Hii nayo ikiendelea itazaa EPA nyingine mbele ya safari.Lazima tamaa itaingia kwenye mioyo ya watu kutaka kutafuna hela zisizo kwenye bajeti yoyoteWana JF, mbunge wa Nzega leo ametoa kauli kali pale aliposema kuwa serikali inatumia pesa bila idhini ya bunge na pia kuwashutumu mawaziri kuwa wana hila na hawana nia njema na wabunge
Katoa mifano kuwa barabara ya Chalinze serikali imetumia fedha bila ruhusa ya bunge na kuwaambia mawaziri watalaaniwa na kama hawajui kifo waangalie makaburi.
Kwa kweli Selelii ni aina ya Wabunge ambao Tanzania inawahitaji ili iendelee.Hivi kweli kila anakuwa kiongozi anafikiria kuendeleza kwao tu,kweli tutafika?
Matumizi yote ya serikali yanatakiwa kupitishwa na Bunge kupitia kwenye Bajeti za serikali, za kila mwaka. Serikali haina mamlaka ya kutumia pesa yoyote bila kufuata utaratibu huo.Serikali inapokuwa inatumia fedha zetu bila idhini yetu sisi walipa kodi, Bunge linawezaje kuiwajibisha serikali kwa ujeuri huo???? Mwenye uelewa hapa naomba anifafanulie ni vipi hapa serikali inaweza kuwajibika???
nadhani hiyo barabara imempofusha kwa sababu inapita mkoani kwakeSasa huyo Mbunge wa Tanga hana uchungu na nchi hii au naye katumwa nini na mafisadi awe anapooza mambo bungeni?
Hayo ndio matokeo ya kuendesha nchi bila sera za kueleweka. Suala la miundo mbinu lazima liwe limejadiliwa na kukubaliwa na wadau wote juu ya wapi tuweke kipaumbele.
Hii mambo ya kuamua mambo kama unashona kiraka kwenye suruali hayatatusogeza popote.
Hata wabunge wenyewe hawana lolote; wanajifanya kupiga kelele, kesho wataipitisha budget hiyo hiyo.
Tatizo la TZ ni kubwa zaidi ya tunavyofikiri hapa. Hatuna mipangilio ya maana ya kutumia pesa zetu vizuri. Mtu anaweza tu akaamua leo apeleke mradi huu kwao bila kuwa na madhara yoyote kwake. Kama tungelikuwa na vigezo vinavyoeleweka vya kuamua namna ya kujenga miundo mbinu ingelikuwa rahisi sana kuwabana hawa mawaziri.
Pia ni hasara kubwa kwa taifa, unaanza mradi mkubwa ghafla unakufa kwasababu tu aliyekuwa waziri kaondoka. Mfano ni ule uwanja wa Mbeya. Kwanini mamilioni mengi yalitumika na ghafla mradi ukasimama? Kama waziri aliyekuwepo alilazimisha kwanini hajachukuliwa hatua mpaka sasa?[/QUOTE]
Uko sahihi, lakini pia kuhusu mradi ule wa uwanja wa Mbeya tuende mbali zaidi, ni vipi kama umekwamishwa kwa sababu za kisiasa? kuonekana kama kuna mtu atanufaika kisiasa ujenzi wake ukiendelea??
Mzizi wa Mbuyu,Hayo ndio matokeo ya kuendesha nchi bila sera za kueleweka. Suala la miundo mbinu lazima liwe limejadiliwa na kukubaliwa na wadau wote juu ya wapi tuweke kipaumbele.
Hii mambo ya kuamua mambo kama unashona kiraka kwenye suruali hayatatusogeza popote.
Hata wabunge wenyewe hawana lolote; wanajifanya kupiga kelele, kesho wataipitisha budget hiyo hiyo.
Tatizo la TZ ni kubwa zaidi ya tunavyofikiri hapa. Hatuna mipangilio ya maana ya kutumia pesa zetu vizuri. Mtu anaweza tu akaamua leo apeleke mradi huu kwao bila kuwa na madhara yoyote kwake. Kama tungelikuwa na vigezo vinavyoeleweka vya kuamua namna ya kujenga miundo mbinu ingelikuwa rahisi sana kuwabana hawa mawaziri.
Pia ni hasara kubwa kwa taifa, unaanza mradi mkubwa ghafla unakufa kwasababu tu aliyekuwa waziri kaondoka. Mfano ni ule uwanja wa Mbeya. Kwanini mamilioni mengi yalitumika na ghafla mradi ukasimama? Kama waziri aliyekuwepo alilazimisha kwanini hajachukuliwa hatua mpaka sasa?[/QUOTE]
Uko sahihi, lakini pia kuhusu mradi ule wa uwanja wa Mbeya tuende mbali zaidi, ni vipi kama umekwamishwa kwa sababu za kisiasa? kuonekana kama kuna mtu atanufaika kisiasa ujenzi wake ukiendelea??
Ndilo tatizo hilo hilo, kama kungelikuwa na creteria tunafuata, hao wanaokwamisha miradi kwasababu za kisiasa ingelikuwa rahisi sana kuwabana.
Ndio hao hao niliokuwa nawaongelea kwenye ujumbe wangu, kwa uwanja wa Mbeya kuna mawili either prof. Mwandosya na awamu ya tatu walifanya makosa na ingetakiwa wawajibishwe au hao wanaoukwamisha huo mradi kwasasa ndio wenye makosa na inabidi waumbuliwe.
Haya mambo ya mradi upi utekelezwe inabidi yaondolewe kutoka kwa wanasiasa na badala yake watendaji kama makatibu wakuu na maofisa wengine wa wizara ndio wawe na nguvu kubwa. Kazi ya waziri iwe kuhakikisha taratibu zote zimefuatwa na pia kutoa mwongozo ili kinachoamuliwa kilingane na sera ya chama tawala.
Kama kawaida yake, Selelii amewawashia moto mawaziri kwelikweli.
Kawaambia kwamba kila siku wanapiga porojo tu kwamba serikali ni sikivu, mara serikali in mipango mizuri, mara mipango iko mbioni lakini wapi ni longolongo tu.Na akaishia kuwaambia Mungu atawalaani.Vilevile amesema wataalamu wa serikali ni 'bomu', akasema kupanua barabara ya Chalinze Segera wakati Chalinze dar haijapanuliwa na ndio kwenye traffic kubwa inaonyesha mipango yao ina walakini, amewataka wakachote ushauri wa bure kwao wabunge!
Baada ya kumaliza kuchangia kuna mbunge mmoja wa kutoka Tanga nadhani ni Rished Abdalla akaomba mwongozo wa spika kwamba Selelii ametumia lugha ya kuudhi/kukera kwa kuwaambia mawaziri Mungu atawalaani. Spika akaimaliza kiutu uzima.