Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Kama Lowassa ni msafi

1.Kwa nini alifukuzwa ukurugenzi wa AICC kwa kujilimbikizia mali ?,alifukuzwa na Juliasi Nyerere.

2.Kwa nini alijiuzulu kwa sakata la Richmond ambalo nyie mnadai hakuhusika,na kwa nini ameendelea kuficha ukweli hadi sasa kama ni mtu anayetakia mema taifa hili? mbaya zaidi kwa unafiki wake alidai anajiuzulu kwa sababu watu wanautaka uwaziri mkuu wake.

3.Atakuwaje mkombozi wa pili na wakati amekuwapo kwenye serikali kwa miaka mingi sana na hatujaona "something so special" from him?.Afadhali hata magufuli tunaona impact kila sehemu anayoenda.

4.Ni maamuzi magumu gani ambayo mnasema Lowassa ameyafanya? Usitaje kujiuzulu kwa sababu hayo pia ni maamuzi magumu kama ya jambazi anayeenda kuvunja nyumba ya mtu.Amejiuzulu ili kuendelea kulindana na aidha wezi wenzake au wazembe wenzake

Until unijibu maswali haya kiufasaha,ntahamia rasmi kwenye kambi ya Lowassa.
Gracious you nailed it

BRAVO!
 
Last edited by a moderator:
Nafanya marejeo tuu kufuatia tetesi ya possibility ya defection!, we don't want tragedy!.

Pasco
pole sana pasco , nawahurumieni sana wewe , zitto , ocampo four , hamis mngeja na serukamba , usiniulize kwanini , nimeamua kuwahurumia tu .
 
maneno ya mwl.nyerere yasije fanya waTZ wakakosa raisi bora ni wazi mh.edward lowasa alitilewa kafara na serikali makusudi na kuahidiwa kusafishwa kiasi kwamba amekua akitumia nguvu za ziada kwake binafsi ili kwenda kuqeka mambo sawa,na hili la kuji udhuru ili kutii dhana ya uwajibikaji limeshaonekana sasa ni jambo bovu kabisa na ndo mana kina muhongo ilikua ngumu kutokana na kutupiwa kila hila mbovu,na ndo mana democrasia ya tz bado ipo chini sanaaa.ila mwisho qa yote kila kitu kitawekwa wazi mwaka huuu na nikimuangalia bwana EL ana mengi kayafumba ni jambo la kungoja muda tu

hahahahah i see
 
Bora EL ambae utajiri wake kidogo anawapa maskin kuliko akina chenge ambao kila deal wamo lakn kuchangia maabara,kanisa,saccos ni shidaaaaa

a thiefa is always a thief

katika wizi wake unajua ni binadamu wangapi wameumia .....
ifike mahali tujitambue tujue haki zetu si ushabiki maandazi wa kypapatika na kanga na tsht wakati mwenzako anamahela tsht zinakusaidieni nn ingepaswa wafilisiwe na bakora za makalio kutumikia kifungo....
 
Hivi mtu anapataje umasikini uliopindukia?????
 
Lowassa ni Tajiri sana hata kabla hajawa waziri mkubwa. Nitashangaa kama tajiri anaulizwa kuwa pesa anatoa wapi. Tatizo la Lowassa na baadhi ya viongozi wengine matajiri ni pale wanaposhindwa ku declare interests zao in time. EL anamiliki ma estate nyingi hapa Arusha, ana Shares kubwa kwenye makampuni ya utalii kama vile Leopard nk.
Kumbe
 
Jamii01, fuatilia thread za Lowassa humu utaziona mpaka mali zake zimeorodheshwa!. Lowassa ni tajiri wa ukweli aliyepata mali zake zote kihalali na ndio maana amezisajili zote kwa jina lake na la mkewe Rejina!.

Ila hakuna ubishi CCM imegubikwa na ufisadi hali inayopelekea kila yeyete mwenye chochote kitu kuonekana fisadi.

Lowassa ni miongoni mwa wanaitwa mafisadi wakuu kufuatia kukubali kulibeba lile zigo kubwa la Richmond ili kumnusuru best wake na chama chake na aibu ya mwaka, hivyo yeye kuchafuka kwa kukubali kujitwisha msalaba wa ukombozi na salama ya CCM!.

Anachokifanya huko makanisani na kwenye michango mbalimbali ni kuonyesha uwezo wake kwenye kitu kinachoitwa mass mobilization kwa ajili ya kujiletea maendeleo, kitu ambacho JK ameshindwa kabisa!.

Hilo la kuandikwa magazetini, na kwenye vyombo vya habari, ni kufuatia EL kuwa na mvuto wa ajabu uliotoka kwa Mungu. Kila asemalo linamantik kwa hali ilivyo sasa!. Lowassa ni photo genic!, akipigwa picha anapendezea!, akiongea anavutia kumsikiliza!, na kikubwa zaidi yeye sio mtu wa maneno maneno na vitendo sifuri kama JK, yeye ni mtu wa maneno mafupi na vitendo virefu.

Wakuu wengi waliopo wakisikia JK atatembelea mahali, huandaa taarifa safi, mkuu akifika, akishasomewa taarifa, hupiga makofi na kuendelea na ziara!. Enzi za Lowassa akishasomewa taarifa huipokea na kuelekea physically kuyaangalia hayo yaliyozungumziwa!. Hivyo watu wakisikia JK anakuja, hukaa miguu juu, ila wakisikia ni Lowassa!, kijasho huwa kinawatoka maana jamaa hakubali kabisa longo longo yoyote!.

Ni kufuatia utendaji huu ndio maana mimi na wenzangu wachache humu jukwaani, tumeamua kujitolea kumsafisha Lowassa na ule uchafu wa Richmond, tunamtaka alitue hilo zigo amkabidhi mwenyewe, na yeye ndie ateuliwe kuwa mgombea wa CCM tumpigie debe, aingie Ikulu!.
Baada ya Edward Lowassa kusifiwa na rais Magufuli kuwa ni Superman, namdurufu kidogo Lowassa kwa kujikumbusha niliwahi kusema nini kuhusu mtu huyu.
P
 
Kuanzia leo mpaka atakapo pumzishwa kwenye makao yake ya milele, as my tribute to this fallen hero, namuaga kwa kujikumbusha niliwahi kusema nini kumhusu.

RIP Shujaa Edward Lowassa

Paskali
 
bado nawe una mawazo mgando kuwa n2 akishateuliwa kugombea urais kwa tiketi ya ccm bac ataingia ikulu??? watu walikua wanamhofia magufuli tu pale ccm ndo angalau angekua na ubavu wa kucmama na Dr wa ukweli 2015... naye ndo hivyo tena kishaanza kuboronga kwa kauli zake za kupiga mbizi. Endelea kumsafisha Lowasa at the end of the day u'll find that ur efforts=zero
Aisee wewe ulikua mbele ya muda!
 
Najiuliza na kukosa majibu Mh. Lowassa si mfanyabiashara,zaidi ya kuwa mbunge, nimejionea siku za hivi karibuni katika vyombo vya habari akichangia mambo mengi hasa katika miradi ya maendeleo na katika taasisi binafsi na zamakanisa. Huyu mweshimiwa pesa anazitoa wapi?

Je, alikwisha tangaza mali zake hadharani? Na kipato chake kiko vipi? Alipokuwa waziri katika awamu ya tatu kwa nini akufanya hivyo? Na alipokuwa Waziri Mkuu kwa nini alishidwa kufanya hivyo? Na kwanini safari zake na hotuba zake zinapewa umuhimu mkubwa katika vyombo vyetu vya habari?

===============
Utetezi wa Lowassa:
Huyu si alikuwa mfugaji na wafugaji wengi wasoni kawaida huwa wanakuwa na pesa kuzidi hata wafanyabiashara wakubwa? Tatizo liko wapi?

Yaani hii nchi ni invaders tu ndiyo wanaotakiwa kuwa na pesa; wazawa hapana.

Mzawa ukionekana una pesa, aidha unatekwa au unazushiwa maskendo yasiyo na maana ili uhamishie miradi yako kwingine, au unazushiwa skendo uachie mamlaka ya kisiasa, kama unayo

Kipindikile cha JK, RA mwishowe alilazimika kuhamishia miradi yake Kenya, na nilimuona alianza kurudi tena wakati wa Hayati JPM, ila kwa sasa simuoni tena

Mo alitekwa na sijui kama naye baadhi ya miradi yake hajahamisha.

Yaani hii nchi ni invaders tu ndiyo wanaotakiwa kuwa na fedha, wazawa hapa
 
Back
Top Bottom