Hayo ndio matokeo ya kuendesha nchi bila sera za kueleweka. Suala la miundo mbinu lazima liwe limejadiliwa na kukubaliwa na wadau wote juu ya wapi tuweke kipaumbele.
Hii mambo ya kuamua mambo kama unashona kiraka kwenye suruali hayatatusogeza popote.
Hata wabunge wenyewe hawana lolote; wanajifanya kupiga kelele, kesho wataipitisha budget hiyo hiyo.
Tatizo la TZ ni kubwa zaidi ya tunavyofikiri hapa. Hatuna mipangilio ya maana ya kutumia pesa zetu vizuri. Mtu anaweza tu akaamua leo apeleke mradi huu kwao bila kuwa na madhara yoyote kwake. Kama tungelikuwa na vigezo vinavyoeleweka vya kuamua namna ya kujenga miundo mbinu ingelikuwa rahisi sana kuwabana hawa mawaziri.
Pia ni hasara kubwa kwa taifa, unaanza mradi mkubwa ghafla unakufa kwasababu tu aliyekuwa waziri kaondoka. Mfano ni ule uwanja wa Mbeya. Kwanini mamilioni mengi yalitumika na ghafla mradi ukasimama? Kama waziri aliyekuwepo alilazimisha kwanini hajachukuliwa hatua mpaka sasa?[/QUOTE]
Uko sahihi, lakini pia kuhusu mradi ule wa uwanja wa Mbeya tuende mbali zaidi, ni vipi kama umekwamishwa kwa sababu za kisiasa? kuonekana kama kuna mtu atanufaika kisiasa ujenzi wake ukiendelea??
Mzizi wa Mbuyu,
Ndilo tatizo hilo hilo, kama kungelikuwa na creteria tunafuata, hao wanaokwamisha miradi kwasababu za kisiasa ingelikuwa rahisi sana kuwabana.
Ndio hao hao niliokuwa nawaongelea kwenye ujumbe wangu, kwa uwanja wa Mbeya kuna mawili either prof. Mwandosya na awamu ya tatu walifanya makosa na ingetakiwa wawajibishwe au hao wanaoukwamisha huo mradi kwasasa ndio wenye makosa na inabidi waumbuliwe.
Haya mambo ya mradi upi utekelezwe inabidi yaondolewe kutoka kwa wanasiasa na badala yake watendaji kama makatibu wakuu na maofisa wengine wa wizara ndio wawe na nguvu kubwa. Kazi ya waziri iwe kuhakikisha taratibu zote zimefuatwa na pia kutoa mwongozo ili kinachoamuliwa kilingane na sera ya chama tawala.