Bourgeoisie
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 656
- 162
hivi umbumbu huu unaweza kufumbiwa macho na vyombo vya dola?
watu hawakunielewa, wamehusisha kauli yangu na nguvu za giza ... Mimi sikuzungumzia nguvu za giza na wala sifanyi uchawi au ushirikina, nilikuwa nazungumzia majini ambao ni viumbe kama sisi, isipokuwa wao wameumbwa kwa moto na sisi tumeumbwa kwa udongo na wametajwa katika vitabu vyote vitakatifu vya waisalamu na wakristo na mwenyezi mungu amesema tushirikiane nao, alisema sheikh yahya.
alisema kuwa mfalme solomon alikuwa na jeshi la majini na aliwatumia katika ujenzi na vita na kila mwanadamu lazima aelewe kuwa ana jini lake ambalo linamlinda bila yeye kujua.
alibainisha kuwa tayari ameshawaagiza hao walinzi wasioonekana (majini) kumlinda rais kikwete popote anapokwenda katika mikutano yake ya kampeni mpaka atakapomaliza.
aliongeza kuwa hata mgombea urais wa chadema, dk. Willibrod slaa, ana jini wake ambaye anaitwa subiyani, ambaye yeye (sheikh yahya) amemuona na anamtambua.
juzi katika mikutano yake ya kampeni, dk. Slaa alimtaka rais kikwete kumkemea mnajimu huyo kwani asipofanya hivyo wananchi wanaweza kuamini kile kilichosemwa na mtabiri huyo.
source: tanzania daima.
Kama ni wa kweli utafumbiwa macho!
Eh! Tanzania yangu hii!!!!!!!!!!