuu wa magazeti ya NEW HABARI LTD(2006) ambaye ndio CEO na kwa mantiki hiyo amenunua magzeti ya mtanzania kama chombo cha habari chenye interest kubwa nae,katika harakati hizii..pia kutokana na mjumbe wa bodi ya Tanzania Daima kuwa karibu na Lowassa jambo ambalo kwa sasa kuna CONSPIRACY dhidi ya kumuandika na kutawala vyema chombo hicho cha habari kikuu cha Chadema lengo ni kutimiza ndoto hewa aliyonayo Bwana Lowassa.

Matumizi ya Fedha hizo ni pamoja na kuwanunua vijana waweze kuimba wimbo wa jina lake kila mahali na kuwahadaa viongozi wa dini. Kujaribu kutumia hela nyingi kusafisha uovu wake.Bahati mbaya mh Raisi kikwete amshtukia Bahati Nzuri.

kama kweli
Lowassa Ngoyai Edwardanapesa na anaona haja ya kuwassaidia Watanzania kwa nini asifanye kama Mkono alivyokua anafanya kule kwetu Musoma anajenga Shule anawamilikisha Wananchi, au basi ajenge zahanati agawe kwa Wananchi ili iwe Msaada kwa jamii yote kuliko kulenga Makundi flani anayoona yanafaida kwa Mustabaki wake.

Kwa taarifa hizo tujiulize maswali je anaenda ikulu kufanya nini? Je kuna biashara gani ikulu? Je Anapotumia hela atazirudishaaje?


TUTAFAKARI KWA KINA NA DHANA YA UADILIFU KATIKA TAIFA!!!!

 
Sijui dini yenu yanguu inasemamema yanchi dunia n mbinguni mahesabu
 
CCM inapita katika tanuru la moto. Ikitokea kwamba Lowassa hajapitishwa sijui nini kitatokea, amekamata kila mahala kuanzia makanisani, misikitini, ndani ya CCM hadi wapinzani.
 
Aogopwe kama ukoma huyo.

Aogopwe kwa nini ? Akili za kuambiwa Changanya na zako usikumbilie kukariri Story za kupikwa na Wapambe wa Membe ambaye ndiye anatumia Mapesa mengi tena Mengi ya Ufisadi na Mengine ni Mapesa ya Marehemu Gadafi ambayo ameyaficha kwenye Mahandaki kwake akiogopa kuyaweka Benk Maana Walibya watatakamata na Pengine kumfikisha mahakama ya kimataifa.

Membe ndiye anayetumia Pesa nyingi kununua njia ya kuelekea ikulu kwani amewekeza kwenye kuwachafua wapinzani wake kwenye mitandao hususani Lowasa, kajisahau Kuwa yeye Pia ni Fisadi mkubwa tena Mchuma Dhambi kwani Kile kipapai alichompiga Barozi wa Libya hadi akajiua mwenyewe hakijasahaulika na roho ya Balozi huyo bado inadai Pesa zake za Mgao ktk ya Mapesa ya Marehemu Gadafi ndiyo Maana Membe Hana Mvuto wa Kisiasa hata akiwanunua wapiga kura watakula pesa zake tu lakini mwisho wa siku ataambulia patupu.
 
Back
Top Bottom