Elections 2010 Mh. Kikwete anaumwa nini na Ulinzi wa Sheikh Yahya

Elections 2010 Mh. Kikwete anaumwa nini na Ulinzi wa Sheikh Yahya

Shehe Yahya Hussein halindi Serikali, na amekua akimlinda JK Kikwete tangu siku nyingi tu, anasema atamuongezea nguvu.
hajasema atailinda serikali, hayo ni makubaliano ya Shehe Yahya na Kikwete, wanakutana wapi na vipi wanajuana.ila lililowazi ni kua JK amepokea huduma hiyo, ni yeye mwenyewe wakukanusha, kukubali na kumkana mtu huyo.
lakini wana urafiki wa karibu hawa, nasikia JK aliwahi hata kumpeleka mganga wake hospitali nje ya nchi kwa ukaribu wao.

Mkuu do not tell me that tunaongozwa kwa nguvu za giza? Kama ushetani na majini yameanza kuwa sehemu ya uongozi wetu basi tunaweza kuwa failed state. Na kama watu wameanza kujitangaza hadharani kuwa ni watoa ulinzi wa nguvu za giza kwa rais wetu ni hatari. Inawezekana nchi yetu iko chini ya haimaya ya nguvu za giza.
 
Au anatumiwa na CHADEMA kufanya kampeni za maji 'TAKA'

Aisee!! yaani nimejikuta ninacheka kwa hasira. Tangu lini Sheik Yahya akachangamana na CHADEMA? CHADEMA hawana historia ya kuendekeza majini na ushirikina kama CCM. CHADEMA wanamtumaini Mungu tu, ndiyo maana tunataka washike nchi ili waiweke mikononi mwa Mungu si kama hivi sasa ambapo nchi inaongozwa na majini, mashetani na wasoma nyota, kama akina sheik yahya.
 
JK ataanguka tena, kama anawategemea waganga wa kienyeji. Ataacha ushauri wa wataalamu.

Hakuna kumpa kura JK kwani ni mshirikina.
 
mie nikuuluzeni mungu gani anaekuwa na mzinzi?

unajua biblia imakataza sana uzinzi

na inamini familia na jamii bora ni ile watu waliooana na sio kukamatana wakazaa(kama alivyofanya Dr slaa kwa mwanamke wa kwanza), kuchochea kuvunjika ndoa za wengine kwa kuwaibia wake/waume zao

na tunapotafuta rais moja ya kazi yake ni kujenga jamii yenye maadili, ambayo hii ndio itakuwa na uelewa na uwezo wa kujenga uchumi ulio imara

itawezekanaje taifa linaloongozwa na mzinzi na aliefeli maadili kutufikisha hapo?

Katika viongozi wa juu wa serikali, JK anaongoza kwa kujua kusafisha his brown stick. Tunawajua wanawake wengi ambao wamekuwa wakipata kazi kwenye balozi zetu za nje bila kuwa na qualifications.
Mpaka leo hatujasikia mpayukaji Makamba akikana tuhuma za kubaka mwanafunzi. That is serious allegation.
 
Black magic in Islam, is totally prohibited and must be kept away at all time. A person is not in any condition is permitted to use the black magic to help overcome his/her nessesities. In Islam, a person is a mushrik or a polytheistic if he is engaged in Black magic. The Prophet (peace and blessings be upon him) said, “Whoever blows on knots practices magic, and whoever practices magic is a mushrik (polytheist).” (Reported by At-Tabarani)

`Abdullah ibn Mas`ud reported, “Anyone who goes to a diviner, a practitioner of magic or a soothsayer, asking something and believing in what he says, denies what was revealed to Muhammad.” (Reported by Al-Bazzar and Abu Ya`la)

Magic can be dispelled through magicians themselves or sorcerers or through applying their methods. However, it is forbidden to go to a magician or a soothsayer or the like to dispel the magic as stated in the hadiths of the Prophet.

Magic can also be dispelled by the power of the Glorious Qur’an, which was sent down as a cure and mercy for believers; doing so is highly commendable. This is based on what is known in the Sunnah that angel Gabriel used the Qur’an (Al-Mu`awwidhatayn, or the Two Protective Surahs, i.e. Al-Falaq and An-Nas) in dispelling the evil charm done to the Prophet (peace and blessings be upon him) by the Jews. Moreover, surat Al-Baqarah is known to have the power of driving away evil spirits and dispelling magic.

Regarding Black magic and how to dispel it, the eminent Muslim scholar, Sheikh Muhammad Al-Hanooti, member of the North American Fiqh Council, states:

“The Qur'an talks about black magic in surat Al-Baqarah: “And they followed what the Shaitans chanted of sorcery in the reign of Sulaiman, and Sulaiman was not an unbeliever, but the Shaitans disbelieved, they taught men sorcery and that was sent down to the two angels at Babel, Harut and Marut, yet these two taught no man until they had said, "Surely we are only a trial, therefore do not be a disbeliever." Even then men learned from these two, magic by which they might cause a separation between a man and his wife; and they cannot hurt with it any one except with Allah’s permission, and they learned what harmed them and did not profit them, and certainly they know that he who bought it should have no share of good in the hereafter and evil was the price for which they sold their souls, had they but known this.” (Al-Baqarah: 102 )þ

Another reference from the Qur’an is surat Al-Falaq: “Say: I seek refuge in the Lord of the dawn. From the evil of what He has created. And from the evil of the utterly dark night when it comes. And from the evil of those who blow on knots. And from the evil of the envious when he envies.” (Al-Falaq: 1-5)

There is another verse that is relevant to this issue from surat Al-Baqarah: “Those who swallow down usury cannot arise except as one whom Shaitan has prostrated by (his) touch does rise. That is because they say, trading is only like usury; and Allah has allowed trading and forbidden usury. To whomsoever then the admonition has come from his Lord, then he desists, he shall have what has already passed, and his affair is in the hands of Allah; and whoever returns (to it)-- these are the inmates of the fire; they shall abide in it.” (Al-Baqarah: 275)

From the above verses from the Glorious Qur'an and Hadith, it is explicit, that Black magic is Haram, and one's doing so, one becomes a mushrik.

Narrated Sad: Allah's Apostle said, "He who eats seven 'Ajwa dates every morning, will not be affected by poison or magic on the day he eats them." (Al-Bukhaari 65, Hadith 356)

this guy he was not supposed to be dressed as shekh!.. na hana bahati hatuna sharia TZ , tungekuwa na sharia tungeshanyonga washirikina wote kama hawa

Weeee bwana wacha kutuwekea hivi vitu hapa badala yake peleka kule dilisha la dini. Maana tukianza kuchambua hayo uliyoweka hapo utaanza kulia lia hapa na Mods ili tupate ban.
Hizo hadithi za kikwenu zimejaa utata tupu. Maana kwa mlango mwingine mwawakubali kwa mlango mwingine mwawakataa. Basi bana wacha niishie hapa, kwani si sehemu yake.
 
Sheikh%20Yahya%20Hussein,%285%29.jpg

Mnajimu Sheikh Yahya Hussein


Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema, Dk. Willibroad Slaa, amemkemea mnadhimu Sheikh Yahya Hussein na kumtaka aache kuingiza masuala ya ushirikina katika siasa na uongozi wa nchi na kueleza kuwa hawezi kuvumilia nchi kuongozwa na imani za kiganga.
Dk. Slaa aliyasema hayo jana katika mji mdogo wa Katoro, Jimbo la Busanda alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi.
Alisema kimsingi anaheshimu kila imani ya Watanzania ikiwemo ya Sheikh Yahya lakini akakemea tabia yake ya kutoa vitisho kuwatishia wananchi hususan pale aliposema atakayeshindana na Rais Kikwete katika kinyang'anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, atakufa ghafla.
Hata hivyo, alisema yeye mwenyewe hatishiki na vitisho hivyo na kufafanua kuwa ana imani kuwa Rais Kikwete atakanusha taarifa hizo za Sheikh Yahya alizosema atamuongezea ulinzi wa ziada usioonekana.
"Majini hayawezi kuliendesha taifa hili...Hatupendi taifa hili liongozwe na waliomuasi Mungu. Tunaheshimu imani ya kila mmoja ikiwemo ya Sheikh Yahya lakini hatutaki Sheikh Yahya aendelee kutoa vitisho," alisema.
Alifafanua kuwa kama Rais atakubali ulinzi huo wa Sheikh Yahya, basi awaruhusu walinzi wengine wanaolipwa mshahara unaotokana na kodi za wananchi ili wakafanye kazi nyingine.
Dk. Slaa jana alifanya mikutano mitano katika maeneo ya Nyarugusu, Ushirombo, Bukombe, Kikobe na Masumbwe.
Leo Dk. Slaa anatarajiwa kuhutubia mkutano wake wa kampeni katika Jimbo la Geita kwenye machimbo ya dhahabu, Buchosa na Nyamagana.



CHANZO: NIPASHE
 
quote_icon.png
Originally Posted by Burn
Au anatumiwa na CHADEMA kufanya kampeni za maji 'TAKA'

Unataka kumkanushia aliyepewa ulinzi wakati anayelindwa hajasema kitu. Mwenzio anafurahia ulinzi wake wa MAJINI.


CHADEMA inaingiaje hapa kwa mtu wa karibu (MLINZI) wa JK?
CHADEMA wamekuchukiza nini hata uwaingize msambweni ilihari ukijua anayependa ushirikini CCM na Kikwete anayeanguka kwa sababu ya kuzidiwa na nguvu ya majini yanayomlinda.
 
quote_icon.png
Originally Posted by Burn
Au anatumiwa na CHADEMA kufanya kampeni za maji 'TAKA'

Unataka kumkanushia aliyepewa ulinzi wakati anayelindwa hajasema kitu. Mwenzio anafurahia ulinzi wake wa MAJINI.
mkuu jk yupo bize na kampeni hana muda wa kujibu hoja zisizo na kichwa wala miguu
wa kuulizwa ni sheiikh yahaya katumwa na nani kutoa huo "ulinzi"
 
mkuu jk yupo bize na kampeni hana muda wa kujibu hoja zisizo na kichwa wala miguu
wa kuulizwa ni sheiikh yahaya katumwa na nani kutoa huo "ulinzi"

Abdul Rahim Kinana! Yule Msomali
 
Sijamtetea ila nimetumia logic ya kawaida tu, kama mume akidai haki zake kwa kuibiwa na kudhalilishwa kwa kuibiwa mkewe ni mbinu ya CCM kumchafua Slaa basi inawezekana pia Mchawi kujihusisha na JK ni mbinu ya CHADEMA kumchafua JK.
Mbona umeanza na chadema??kwanini usiseme wengine palipo na waganga wakienyeji ni wapi kama siyo ccm??Wabunge vilaza,waganga wakienyeji ndani ya bunge??.......mwaka huu mmechoka kwenda mbali hadi mmeamua kudeploy katika bunge vigagula!Yani mlinzi wa rais atoke chadema??you are not serious MR Burn.
 
Iwapo unataka kwa haraka kuona Majini na kuwatumia; tamka Majina haya MARA 1,000;
  • 1. Salsal, Salsal ........................x 1,000.
  • 2. Akmash, Akmash..................x 1,000.
  • 3. Laash, Laash..........................x 1,000.
Tamka majina hayo hapo juu, huku ukiwa unafukiza Ubani Maka, Kuzbara na Majani ya Mnazi wa Kipemba au majani ya Mtende au majani ya Mchikichi.
Ukiwa sawa (yaani uwe msafi, mahali safi na nguo safi); atakutokea Paka mweusi au Taa kuzimika au kutokea Moshi mweusi. yaani uwe umetawaza
Ndio huyo – Muagize lolote lile ulitakalo; akuitie Mpenzi, Pesa, cheo au Ushindi.
 
MTAALAMU wa Tiba za Asili, Dk. Sadiki Kalimauganga, amelitaka Jeshi la Polisi kumkamata mnajimu wa Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Husein na kumpeleka katika vyombo vya sheria kwa kosa la kumdhalilisha Rais Jakaya Kikwete kuwa alianguka jukwaani kutokana na kuzidiwa nguvu za giza.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Dk. Kalimauganga ambaye alitaka kugombea ubunge katika Jimbo la Urambo Mashariki kupitia CCM na baadaye kuachia ngazi, alimtaka Sheikh Yahya kuacha kutangaza utabiri kwa Rais Kikwete, utabiri ambao alidai kuwa ni wa uongo.

"Namwomba Sheikh Yahya aache kuwatabiria uongo viongozi na chama chetu, kwani katika uchaguzi wa mwaka 2005 alitabiri vitu vya ajabu sana, ambavyo hakuna hata kimoja kilichokuwa cha kweli," alisema.

Alisema ni jambo la ajabu kwa mtabiri huyo kuuambia umma kuwa Rais Kikwete alianguka jukwaani kutokana na kuzidiwa nguvu na majini waliotumiwa na wagombea wenzake wa urais wakati si kweli.

Alibainisha kuwa ni udhalilishaji kutangaza hadharani kuwa rais atapatiwa ulinzi usioonekana (majini) katika kampeni zake ili kujikinga na watu wanaomfanyia ushirikina.

Aliwataka wananchi wakumbuke utabiri wa mnajimu huyo alioutoa maka 2005 kwamba CCM isipomsimamisha mgombea urais wa kike itaanguka, alidai kuwa CCM ilishinda na yeye (Sheikh Yahya) kubadilisha kauli yake kuwa Rais Kikwete ana sura ya kike.

Alisema kauli ya kumuita kiongozi wa nchi ana sura ya kike ni udhalilishaji ambao haupaswi kuvumiliwa na vyombo vya dola.

Dk. Kalimauganga aliwataka wananchi kukumbuka kauli nyingine ya mnajimu huyo, mwanzoni mwa mwaka huu akiwa katika chombo cha habari (televisheni) kwamba timu ya Simba Sports Club, haitachukua ubingwa na baadaye ikatwaa ubingwa, hali iliyowafanya mashabiki kutaka kuchoma nyumba yake.

Alisema kutokana na matukio hayo ambayo alidai kuwa yalikuwa na utabiri wa uongo, anaomba mnajimu huyo asipuuzwe na wananchi pamoja na Rais Kikwete anayeendelea na kampeni.

Wakati huo huo, Sheikh Yahya amebainisha kuwa hakueleweka kwa wananchi alipotoa kauli ya kumpa ulinzi usioonekana Rais Kikwete.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana jijini Dar es Salaam, Sheikh Yahya alisema kuwa alikuwa anazungumzia majini ambayo ni viumbe kama binadamu lakini wao wameumbwa kwa moto na binadamu wameumbwa kwa udongo.

"Watu hawakunielewa, wamehusisha kauli yangu na nguvu za giza ... mimi sikuzungumzia nguvu za giza na wala sifanyi uchawi au ushirikina, nilikuwa nazungumzia majini ambao ni viumbe kama sisi, isipokuwa wao wameumbwa kwa moto na sisi tumeumbwa kwa udongo na wametajwa katika vitabu vyote vitakatifu vya Waisalamu na Wakristo na Mwenyezi Mungu amesema tushirikiane nao," alisema Sheikh Yahya.

Alisema kuwa Mfalme Solomon alikuwa na jeshi la majini na aliwatumia katika ujenzi na vita na kila mwanadamu lazima aelewe kuwa ana jini lake ambalo linamlinda bila yeye kujua.

Alibainisha kuwa tayari ameshawaagiza hao walinzi wasioonekana (majini) kumlinda Rais Kikwete popote anapokwenda katika mikutano yake ya kampeni mpaka atakapomaliza.

Aliongeza kuwa hata mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, ana jini wake ambaye anaitwa Subiyani, ambaye yeye (Sheikh Yahya) amemuona na anamtambua.

Juzi katika mikutano yake ya kampeni, Dk. Slaa alimtaka Rais Kikwete kumkemea mnajimu huyo kwani asipofanya hivyo wananchi wanaweza kuamini kile kilichosemwa na mtabiri huyo.


Source: Tanzania Daima.
 
What Goes Around Comes Around, Waache kutubabaisha Sheikh Yahya ni Mlozi so ana uhakika na Anachosema
 
Source Tanzania Daima

[QOUTE]

"Watu hawakunielewa, wamehusisha kauli yangu na nguvu za giza ... mimi sikuzungumzia nguvu za giza na wala sifanyi uchawi au ushirikina, nilikuwa nazungumzia majini ambao ni viumbe kama sisi, isipokuwa wao wameumbwa kwa moto na sisi tumeumbwa kwa udongo na wametajwa katika vitabu vyote vitakatifu vya Waisalamu na Wakristo na Mwenyezi Mungu amesema tushirikiane nao," alisema Sheikh Yahya.

Alisema kuwa Mfalme Solomon alikuwa na jeshi la majini na aliwatumia katika ujenzi na vita na kila mwanadamu lazima aelewe kuwa ana jini lake ambalo linamlinda bila yeye kujua.

Alibainisha kuwa tayari ameshawaagiza hao walinzi wasioonekana (majini) kumlinda Rais Kikwete popote anapokwenda katika mikutano yake ya kampeni mpaka atakapomaliza.
Aliongeza kuwa hata mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, ana jini wake ambaye anaitwa Subiyani, ambaye yeye (Sheikh Yahya) amemuona na anamtambua.

Juzi katika mikutano yake ya kampeni, Dk. Slaa alimtaka Rais Kikwete kumkemea mnajimu huyo kwani asipofanya hivyo wananchi wanaweza kuamini kile kilichosemwa na mtabiri huyo.
[/QUOTE]


My Take.
Huyu Mchawi sasa na cross boda,na JK anachekacheka tu kwa kauli za huyu mwanga,
Mbona hasemi Mwanza alianguka kwa sababu gani,tusidanganywe na huyu mwanga,JK ni mgonjwa na zaid ya Jangwani kashaanguka zaid ya Mara 2 tayar ila wanaficha tu,sasa sijui jini la jk LINAITWA NANI VILE
 
Back
Top Bottom