Elections 2010 Mh. Kikwete anaumwa nini na Ulinzi wa Sheikh Yahya

Elections 2010 Mh. Kikwete anaumwa nini na Ulinzi wa Sheikh Yahya

“watu hawakunielewa, wamehusisha kauli yangu na nguvu za giza ... Mimi sikuzungumzia nguvu za giza na wala sifanyi uchawi au ushirikina, nilikuwa nazungumzia majini ambao ni viumbe kama sisi, isipokuwa wao wameumbwa kwa moto na sisi tumeumbwa kwa udongo na wametajwa katika vitabu vyote vitakatifu vya waisalamu na wakristo na mwenyezi mungu amesema tushirikiane nao,” alisema sheikh yahya.

alisema kuwa mfalme solomon alikuwa na jeshi la majini na aliwatumia katika ujenzi na vita na kila mwanadamu lazima aelewe kuwa ana jini lake ambalo linamlinda bila yeye kujua.

alibainisha kuwa tayari ameshawaagiza hao walinzi wasioonekana (majini) kumlinda rais kikwete popote anapokwenda katika mikutano yake ya kampeni mpaka atakapomaliza.

aliongeza kuwa hata mgombea urais wa chadema, dk. Willibrod slaa, ana jini wake ambaye anaitwa subiyani, ambaye yeye (sheikh yahya) amemuona na anamtambua.

juzi katika mikutano yake ya kampeni, dk. Slaa alimtaka rais kikwete kumkemea mnajimu huyo kwani asipofanya hivyo wananchi wanaweza kuamini kile kilichosemwa na mtabiri huyo.

source: tanzania daima.
hivi umbumbu huu unaweza kufumbiwa macho na vyombo vya dola?
Kama ni wa kweli utafumbiwa macho!
Eh! Tanzania yangu hii!!!!!!!!!!
 
Iwapo unataka kwa haraka kuona Majini na kuwatumia; tamka Majina haya MARA 1,000;

  • 1. Salsal, Salsal ........................x 1,000.
  • 2. Akmash, Akmash..................x 1,000.
  • 3. Laash, Laash..........................x 1,000.
Tamka majina hayo hapo juu, huku ukiwa unafukiza Ubani Maka, Kuzbara na Majani ya Mnazi wa Kipemba au majani ya Mtende au majani ya Mchikichi.
Ukiwa sawa (yaani uwe msafi, mahali safi na nguo safi); atakutokea Paka mweusi au Taa kuzimika au kutokea Moshi mweusi. yaani uwe umetawaza
Ndio huyo – Muagize lolote lile ulitakalo; akuitie Mpenzi, Pesa, cheo au Ushindi.

I hope huyu "Paka mweusi" sio yule mwanachama wa JF mwenye jina hilo.

Anyway - wagombea urais, ubunge na udiwani mmepewa formula hapo. Kazi kwenu.
 
Source Tanzania Daima

[QOUTE]Aliongeza kuwa hata mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, ana jini wake ambaye anaitwa Subiyani, ambaye yeye (Sheikh Yahya) amemuona na anamtambua.

Na huyu pia anahusika na kuanguka kwa slaa ****** au?
 
Source Tanzania Daima

[QOUTE]

"Watu hawakunielewa, wamehusisha kauli yangu na nguvu za giza ... mimi sikuzungumzia nguvu za giza na wala sifanyi uchawi au ushirikina, nilikuwa nazungumzia majini ambao ni viumbe kama sisi, isipokuwa wao wameumbwa kwa moto na sisi tumeumbwa kwa udongo na wametajwa katika vitabu vyote vitakatifu vya Waisalamu na Wakristo na Mwenyezi Mungu amesema tushirikiane nao," alisema Sheikh Yahya.

Alisema kuwa Mfalme Solomon alikuwa na jeshi la majini na aliwatumia katika ujenzi na vita na kila mwanadamu lazima aelewe kuwa ana jini lake ambalo linamlinda bila yeye kujua.

Alibainisha kuwa tayari ameshawaagiza hao walinzi wasioonekana (majini) kumlinda Rais Kikwete popote anapokwenda katika mikutano yake ya kampeni mpaka atakapomaliza.
Aliongeza kuwa hata mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, ana jini wake ambaye anaitwa Subiyani, ambaye yeye (Sheikh Yahya) amemuona na anamtambua.

Juzi katika mikutano yake ya kampeni, Dk. Slaa alimtaka Rais Kikwete kumkemea mnajimu huyo kwani asipofanya hivyo wananchi wanaweza kuamini kile kilichosemwa na mtabiri huyo.

MHH!! Huyu mzee anazeeka vibaya! Kama hawa viumbe waliumbwa na Mungu kama anavyodai, sisi binadamu hatuwaoni, na sijui tutashirikiana vipi na kitu usichokiona ... yeye anawaamuru kama nani?
 
Ufunuo wa Yohana 12

7 Basi palikuwa na vita mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na hilo joka, nalo joka pamoja na malaika zake likapigana nao.

8 Lakini joka na malaika zake wakashindwa na hapakuwa tena na nafasi kwa ajili yao mbinguni.

9 Lile joka kuu likatupwa chini, yule nyoka wa zamani aitwaye
Ibilisi au Shetani, aupotoshaye ulimwenguni wote. Akatupwa chini duniani, yeye pamoja na malaika zake.

Shetani mwanzo alikuwa malaika wa sifa wa Mwenyenzi Mungu, akijulikana kwa jina la Lucifer masikani yake yakiwa ni mbingu ya pili. Lucifer alitamani sana ukuu wa Mwenyenzi Mungu, hivyo akawashawishi malaika aliokuwa nao, waondoke mbingu ya pili na kupanda hadi mbingu ya tatu anapokaa Mwenyenzi Mungu.

Mwenyenzi Mungu alichukizwa na mipango ya Lucifier, Hivyo alimwangiza malaika wa vita Mikaeli, azime jaribio la uasi la Lucifier. Mikaeli na jeshi la malaika walimpiga pigo kuu, na kutupwa duniani kwenye shimo la kuzimu, yeye pamoja na malaika wake, wakisubiri siku ya hukumu ya Bwana.

Malaika walioasi, ndiyo wanajulikana kama majini, na Uislamu umewakubali, na hapa Yahaya anasema ndio wanatulinda, huu ni uongo mtupu.

Shetani na majini siku zote ni kupotosha kweli ya Mwenyenzi Mungu, hakuna jini mwema au jini mbaya. Jini ni jini tu, shughuli yao kubwa ni kuhakikisha, hawaendi jehanum ya moto peke yao, siku zote ni kupotosha, kudanganya wakiwatumia mawakala wao walioko duniani, kina Yahaya, wachawi, madaruweshi, wasoma nyota, na wanganga wa kienyeji.
 
Tangu JK aigie madarakani, kumekuwa na maneno mengi yanayohusu fikra za ushirikina kuwa sehemu muhimu ya utawala wake. Ukiyafuatilia utaonekana wewe pia ni mshirikina, lakini kinachoyapa maneno haya uzito ni:
-Watu wazito katika serikali yake ambao wanayasema pembeni na kuombwa wahifadhiwe. Imefikia hata walinzi wanaogopa kufanya kazi yao kwa kujiamini. Sasa ona Shehe Yahya hata hao walinzi yeye anawaita majini (amesema ni wanadamu).
-JK mwenyewe hajayakemea hadharani, na sasa ona yanaanza kugusa hata mustakabali wa usalama wake.

Ndugu yangu mmoja aliye USA amenitumia kitabu kimoja, ndo nimemaliza kukisoma, kinaitwa "IN THE PRESIDENT'S SECRET SERVICE: Behind the Scenes with Agents in the Line of Fire and the Presidents they Protect" By Ronald Kessler.

Kwa mujibu wa kitabu hiki, rumours na maneno kama aliyoyasema Shehe Yahya, yangetosha kumchukua maelezo ya kutosha na vyombo vya dola ili kuhakikisha kuwa usalama wa Rais hauchezewi. Kwa bahati mbaya, security details ya Rais wetu imejaa wapwa na wajomba!
 
Usikute na yeye mwenyewe Ana Kamati ya ndumba
 
Yule Shehe ni mpotoshaji na mara nyingi watu kama wale huwa wanawanasa watu ambao hawana uhakika na mambo yao. Wana wasi wasi hata wa kile walichonacho. Amini usiamini kuna watu ambao hata kama hana mgombea mwenza wanaenda kwa kalumanzila. Sasa JK hawezi kusema kitu chochote kuhusu hii kauli ya shehe huyu kwa sababu ndio watu ambao anafanya nao kazi, maana hajiamini kwa kila jambo akijua pale alipo ka force tu na anataka kuendelea ku force king tena. Mimi huwa simwangalii wala kumsikiliza yule shehe.
Watu kama hawa ni sawa na wahubiri wakubwa kama akina lwakatale, kakobe, mzee wa upako, mwingira amabo wana win mass kutokana na convising power walizo nazo. Kwa waliosoma probability wanajua ukiwa na unahubiria watu 500 utakalo tabirikesho litawayokea baadhi yao na utakalo sema sasa kuwa anayeumwa gonjwa ambalo ni common kwa watu utawapata baadhi na wale sasa ndo watatumika kuku market saaana.
 
ku******** Sheikh Yahya, hivi anadhani sisi Watanzania tumerogwa!!??
 
Tangu JK aigie madarakani, kumekuwa na maneno mengi yanayohusu fikra za ushirikina kuwa sehemu muhimu ya utawala wake. Ukiyafuatilia utaonekana wewe pia ni mshirikina, lakini kinachoyapa maneno haya uzito ni:
-Watu wazito katika serikali yake ambao wanayasema pembeni na kuombwa wahifadhiwe. Imefikia hata walinzi wanaogopa kufanya kazi yao kwa kujiamini. Sasa ona Shehe Yahya hata hao walinzi yeye anawaita majini (amesema ni wanadamu).
-JK mwenyewe hajayakemea hadharani, na sasa ona yanaanza kugusa hata mustakabali wa usalama wake.

Ndugu yangu mmoja aliye USA amenitumia kitabu kimoja, ndo nimemaliza kukisoma, kinaitwa "IN THE PRESIDENT'S SECRET SERVICE: Behind the Scenes with Agents in the Line of Fire and the Presidents they Protect" By Ronald Kessler.

Kwa mujibu wa kitabu hiki, rumours na maneno kama aliyoyasema Shehe Yahya, yangetosha kumchukua maelezo ya kutosha na vyombo vya dola ili kuhakikisha kuwa usalama wa Rais hauchezewi. Kwa bahati mbaya, security details ya Rais wetu imejaa wapwa na wajomba!

duh... nasoma kama niko majestik vile
 
Aliwataka wananchi wakumbuke utabiri wa mnajimu huyo alioutoa maka 2005 kwamba CCM isipomsimamisha mgombea urais wa kike itaanguka, alidai kuwa CCM ilishinda na yeye (Sheikh Yahya) kubadilisha kauli yake kuwa Rais Kikwete ana sura ya kike.

Alisema kauli ya kumuita kiongozi wa nchi ana sura ya kike ni udhalilishaji ambao haupaswi kuvumiliwa na vyombo vya dola.

Dk. Kalimauganga aliwataka wananchi kukumbuka kauli nyingine ya mnajimu huyo, mwanzoni mwa mwaka huu akiwa katika chombo cha habari (televisheni) kwamba timu ya Simba Sports Club, haitachukua ubingwa na baadaye ikatwaa ubingwa, hali iliyowafanya mashabiki kutaka kuchoma nyumba yake.

"Watu hawakunielewa, wamehusisha kauli yangu na nguvu za giza ... mimi sikuzungumzia nguvu za giza na wala sifanyi uchawi au ushirikina, nilikuwa nazungumzia majini ambao ni viumbe kama sisi, isipokuwa wao wameumbwa kwa moto na sisi tumeumbwa kwa udongo na wametajwa katika vitabu vyote vitakatifu vya Waisalamu na Wakristo na Mwenyezi Mungu amesema tushirikiane nao," alisema Sheikh Yahya.

Alisema kuwa Mfalme Solomon alikuwa na jeshi la majini na aliwatumia katika ujenzi na vita na kila mwanadamu lazima aelewe kuwa ana jini lake ambalo linamlinda bila yeye kujua.

Alibainisha kuwa tayari ameshawaagiza hao walinzi wasioonekana (majini) kumlinda Rais Kikwete popote anapokwenda katika mikutano yake ya kampeni mpaka atakapomaliza.

Aliongeza kuwa hata mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, ana jini wake ambaye anaitwa Subiyani, ambaye yeye (Sheikh Yahya) amemuona na anamtambua.

Juzi katika mikutano yake ya kampeni, Dk. Slaa alimtaka Rais Kikwete kumkemea mnajimu huyo kwani asipofanya hivyo wananchi wanaweza kuamini kile kilichosemwa na mtabiri huyo.
B]

Sheikh Yahya anathibitisha tena kwa kauli yake kwamba JK amechezewa na majini!
 
mimi nijuavyo, huyu ni shushushu wa serikali miaka nenda miaka rudi tangu kipindi cha nyerere. Kwa hiyo sioni sababu ya kumjadili kwani pia ikizingatiwa yeye ni mtanzania na anauhuru wa kutoa mawazo yake.
 
Kuna kipindi mashabiki wa simba walimvamia wakitaka kutwa....naona kaanza kuwa chokonoa CHADEMA
 
Iwapo unataka kwa haraka kuona Majini na kuwatumia; tamka Majina haya MARA 1,000;
  • 1. Salsal, Salsal ........................x 1,000.
  • 2. Akmash, Akmash..................x 1,000.
  • 3. Laash, Laash..........................x 1,000.
Tamka majina hayo hapo juu, huku ukiwa unafukiza Ubani Maka, Kuzbara na Majani ya Mnazi wa Kipemba au majani ya Mtende au majani ya Mchikichi.
Ukiwa sawa (yaani uwe msafi, mahali safi na nguo safi); atakutokea Paka mweusi au Taa kuzimika au kutokea Moshi mweusi. yaani uwe umetawaza
Ndio huyo – Muagize lolote lile ulitakalo; akuitie Mpenzi, Pesa, cheo au Ushindi.
Hapo mpaka uwezo wako wa kukumbuka mambo mengine lazima upotee na kuanza kuahidi yaleyale uliyoahidi bila kutekeleza ukadhani ni mapya.
 
Duh, nimefika 120! hii ngumu kweli na umesema yote yaende baada ya jingine? Naona kizunguzungu, AISEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
 
Back
Top Bottom