OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Katika miaka zaidi ya 15 sasa ya kuipenda na kuifuatilia Chadema, nimekuwa nikisikia na kusoma kuwa malengo yake makuu yamekuwa ni;
Kushika Dola; Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.
Mh. Mbowe katika miaka yote hakuna alichotimiza hata kimoja. Kama kiongozi wa taasisi unaposhindwa kutimiza malengo ya taasisi anayoiongoza katika misimu kadhaa, ni dhahiri kwamba mbinu na jitihada zako zote zimegonga mwamba.
Tunaweza kusema kuna sababu zilizo nje ya uwezo wake katika kutimiza malengo hayo. Lakini inatosha kusema uwezo wako umeishia hapo katika kukabiliana na vikwazo hivyo.
Unajua chama sio familia, kwamba ukishindwa kutimiza malengo ya familia kuishi maisha mazuri hauwezi kujiuzuru nafasi ya baba. Sasa ile ni taasisi mambo ni tofauti sana.
Kwa kushindwa huko kutimiza malengo makuu ya Chama, ni tiketi ya kupumzika na kupisha wengine, na watu watakushukuru na kukuheshimu kwa mchango wako mkuu.
Ni dhahiri umeishiwa mbinu na kujisalimisha kwa Rais kwa kuamini anaweza kukusaidia kutimiza malengo ya Chama chako.
Kukubali kushiriki uchaguzi wa LG bila tume huru ni kutegemea huruma ya CCM
Tuwe wakweli, katika kipindi cha hivi karibuni Mbowe ana jipya gani zaidi ya kuita wanahabari na kutoa matamko yasiyo na impact yeyote.
Unapotaka kuendelea kuongoza licha ya kushindwa kutimiza malengo, hizo ni tamaa na uroho wa madaraka. Na mpaka hapo huwezi kujitofautisha na kina Kaguta Mseveni