Afrikasana
JF-Expert Member
- Oct 27, 2021
- 320
- 288
Kupitia ukurasa wa ofisi ya Rais TAMISEMI,imeripotiwa kwamba waziri wa TAMISEMI amatoa maelekezo kwa katibu tawala mkoa wa Tabora kumshusha cheo mwalimu mkuu wa shule ya Makazi iliyopo wilaya ya Uyui mkoani Tabora. Ummy amedai kwamba mwalimu huyo ana hana maadili na sio muadilifu. Ninaviarifu vyombo vinavyotenda haki kwamba Tanga jiji ambapo ni jimboni kwa Ummy pameoza.
Mosi; Yupo mkuu wa shule ambaye alikua anaishi kinyumba na mke wa mwalimu mwenzake. Mkuu huyo wa shule ambaye aliteuliwa na kuwa mkurugenzi alisababisha ndoa ya mwalimu mwenzake kufa. Mwanamke huyo aliyesaliti ndoa yake na mkuu huyo wa shule nae ni mwalimu na alikua akifanya kazi shule moja na mgoni wake.
Suala hilo lilikua wazi hata wanafunzi wanajua maana mkuu huyo wa shule ambaye kwasasa ni mkurugenzi alimhamishia mke wa mtumishi mwenzie shuleni hapo. Jambo hili lipo wazi Afisa Elimu Sekondari analijua, katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC)Tanga analijua,aliyekua mkurugenzi analijua lakini hawakumchukulia hatua kwakua wote ni walewale. Je Ummy hili halijui? Kwanini huyo mtumishi mmetoa mapendekezo akapanda cheo tena bila aibu unashusha watu vyeo wakati kwako kumeoza.
Pili;Yupo Afisa Elimu Taaluma amenyanyaswa na Afisa Elimu sekondari mpaka akaamua mwenyewe kuacha kazi na ameikimbia ofisi. Ummy anajua wazi namna mama wa watu alivyonyanyasika akaikimbia ofisi. Mkurugenzi aliyeondolewa ofisini pamoja na Afisa Elimu Sekondari mbona hujawashuhulikia. Wewe husikii harufu ya ngono na malalamiko kwenye halmashauri ya Tanga?
Hujasikia malalamiko ya rushwa ya ngono? Hujui watu waliopewa nafasi kwasababu zinazoendana na rushwa? Kipi hukielewi wewe Ummy kuhusu dhuluma wanayofanyiwa watumishi jijini Tanga? Kwanini ukapigiie kelele mbali wakati kwako kumeoza pananuka? Ummy kama umemmudu kumdanganya na kumhadaa Mh. Rais sawa ila Mungu yeye yupo na hadhihakiwi. Acha kuumiza watu wanaofanya mambo madogo wakiwa mbali wakati upo ndani mwako na wahalifu unakula na kunywa nao
Tatu; Wapo makatibu wa TSC wa Tanga na Mkinga. TSC makao makuu walituma watu wao kufanya ufuatiliaji wa ubadhirifu walioufanya makatibu hao. Walikua wanasainiana na kula hela za serikali wenyewe wawili bila kushirikisha watumishi wengine kwenye ofisi zao. Hakuna hatua zilizochukuliwa aidha na wewe Ummy au katibu wa TSC Dodoma.
Je, kama hawakutaka kuchukua hatua kwanini waliingiza serikali gharama za kutuma watu kufanya ufuatiliaji? Ummy hili nalo hulijui? Au halipo TAMISEMI? Unapiga sana kelele kwenye halmashauri za wenzako ila wenzako Tanga unawachekea ili uonekane mtu poa usiena tabu. Tenda haki au tulia kama mtangulizi wako kwenye wizara hiyo, acha mbwembwe. Usipochukua hatua juu ya hayo machache huna sifa ya kutembea halmashauri nyingine kusimamisha watumishi kazi na kuwashusha vyeo wengine.
Kwaleo ninamuachia Ummy kazi ya watu wachache, nitampandia tena jukwaani akifanya uonevu.
Mh. Rais tambua kwamba Ummy anafanya maigizo na ukandamizaji hivyo anaonekana kama anakuhujumu wewe pale ambapo hatendi haki tena kwa makusudi