palalisote
JF-Expert Member
- Aug 4, 2010
- 8,335
- 1,459
Vicky ni chakula chema...
Watu wengine hawajui wanachokiongelea kwa sababu ya fitina zao uwe na uwezo wa kutofautisha kati ya Southampton University na Southampton Solent University maana hizo ni University mbili tofauti zinazopatikana katika Jiji la Southampton kwa hiyo msiingize makosa kwenye CV yake kwa sababu ya fitina zenu. Nasisitiza kwamba CV ya huyu mdada imekaa poa tu kama za watu wengine wa kawaida na anafaa kuwakilisha jamii.
Mkuu, hapo kwa Bill gates jaribu kumsoma upya. Mi nijuavyo ni kwamba alichokuwa akikisoma ndo alimoinvest though hakuwa alone kwenye hiyo iliyompelekea kuwa tajiri. Anajuwa vzr mambo yake hayo ya computer, so, tunaweza kusema aliinvest kwenye kipaji.
kuna topic imeanzishwa kuhusu jamaa mmoja from certificate to PHD,nenda na huko katoe maoni yakoChakula ya wakubwa iyo so ata CV imewekwa kiaina!
Diploma to Msc wapi na wapi?
JE unafahamu msemo " ukipandacho ndicho ukivunacho"? Nimeuliza hivyo kwasababu hoja yako inataka tuamini kwamba digrii,masters na PHD si kitu wakati hiyo si kweli. Naomba nikufahamishe tuzo za kielimu zinafaida iliyo kubwa kwa Mtu na jamii katika kukabiliana na mazingira. "The challenge is how academic qualification is converted into practical application at a particular time".It is more of challenge in our country because we are being led by failures of academic system who have con the society to belive that they have academic qualification. Kujenga nyumba ni jambo la msingi hata Kama utaamua kutoitumia. Tanzania hatujajipanga kufuatana na uwezo na tuzo za kielimu. Tufanye hivyo kwanza kwa kuwapa WATU wenye elimu za kweli nafasi za kuonyesha uwezo wao na kuwatupa wote wenye tuzo za kimagumashi tuone. NAAMINI KWAMBA ELIMU NDIO MSINGI WA KUWEZA KUYAKABILI MAZINGIRA YA DUNIA TUNAYOISHI NA HAKUNA MBADALA. Home work yako ni Bill Gates na wengine walipata elimu gani bila kupata tuzo Kama degree,masters n.k?
CV ya mtu sio issue. Ila anaweza ku-deliver? Kwani Thomas Edison aliyevumbua bulb baada ya kufanya experiment mara elfu kumi( 10,000 x) alikuwa na masters ya nini? Bill Gates ambaye ni owner wa Microsoft(unatumia Windows PC?) ana degree? Tatizo la watu walio wengi Tanzania wanaangalia CV za watu kana kwamba CV ndio zinazoleta maendeleo ya nchi yetu. CV zenye PhD,masters lukuki zimejaa maofisi ya serikali lakini zainabakia kucheza karata tu,ufanisi hamna.
Tukokane na huu upuuzi wa kufikiri kuwa CV za watu ndio kielelezo sahihi cha kumthamini mtu na thamani ya kile ambacho mtu anaweza kufanya. CV ina umuhimu wake lakini muhimu zaidi ni "deliverables"
Nadhani kuna vitu tunatakiwa kuwa wadadisi kidogo
kuna hisia zimetumika zaidi katika kujadili hiyo CV .
Ni vyema kila mtu akaukumiwa kwa HAKI hata kama ana makosa mengine.
Ukweli ni huu
kwa mtu mwenye work experience miaka 5 (managerial ) na diploma (sometime bila Diploma ) kama una uzoefu wa kiuongozi vyuo vingi UK zinaweza kukubali kusoma Masters kwa mwaka mmoja.
Kwa maana hiyo sio kweli kwamba kusoma MASTERS lazima uwe na SHAHADA ya kwanza
Mkuu shida ipo pale panapokuwa na harufu ya udanganyifu katika wasifu wa mtu, kama angekua mkweli na elimu yake hata kama ni std 7 watu wasingechonga hivi. Lakini pia lazima tufike mahali tukubali kuwa ili kwenda na kasi ya maendeleo na utandawazi na kuweza kung'amua mikataba mbalimbali na kuweza kuisimamia serikali, elimu ni muhimu mno
unamfahamu vizuri Bill Gates wewe?