Elections 2010 Mh. Kikwete anaumwa nini na Ulinzi wa Sheikh Yahya

Elections 2010 Mh. Kikwete anaumwa nini na Ulinzi wa Sheikh Yahya

Sheikh%20Shariff.jpg

Mtoto Sheikh Sharif Yusufu Mohammed

Maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, jana walipigana vikumbo kugombea kupata huduma ya mtoto mwenye umri wa miaka 12 anayeaminika kuwa na karama ya uponyaji kutoka kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya magonjwa yote yanayomsumbua mwanadamu.

Nipashe ilifika jana asubuhi katika Mtaa wa Luponda, ulioko Magomeni Makuti, Wilaya ya Kinondoni na kushuhudia maelfu ya watu wa rika na jinsia tofauti wenye maradhi tofauti wakiwa wamefurika ndani na nje ya nyumba inayotumiwa na mtoto huyo kutolea huduma zake, wakisubiri kuhudumiwa.

Mtoto huyo, Sheikh Sharif Yusufu Mohammed, ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi ya Kiembesamaki, visiwani Zanzibar, amekuwa akitoa huduma yake kwa njia mbalimbali, ikiwamo kuwaombea dua (maombi) wagonjwa ili kupona maradhi yanayowasumbua.

Dua hiyo husomwa na Sheikh Sharif kwa awamu mbili tofauti; moja ikiwa ni kwa watu wote, ambayo huisoma kwa kushirikiana na wasaidizi wake na nyingine humsomea mgonjwa mmoja mmoja, huku akiwa amemuwekea mkono kichwani.

Wasaidizi wengine wa mtoto huyo ni Sheikh Salim Khamisi, maarufu kama "A'inan Mardhwiyyah", Sheikh Maulana Habshiy na Sheikh Sultan Khamisi (bwana dawa).

Njia nyingine inayotumiwa na mtoto huyo katika kuwahudumia wagonjwa, ni kuwapatia maji kwa matumizi ya kunywa kwa masharti, baada ya kuyaombea maji hayo.

Baadhi ya wagonjwa waliozungumza na Nipashe, walidai wanaamini huduma inayotolewa na mtoto huyo ni ya uhakika kwa vile kila aliyebahatika kuhudumiwa naye, alipona, wakiwamo watu waliokuwa wakisumbuliwa na maradhi sugu na yasiyotibika.

Mmoja wa wasaidizi na kaka ya mtoto huyo, Sheikh Salim Khamisi, alisema miongoni mwa wagonjwa waliokwishahudumiwa na mdogo wake, ni pamoja na mama mjamzito, mkazi wa Mabibo, jijini Dar es Salaam aliyedumu na ujauzito kwa miaka minne.

Alisema baada ya kuhudumiwa na Sheikh Sharif, hivi sasa mama huyo yuko hospitali na kwamba, uchunguzi wa kidaktari umethibitisha kuwa ana ujauzito wa watoto mapacha na anatazamiwa kujifungua wakati wowote kuanzia hivi sasa.

Kwa upande wake, Sheikh Sharif alisema karama aliyonayo, amejaliwa na Mwenyezi Mungu na kwamba, kwa karama hiyo kamwe hawezi kuthubutu kujiita yeye ni Nabii wala Mtume kwa vile anaamini kuwa Nabii Muhammad (S.A.W.) ndiye Mtume wa mwisho.



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Huyu ndiye anafaa kumlinda JK siyo Mtabiri Yahya.
 
Mficha maradhi mauti humuumbua. Hatumwembei mauti ila kwa hali aliyonayo mauti iko karibu, ukizingatia ameongezewa muda wa kampeni. Tunayoyaona nje ni hadi aanguke. Lakini hatujui ana-undergo taabu kiasi gani hadi anafikia kuanguka. Sina hakika kama yeye mwenyewe anajali afya yake, kwani angeshawaambia kuwa anahitaji kupunzika.

Kwani ni aibu kuongoza miaka mitano tu? Tena kwa umri wake angeomba kupunzika akiwa bado na heshima yake, anaweza tena kugombea baada ya miaka mitano akishaweka sawa afya yake, ikiwa kutakuwa na haja naye.
 
Sheikh Yahya aingiza ushirikina uchaguzi Mkuu


Mnajimu mashuhuri wa Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein, amezua jambo kwa kuelekeza harakati za uchaguzi katika mambo ya kishirikina huku akitangaza kuwa utatawaliwa na mambo ya giza.

Uchaguzi gani huo anaouzungumzia, kwani yeye si alishatabiri mwaka huu hakuna uchaguzi, au kasahau???????
 
Shekh yahaya mpumbavu tu, Raisi wetu haitaji ulinzi wa mashetani yake... kuhusu waganga Wamejaa kibao! utasikia leo katangaza katoa misukule 100! .. TEHETEHE!! Alafu wanaimba mapambio wasivokuwa na akili:becky:

Kama hatumii nguvu za giza na dokta wake ni Shehe Yahya, basi akanushe aliyosema Yahya Husein kumhusu yeye. Kinyume chake tutarajie kuwa na kiongozi anayoongoza nchi kwa nguvu za giza.
 
hii topic imegeuzwa heading ili kuipunguza makali, nilipenda ile heading ya shehe hussein kumlinda Kikwete.

That was news ...... think of it.
The guy anatishia watu wanaomloga Kikwete kuwa atawaloga hadi wakome na kisha nobody from state house says a word
 
shindwa katika Jina la Yesu... Ikulu haiezi kaliwa tena na mtu anaetegemea waganga wa kienyeJi, Mchawi, kwa kifupi.... DR. SLAA ndo Mbadala.
 
Inawezekana ikawa swaumu wakati wa mfungo wa mwezi mtukufufu wa Ramadhani; lakini je anapoanguka wakati usio wa mfuno pia inakuwa swaumu? CCm hawataki kukubali kuwa Rais wetu ni mgonjwa na kutaka kuonesha hilo wamejiandaa baada ya sikukuu ya IDD wampe Rais ratiba kabambe ya kuomba kura kwa wananchi; kwa kufanya hivyo ni dhahili kuwa Makamba na wapambe wengine hawampendi Jakaya kwani hawajali afya yake bali maslahi yao; je akianguka tena watasema nini? Hata Jakaya akishinda wasiwasi wangu ni kuwa hali ya afya yake itaruhusu wajajnja watawale kwa niaba yake na hilo si jambo zuri kwa mustakabali wa Taifa letu!! Kumbukeni tu kuwa wakati ule Mkapa alipougua na kwenda kutibiwa Ulaya ndio wakati wajanja walipogundua mbinu za kuliibia Taifa rasilimali nyingi sana!!

Kwenye red, ni kweli hata kiwira, anaben bank na mengine mengi alikuwa nje! shame say.
Nashangaa kwa nini nyinyi wa chadema mnalalamika kuwa slaa anachafuliwa, wakati nyinyi ni namba moja kwa kuchunguza maisha binafsi ya mtu. mara mmuambie ana HIV, sasa mnalalamika nini? Haya ya JK niyakufikirika zaidi kuliko ya slaa ya kuiba mke wa mtu na kesi imefunguliwa mahakama kuu, au ndo mkuki kwa nguruwe.....! Aggghhh...
 
. ,anabadilishwa damu...na wamepewa deatils hadi za hospitali hiyo...na anatakiwa kubadilishwa damu kila baada ya miezi sita......


Mkuu, nilizani wewe umeelimika na sasa nashawishika kuamini vinginevyo! HIV HAITIBIWI kwa kubadilisha damu...this is just a myth prevailing in Africa. Hakuna kitu kinachoitwa kubadili damu kwa mtu mwenye HIV kwasababu HIV sio ugonjwa wa damu pekee bali ni wakila chembe hai (cells) za mwili wa binadamu. Watanzania tuna safari ndefu sana!!
 
Kuna mstari umeandikwa kwenye biblia ila nimesahau uko wapi ila maneno yako yanasema kitu kama hiki:

".......Kama nyumba/Mji haulindwi na Bwana, walindao wanafanya kazi bure."

Heri basi walau angelianza kuwa mcha Mungu wa kweli. Haya majini hayamfikishi popote.

Utatafuta wachawi wee kumbe wachawi unao hapohapo wamekuzunguka akina Rostam, Lowassa, And all Mafisadi.

Namsikitikia sana JK, ila Slaa ina usimame kwa zaburi 125:1. Dr Slaa na wote tuaminio ulinzi wa mungu alie hai tusimamie Zab 140.
 
Ukiona hivyo ujue bado kuwashika sehemu ndogo sana walipohifadhi pumzi zao ili tuwapore madaraka
 
Wasomi wa nchi hii tumeenda wapi?
Kwanini tunaacha nchi inaendeshwa kigagura?
Au na sisi tumerogwa?
 
halafu hakuna tamko lolote toka ikulu au kwa yule jambazi Kinana. Inaonekana ikulu na ccm wanakubaliana kabisa na shehe yahaya
 
Jamani haya sasa si kweli. JK anaumwa lakini si ukimwi. Anasumbuliwa na uti wa mgongo pamoja na sehemu ya mishipa ya fahamu nyuma ya kichwa. Anatakiwa kupata mapumziko kadri iwezekanavyo, lakini amekuwa hafanyi hivyo na ndiyo maana anapatwa na hayo matatizo ya kuanguka.

Sasa kama anahitaji mapumziko ya mara kwa mara mbona yeye ndio kwanza anasafiri mara kwa mara tena safari za nje ya nchi!!!
 
Mkuu, nilizani wewe umeelimika na sasa nashawishika kuamini vinginevyo! HIV HAITIBIWI kwa kubadilisha damu...this is just a myth prevailing in Africa. Hakuna kitu kinachoitwa kubadili damu kwa mtu mwenye HIV kwasababu HIV sio ugonjwa wa damu pekee bali ni wakila chembe hai (cells) za mwili wa binadamu. Watanzania tuna safari ndefu sana!!

Ni vema ukitoa na sources kupunguza utata mkuu...
 
No wonder and nothing new kama tunavyo fahamu utalii huko Bagamoyo nyakati hizi za uchaguzi huwa uko juu sana, na ni utalii wa ndani jiulize kulikoni?
 
Kwani kuanguka jukwaani kulimfanya ashindwe kuongoza taifa? sijawahi msikia raisi wetu anaumwa ameshindwa kufanya shughuli zake toka aingie madarakani, siku zote yupo busy. wabongo bwana!
 
Mkuu, nilizani wewe umeelimika na sasa nashawishika kuamini vinginevyo! HIV HAITIBIWI kwa kubadilisha damu...this is just a myth prevailing in Africa. Hakuna kitu kinachoitwa kubadili damu kwa mtu mwenye HIV kwasababu HIV sio ugonjwa wa damu pekee bali ni wakila chembe hai (cells) za mwili wa binadamu. Watanzania tuna safari ndefu sana!!


He he heee! Jandulo lingine hilo.

Hata wewe jaribu kwenda hospitali kuwekewa damu nyingine.

Mwaka huu hata mfanye vipi nyie vifisadi vidogo vidogo, sisi tupo imara.
 
Hayahaya anahangaika nini tena? Mbona kuzimu walishamwapisha kuwa rais.
 
Sheikh Yahaya kamfanya JK kukosa kura za waumini kwani wengi hatutaki tuongozwe kwa nguvu za giza.
 
Back
Top Bottom