Mh. Mwigulu Nchemba kutikisa Marekani na Uingereza mwezi mzima

Mh. Mwigulu Nchemba kutikisa Marekani na Uingereza mwezi mzima

Mkuu Fitinamwiko hapo umemtisha wala hawezi kuja huko DMV. Huyo ni wa kumfata huko California.....
Cali ndipo pazuri, maana LAPD wapo kama nyuki, jamaa akirusha ngumi tuu, tumsahau. Freedom of speech na wanaTanganyika tupo and CCTV kila kona. Wenye ratiba wekeni hapa tumuonyeshe, sababu inayomfanya JK na Membe kukimbia mikutano ya hadhara DMV
 
Mwigulu amesikia Dr Slaa anaenda Marekani nae anamfata anafikiria Dr anamaind Uliberali?

Poor Mwigulu
Both are wanted, wote wataonja joto la jiwe. Kama wapo smart na wanajua kujibu maswali wasiogope
 
Cali ndipo pazuri, maana LAPD wapo kama nyuki, jamaa akirusha ngumi tuu, tumsahau. Freedom of speech na wanaTanganyika tupo and CCTV kila kona. Wenye ratiba wekeni hapa tumuonyeshe, sababu inayomfanya JK na Membe kukimbia mikutano ya hadhara DMV

Sijui atakuja huko na Yule Tesha aliyekuwa anazunguka naye kutafuta huruma ya wananchi kuwa amemwagiwa tindikali na CHADEMA.... Zile kesi zilikufa kwa aibu....
 
Lazima TUTAREPORT HII KWA LAPD KWAMBA WANAKUJA KUFANYA KAMPENI USA TUTAONA
 

MWIGULU NCHEMBA APASUA ANGA KIMATAIFA,SASA KUTIKISA MAREKANI NA UINGEREZA ZAIDI YA MWEZI MMOJA ---KUIMARISHA CCM KIMATAIFA,KUZUNGUMZA NA WATANZANIA KWENYE MATAIFA HAYO MAKUBWA DUNIANI.
CHADEMA WAWEWESEKA,YEYE AAHIDI KUKAZA KAMBA MWANZO MWISHO NDANI NA NJE YA NCHI.
nchemba.jpg
Ni kweli,ni uhakika,ni dalili za wazi kuwa Mh.Mwigulu Nchemba sasa hakamatiki,ni moto wa kuotea mbali katika siasa za nchi hii.Akabidhiwa beji ya kuimarisha chama kimataifa.Camera yetu imenasa habari za uhakika kuwa ,Mbunge wa Iramba Mgharibi na Naibu katibu Mkuu wa CCM-TANZANIA BARA Mh.Mwigulu Nchemba anaanza rasmi ziara yake ya kikazi,ziara ya kujenga na kuimarisha chama cha mapinduzi kimataifa,Ziara ya kuzungumza na vyama rafiki wa CCM ndani ya Marekani na Uingereza, ziara ya kuzungumza na watanzania kule kule waliko “MAREKANI NA UINGEREZA”.

Mwigulu Nchemba anategema kuanza ziara yake siku ya kesho katika majimbo mbali mbali ndani ya Marekani na baadae kuelekea Uingereza katika miji ya West London,Birmigham,Reading Na Manchester kwa kazi maalum zifuatazo.

1.Mbunge huyo mwiba mkali kwa CHADEMA anategemea kuzunguka zaidi ya Mwezi Mzima Marekani na uingereza kufungua matawi mbalimbali na kuzungumza na wanachama wa CCM Katika Mataifa hayo makubwa mawili Duniani.


2.Pia Mh.Mwigulu Nchemba anategema kwenda kukutana na viongozi wa juu wa vyama vikubwa na vikongwe vya mataifa hayo mawili,Vyama rafiki vya CCM ndani ya Marekani na Uingereza.Hii ni fusa ambayo itatumika kujenga uimara wa CCM kidiplomasia hasa kwenye siasa za kimataifa.


3.Mbunge huyo anategemea kushiriki mkutano wa UN unaotegemea kufanyika mwishoni mwa Mwezi huu ndani ya WASHINGTON D.C (Hapa anategemea kupata uzoefu wa kukaa na kujadili mambo na mataifa makubwa duniani na viongozi wenye beji za heshima mbalimbali katika ulimwengu huu).


4.Pia Mh.Mwigulu Nchemba anategemea kuzungumza na watanzania karibia wote wanaoishi ndani ya nchi hizo mbili.Katika mambo muhimu anayokwenda kuzungumza ni pamoja na Katiba mpya,Maendeleo ya kiuchumi ndani ya Taifa letu,ajira,Amani na mwenendo wa siasa ndani na nje ya Tanzania.Pia anakwenda kujadiliana na watanzania maisha yao nje ya nchi na changamoto wanazokutana nazo.Kubwa zaidi anakwenda kuzungumza uimara wa CCM na uhakika wa kuendelea kuongoza nchi na namna watakavyobwaga upinzani kwenye uchaguzi ujao kwa sababu Upinzani Watanzania haujitambui,hawana malengo,ni vyama vyenye ubinafsi na ufamilia ndani yake hivyo havifai kupewa nchi.

KUWEWESEKA KWA CHADEMA,Paparazi wetu amenasa tetesi kuwa Viongozi wa juu wa CHADEMA wamesikia Taarifa za Mwigulu Nchemba kutua Marekani na Uingereza,jambo hilo linaonekana kuwapa wakati mgumu sana viongozi wa CHADEMA na kupelekea kufanya vikao vya ghafla vya hapa na pale na kufikia maamuzi ya kumwmbia Dr.slaa naye afunge ziara kwenda marekani siku tatu akajaribu kujibu mapigo ya Mh.Mwigulu Nchemba.
Kuweweseka huku kwa CHADEMA si mara ya kwanza,kila mmoja anakumbuka kuwa Mh.Mwigulu Nchemba aliporejea kutoka china baada ya kukutana na viongozi wa juu wa kikomunisti wa nchi ile,CHADEMA waliloa jasho,wamekuwa wakilia kila siku kuwa Mwigulu anawadhoofisha kisiasa na wamekuwa wakisema alikwenda china kwa lengo maalumu la kujifunza siasa za kisayansi.JE MWIGULU NCHEMBA AKIREJEA KUTOKA MAREKANI NA UINGEREZA CHADEMA MTAPONA KWELI???Mziki wa China tu imewafanya chadema wachuje kiasi kwamba inaonekana sio chama cha upinzani tena.Hii yote ni kazi ya mikono ya Mh.Mwigulu NChemba kuhakikisha upinzani hawafui dafu mbele ya CCM na kweli imewezekana.
Je ikirejea kutoka ziara ya Marekani tutegemee nini kama sio kifo cha chadema ama kusambaratika kabisa???
8E9U6377xx.JPG

Duru za habari zainaonesha wazi kuwa Mh.Mwigulu Nchemba ndiye kijana anayeandaliwa na watu wakubwa wanchi hii kuchukua nafasi ya Urais,Rejea kauli ya JK kuwa nchi hii hatamuachi mtu Mzee.BASI kaaa ukijua kuwa Mh.Mwigulu Nchemba anaandaliwa kiti cha kugombea Urais,na vijana wa CCM wanasubiria kwa hamu sana kuona Mbunge huyo anatajwa kuwa ndiye atapeperusha bendera ya CCM kwenye kiti cha Urais.
Hii ya Urais inaonekana kuwa mwiba sana Kwa CHADEMA kutokana na namna wanavyomuogopa Mbunge huyu,iwapo yeye ni mbunge tu amewashinda kisiasa kiasi hiki,Je akiwa Rais wanchi tutegemee kuiona chadema tena??Tusubiri macho yetu tu kuona chadema na vyama vya upinzani vikitafuta njia mbalimbali za kukimbilia.

Nilipojaribu kumtafuta Mh.Mwigulu Nchemba kuhusiana na ziara hii kama ni kwelu au la!!akaniambia “Ni kweli naeleka kikazi zaidi huko Marekani na Uingereza,napeperusha bendera ya nchi yangu na chama changu kimataifa,Nakwenda kukutana na viongozi mbalimbali wa vyama rafiki na CCM,nakwenda kuzungumza na Watanzania wenzangu,nakwenda kuimarisha chama na kufungua matawi ya CCM huko nje ya nchi,Nimezaliwa kwaajili ya kulitumikia Taifa langu na chama change CCM,Na furaha yangu ni kuona wale ninaopambana nao kwenye siasa wanakasirika kila siku kwani ni ishara ya wazi kuwa nawapiga kisawasawa na nitaendelea kufanya hivyo bila kukata tamaa.” alidokeza.
7891139_orig.jpg

MY TAKE ::Mh.Mwigulu Nchemba anaziwezea sana siasa za nchi hii,na swaga zake za kijamaa “Chegua Vara,Fidel Castro n.k” atafika mbali sana.Na kwa Taifa hili lenye vyama vibovu vya upinzani tunahitaji mtu wa aina ya Mh.Mwigulu Nchemba.Huyu mbunge hana cha kulaza damu,yeye ni kazi kazi,ni MORINGE SOKOINE MWINGINE NDANI YA TAIFA LETU.
ASANTE.

KWANZA; Jaribu kweli kuongelea hiyo ziara kuwa ni ya kikazi na sio ya KICHAMA... KISIASA sababu anajulikana ni yuko upande wa na ni kibaraka wa WACHINA hadi kuvaa kofia zao kuja MAREKANI ni lazima kuwe na sababu Muhimu zaidi ya kuzunguka kutembelea watanzania kama ni hivyo basi hata pata hiyo VISA hata kidogo

Na hao CHADEMA hawana cha kuhofia chochote; Sababu katiba ya AMERICA hairuhusu vyama vya kisiasa kufanya campaign kwenye ARDHI ya MAREKANI labad aje kwa jina lingine na sio kuwatembelea watanzania wana CCM; mtashitukia AMEPIGWA VISA NON-GRANTA.

Kama Mmezoea kuishi kwenye nchi isiyo na sheria kama Tanzania kila kitu ni kufyatuka fyatuka tu USA is a different chapter hapo atajiadhirisha MWENYEWE... Labda kwenda CHINA hata hitaji hizo VISA...'


Sijui kwanini WATANZANIA jinsi miaka inavyoendelea na technologia zinavyoendelea watanzania tunazidi kuwa mambumbumbu na kutojua chochote, tunadhani CCM na kina MWINGULU na NAPE ndo MWISHO DUNIANI hawana pingamizi lolote duniani...

LOOOSER's!!!!!
 
We kweli taahira,
Yaani unamzungimzia Mwigulu na Urais katika context ya Kiushindani zaidi against CDM na sio uwezo wake wa kuongoza Nchi.

Labda kwa kua unadhani anaiweza CDM ndio kiwe kigezo cha kua Rais na sio uelewa wake wa mambo na matatizo yanayowakabili Watanzania na utatuzi wake.
 
"3. Mbunge huyo anategemea kushiriki mkutano wa UN unaotegemea kufanyika mwishoni mwa Mwezi huu ndani ya WASHINGTON D.C (Hapa anategemea kupata uzoefu wa kukaa na kujadili mambo na mataifa makubwa duniani na viongozi wenye beji za heshima mbalimbali katika ulimwengu huu). "
Huu ni ushahidi kuwa hii habari imeandaliwa na Bi Juliana Shonza. Nani alikwambia kuwa mikutano ya UN hufanyikia WASHINGTON DC? Rudi chuoni ukatoe matope yaliyoganda katika ubongo wako.
 
'Ndevu bila kuwa na pesa ni uchafu'.- Dr.Salmin Amour aka Commandoo 1995
 
Kesi za ugaidi na tindikali mmechemsha mmeamia kwenye ngonjera nyingine? Majoka ya kibisa Hamna madhara.
 
Sijui atakuja huko na Yule Tesha aliyekuwa anazunguka naye kutafuta huruma ya wananchi kuwa amemwagiwa tindikali na CHADEMA.... Zile kesi zilikufa kwa aibu....
Hilo ni moja ya maswali atakayoulizwa, uchunguzi ulikuwa bado haujakamilika, alijuaje ni chadema walihusika?
 
acheni kuropoka nyie akina dada, awe rais wa nchi ngani !!!!!!!!!!!!!!! ,,,,ccm bana. j.makamba kashinda rais wa TAHILISO, mwigulu rais wa j.shonza na mtela.
 
Afadhali aondoke na ikiwezekana asirudi, mwanasiasa gani asiyependa watanzania wenzake? Mwigulu ningeomba hata apate ajali mbaya afe, hana la maana kwa taifa letu, zaidi ya kuwatetea mafisadi na kuua watanzania wasio na hatia!
 
Nchembe kutikisa Marekani na Uingereza?Wewe Mwandishi lazima utakuwa hamnazo kidogo au ulibugia kiroba wa jua kali na hujakula!Unadhani kule ni Iramba mleta mada?
 
Wamcheki airport atakuwa amebeba unga, kwao kumemshinda watu wasibebe mabox waende kupoteza muda!si aanzie Arusha?
 
Niape kuwa endapo Mwigulu Nchemba atapitishwa na CCM kuwania Urais na/au kuchukua fomu ya kugombea urais basi na mimi nitatoa kinyesi changu kigombee urais kwa kutumia tiketi hiyohiyo ya CCM kwani nitaamini kuwa CCM kila kitu kinafaa kugombea urais kama hata Mwigulu Nchemba atathubutu kugombea..

Tuache masihara na ushabiki wa kiuwehu uwehu..Hii ni nchi na siyo genge la matahira kwamba kila kitu kinaweza kumilikishwa!!
 
Ukiona mtu yeyote anayeshabikia siasa uchwara za mwigulu ujue kama sio mwizi ni mchawi au ni kichaa na anakaribia kufa. Unaweka thread ya upuuzi kutupotezea muda. Kwanza huna evidences zozote. ungeweka ratiba ya ziara ungeeleweka nahisi huyu jamaa ataenda kujifugia kwake na kutafakari jinsi alivyochangia kukidhoofisha ccm wewe unaharisha tu eti mwigulu anaenda nje ya nchi. kima we
 
atatikisa nini? Kibeliti kwani mwigulu ninani kwenye hii nchi? Na siasa zake za kubambikia watu kesi labda huko atatikisa kibeliti
 
Back
Top Bottom