Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Habari Mheshimiwa Rais,
Nikiri wazi Mimi sikua mshabiki wako, sababu pia sikua mshabiki wala mfuasi wa Chama ulichopo. Na hata ulipoanza kua Rais sikua na matumaini yoyote kwako, sababu kubwa hasa ni kua wewe ulikuwepo kwenye madaraka enzi zile za jamaa yule. Hivyo nilijua uongozi wako hautokua tofauti na wa bwana yule.
Lakini soon ulipoanza rasmi Urais nilianza kupata imani na wewe. Yapo mengi uliyoyabadilisha ambayo yalianza kuleta matumaini kwetu. Maneno ya "UNAUPIGA MWINGI" yaliibuka kila sehemu, kutokea kwa wafuasi wako mpaka sie tusio wafuasi wako.
Mama yangu Inawezekana kabisa hili la wewe kusifiwa limewatisha hata wafuasi wa Jamaa yule, shujaa wetu. Inawezekana hawafurahii kabisa uyafanyayo na sifa uzipatazo hivyo wanataka wakuharibie.
Mimi nakuomba usiingie kwenye mitego yao. Hii michezo mbona hawakuifanya kipindi hicho? Mbona waziri wako MWIGULU hakutoa wazo la miamala wala kuongeza bei za mafuta enzi za shujaa? Huku ni kukugombanisha na sisi ili tukuchukie na zile sifa za UNAUPIGA MWINGI zifutike, maana zilikua kwa namna moja ama zingine sifa hizi zinamshusha Shujaa.
Pili inaweza kua ni mipango ya 2025 Mama yangu. Watu walijipanga kuingia 2025 baada ya shujaa kumaliza kipindi chake, ila sababu umeingilia kati na kuanza upya hivyo watatakiwa kusubiri mpaka 2030. Sasa ili usifike huko ndio kukuchomokea mambo kama haya. Wanaona 2030 mbali kwao kusubiri.
Nakuomba tena Mama yangu ufikirie tena hivi vimeo unavyochomekewa, na uwe makini navyo. Mafuta ndio "trigger" ya mfumuko wa bei wa bidhaa mbalimbali za muhimu. Na kwenye miamala ya tigopesa/mpesa ndio wengi wa kipato cha kati na chini hufanya miamala yetu, sababu hatuna hela za kuweza kukaa benki.
Yangu ni hayo tu Mama yangu,