Elections 2010 Mh. Kikwete anaumwa nini na Ulinzi wa Sheikh Yahya

Elections 2010 Mh. Kikwete anaumwa nini na Ulinzi wa Sheikh Yahya

mnnnhh...kweli wewe leo uko bwaxxy mbaya...naona unachokonoa mzinga wa nyuki..au unajua wameenda kutafuta maua mazuri kwenye kampeni hawako bize hapa kukufuatilia wewe ulekuwa bwax.....any way mie namwaga mboga banaaa "mitaani watu wanasema ana nguma-lo-kito"... si unajuwa yale mambo yetu yaleeeee....hasa ukute zipu haifungi freshhhh...ahhh sana tuuu...

ila pia kuanguka kwake hasa kwenye majukwaa ya kisiasa huwa inatokana na "hofu ya nafsi" na "hisia ya ukosefu"..aka..guilty consousness...SI UNAJUA ANADAIWA MADENI KIBAO SASA ANAVYOKUTANA USO-KWA-USO NA WADENI WAKE ambao ndio sie wa-tz tunaokuwa tukimdai utimilifu wa zile "ahadi zake lukuki" basi huwa akituona majukwaani analegea mbayaa na kuishiwa nguvu...ndo maana mie nazidi kumshangaa anakopa tena ili tumdai hapo baadae...

One day hasa 2015 huyu mwananchi anaweza kutufia jukwaani....inshalllah mnyazii mungu atamjalia kheri pia na uelewa aaje "kukopa hovyo " ilhali hana uwezo wa kulipa deni la watanzania wenye kiu ya maendeleo toka kuondoka kwa mkoloni wa ki-jerumani... NI MAONI TUU NA YASITUMIKE NJE YA JAMII FORUMS PASI NA MAKUBALIANAO YA KIMAANDISHI NA MMILIKI WA MAONI HAYA
Umenichekesha hapo bold nyekundu,lolz!guilty bwana,unaweza ukaitika hata hujaitwa!hahahahaa,ila uzuri 2015 (kama sababu ni hizi ulizotoa) hatakuwa anaomba kura tena. labda hatahitaji kuwa na hofu.😛layball:
 
.........jamaaa wana picha ya jamaa akiwa US ,anabadilishwa damu...na wamepewa deatils hadi za hospitali hiyo...na anatakiwa kubadilishwa damu kila baada ya miezi sita.....

.........nadhani kama wangeamua kumwaga hizi details ..kampeni..za kuchafuana sijui zingeishia wapi....wanasema ukiwa na nyumba ya vigae ..usirushe mawe....

Jamani haya sasa si kweli. JK anaumwa lakini si ukimwi. Anasumbuliwa na uti wa mgongo pamoja na sehemu ya mishipa ya fahamu nyuma ya kichwa. Anatakiwa kupata mapumziko kadri iwezekanavyo, lakini amekuwa hafanyi hivyo na ndiyo maana anapatwa na hayo matatizo ya kuanguka.
 
Ahsante sana kwa michango mingi. Habari zilizozagaa kwa watu hasa wale wanaishi na VVU, ni kuwa Jk amakuwa anatumia ARV kwa miaka mingi. Ila amekuwa anajifichaa asijulikane kuwa ana VVU na kwa wale wenye VVU wanamtaka aende Public "awe wazi kuwa ana maambukizi" ili apunguziwe kazi kwa mujibu wa taratibu za kazi.

Lakini anajua kuwa kwa hali ilivyo hapa nchini, akisema tu kuwa ana VVU, watanzania watampiga chini kwa sababu ya ubaguzi/unyanyapaa uliopo nchini. Tuendelee kumwomba awe wazi maana ndiyo nia pekee ya kumsaidia!! Mpo hapo?!
 
Humu ndani ya JF kumezidi umbeya wa kila aina na kila mtu amekuwa daktari anafanya diagnosis na kutoa dawa za kutibu maradhi ya JK.

Mara picha Marekani, mara anatumia ARV, mara uongo huu mara uongo ule. Jamani mwacheni baba wa watu aendelee na kampeni zake kwa amani.

Mwengine amezuka na mpya kwamba ameanguka Mbeya na Sengerema, lakini hakuna mwandishi aliyekuwa na taarifa hizo, sasa yeye amezipata wapi?
 
Humu ndani ya JF kumezidi umbeya wa kila aina na kila mtu amekuwa daktari anafanya diagnosis na kutoa dawa za kutibu maradhi ya JK.

Mara picha Marekani, mara anatumia ARV, mara uongo huu mara uongo ule. Jamani mwacheni baba wa watu aendelee na kampeni zake kwa amani.

Mwengine amezuka na mpya kwamba ameanguka Mbeya na Sengerema, lakini hakuna mwandishi aliyekuwa na taarifa hizo, sasa yeye amezipata wapi?

Sheikh Yahaya amesema kwamba JK karogwa ndo maana alianguka jukwaani siku ya kuzindua kampeni, hilo nalo ni vipi?
 
Ni umbeya tu.

Hivi wewe humo ndani ya moyo wako unaamini kuna mtu anaweza kutabiri lo lote hapa duniani? Hebu angeanza kwa kujitabiria yeye mwenyewe kwamba ataumwa na nini na atakufa lini.

Sh Yahya ameona anao wateja ambao watamuamini kwa lo lote basi ndivyo anavyofanya. Na vyombo vya habari vinazipa kipaumbele hizo habari zake ambazo siku zote huwa hazina ukweli, au yeye huwa anatumika kama chombo cha kutoa taarifa ambazo ni kweli lakini huzipindua kwa kujifanya mtabiri.

Naomba samahani kwa wapenzi wa utabiri wa Sh. Yahya.
 
BitiMkongwe wenyewe wakikusikia, mie simo. Ngoja nikuwekee link kwanza halafu nikupe post 2 tu maana kwenda kusoma mada nzima macho yatakuwa mekundu na ukipita ile mitaa ya kule kwetu na huo ukongwe wako ... unaweza kuitwa mchawi, halafu unajua kitakachofuata!

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/69279-utabiri-wa-sheikh-yahya-hussein-watimia.html

Sheikh Yahya Hussein alitabiri kuwa mtu yeyote ataeshindana na Kikwete atakufa. watu wengi walikanusha na kumbeza, wengine walidiriki kusema mzee amechoka na hana mpya.

kumbe utabiri wake una ukweli wa kutosha, wengi tulifikiri kufa ni kutoka roho tu. lakini hata kufa kisiasa ni kufa

kwa hio ndugu yetu shibuda aliepambana na Kikwete tayari ameshakufa kisiasa

Wakuu,
Mbona mnashambulia sana mleta maada?Hayo ni maoni yake tu.
Kumbuka uchaguzi wa mwaka 2005, Sheikh Yahya, alitabiri kuwa mshindi katika uchaguzi huo angekuwa mwanamke. Na baada ya JK kushinda, Yahya, alisema alikuwa na maana ya mshindi mwenye mvuto wa mwanamke.

Kwa hiyo inawezekana mleta maada akawa yuko sahihi.

Sikuwahi kusikia utabiri kuhusu uchaguzi zama za mzee wa uwazi na ukweli wala mzee ruksa ... ila tangu 2005 utabiri ambao uko related na serikali, uchaguzi na mengineyo naona umeongeza kasi. kuna haja ya kujiuliza kwanini? kwanini huyo anayetabiriwa yuko kimya? kwanini serikali inashirikishwa kwenye haya mambo na inakaa kimya? ccm nayo naona imekaa kimyaaaaaaaaaaaaaaaaaa. ina maana wanaunga mkono huu upuuzi? Rais anaposemekana ana mvuto wa mwanamke maana yake ni nini?

Bibi yangu wewe ni mtu mzima, yawezekana unaweza kuwa na hints, hata mimi ninachoshwa na huu ujinga wa Sheikh Yahaya na bado serikali nayo iko kimya!
 
Mimi macho yangu mekundu bibi yako lakini bado akili inafanya kazi.

Kwa vile mgombea wa mwaka 2005 alikuwa ni Kikwete na yeye alikuwa anashabikiwa na watanzania wengi, na hakukuwa na upinzani madhubuti, jee hapo pana shida ya kutabiri nani angeshinda???? Ndio maana nilikwambia huyo big Sheikh alikuwa anatoa hints ambazo labda alipewa na taasisi fulani kwa kuelewa kwamba Watanzania tunaamini sana mambo ya utabiri.

Mimi huwa nachoshwa na huo utabiri wa huyo Mzee na picha za majini za kuongezea vitisho.

Nakubaliana na wewe sijui kwa nini Serikali inashabikia mambo kama haya kwa kutotoa kauli yo yote ile.
 
Na yule kandideti tuliyeambiwa na magazeti alikutwa anacheza ngoma uchi wa mnyama kwenye kibanda cha sangoma mwaka 2005 aliishia wapi?
 
Leo nimesikia kwenye Magazeti kwamba Sheikh Yahya anadai kwamba Kuanguka Mara kwa Mara kwa Mh JK ni kutokana na Nguvu za Giza, sasa ameamua kumuongezea mheshimiwa Rais Nguvu zaidi "Zisizoonekana"

Swali langu Je JK na CCM ndiyo wameomba huo Ulinzi, Je wao wanasemaje kuhusu huo Ulinzi wa Nguvu za Giza, je Hii haina maana kwamba JK haamini Madaktari?
 
Mungu wangu! Kweli tunaruhusu ujinga kama huu kuendelezwa katika media? Huku ni kufilisika kimawazo. Mtu anapozirai kuna physical na psychological reasons.. mambo ya kuhusisha udini/ imani ni hatari sana .. ndo inapelekea watu kufa wakiamini kuwa wataponyeshwa kwa nguvu za Mungu or any other mysterious powers...
Lakini on the other hand - Sheikh Yahya anataka kutuambia kuwa Kikwete amezidiwa na nguvu za giza .. so he is now EVIL? Kama Darth Vader? Kama amezidiwa it means he has been 'turned'? Hahaha :becky: mwaka huu tutasikia mengi ila hii kali sana...
 
Ndiyo hivyo mkuu, Sheikh amesambaza Barua kwenye magazeti Mbalimbali akionya watu waache "Kumchezea" Prezidaa
 

Hadi jana usiku,nilikuwa sijashawishika kuchangia ninachojua katika CV ya Jakaya Kikwete.Lakini baada ya HABARI LEO "kufungulia mbwa" basi acha nasi tueleza tunachojua kumhusu mgombea urais kwa tiketi ya CCM (KIkwete).

Mambo matatu ambayo NINA UHAKIKA NAYO ni kuwa Kikwete . . . .

La pili ni kwamba Kikwete . . . .

La tatu ni mambo ya kienyeji.Wakati wa kampeni zake za uchaguzi 2005 alikuwa anamtembelea mganga mmoja eneo la Kiberege wilayani Kilombero Mkoani Morogoro.

HAYO NINA UHAKIKA NAYO.

Tetesi nilizowahi kusikia ni kwamba . . .

Kuna mengine nayafanyia kazi,lakini kwa leo ni hayo tu.I repeat, NINA USHAHIDI WA HAYO MATATU YA KWANZA.


Source: https://www.jamiiforums.com/uchaguz...kikwete-in-black-and-white-5.html#post1066269
 
Leo nimesikia kwenye Magazeti kwamba Sheikh Yahya anadai kwamba Kuanguka Mara kwa Mara kwa Mh JK ni kutokana na Nguvu za Giza, sasa ameamua kumuongezea mheshimiwa Rais Nguvu zaidi "Zisizoonekana"

Angekuwa na uwezo wa kumwongezea JK ulinzi wa kishirikina angefanya hivyo kimya kimya. Kutangaza maana yake ni debe tupu lisiloacha kutika.
 
Kwa maana hiyo ni kuwa ulinzi aliopewa hautoshi. Mkuu wa usalama wa Taifa hafanyi kazi yake siyo hivyo amwachie ofisi Sheikh Yahya!!
 
Hivi Shekh Yahaya anapata wapi ujasiri wa kutangaza hayo kama hana 'mkataba' wowote na JK?
yaani rais anatumika kutangaza biashara ya shekh yahya!
kweli raisi tunaye.
 
Back
Top Bottom