Mh. Vicky Kamata CV ...[ Mungu tuokoe]

Mh. Vicky Kamata CV ...[ Mungu tuokoe]

Status
Not open for further replies.
Mi utata wangu ni kuwa alipata Msc ya Fani fulani mwaka 2008 halafu akaandika publication mwaka 2009 katika MBA Programme chuo hicho hicho!!! Mmmmh!!! Au alisoma MBA??
 
this is a very good laugh of the night today...!asante mtoa mada
 
Mtakufa nacho kijiba cha roho<<<<<roho mbaya tu Mtubu kwa mola wenu kwa usengenyaji huu
 
yawezekana
  1. kuna typing error (mistake)
  2. hiyo diploma wali equate na advanced diploma = degree
 
Watu wengine hawajui wanachokiongelea kwa sababu ya fitina zao uwe na uwezo wa kutofautisha kati ya Southampton University na Southampton Solent University maana hizo ni University mbili tofauti zinazopatikana katika Jiji la Southampton kwa hiyo msiingize makosa kwenye CV yake kwa sababu ya fitina zenu. Nasisitiza kwamba CV ya huyu mdada imekaa poa tu kama za watu wengine wa kawaida na anafaa kuwakilisha jamii.

Mkuu na pale kwenye mwaka wa kuzaliwa na kuanza shule ya msingi na penyewe pako poa?
 
Chakula ya wakubwa iyo so ata CV imewekwa kiaina!
Diploma to Msc wapi na wapi?
 
Mkuu, hapo kwa Bill gates jaribu kumsoma upya. Mi nijuavyo ni kwamba alichokuwa akikisoma ndo alimoinvest though hakuwa alone kwenye hiyo iliyompelekea kuwa tajiri. Anajuwa vzr mambo yake hayo ya computer, so, tunaweza kusema aliinvest kwenye kipaji.

Chihaya

Bill Gates hana degree, alikwenda kusoma Havard degree ya Uchumi halafu aliachana nayo. Aliomba indefinite leave of absence. Tafuta kwenye Archives za Havard University. Nina maana kuwa na degree sio issue. Deal ni kutafuta wewe ni mzuri kwenye nini halafu unakifanyia hicho kipawa chako kazi. Hayo ndio aliyofanya Bill Gates na wengine wengi. Usinelewe vibaya kwamba degree haifai
 
Analipa, mkulu anapiga vitu vya ukweli...
 
JE unafahamu msemo " ukipandacho ndicho ukivunacho"? Nimeuliza hivyo kwasababu hoja yako inataka tuamini kwamba digrii,masters na PHD si kitu wakati hiyo si kweli. Naomba nikufahamishe tuzo za kielimu zinafaida iliyo kubwa kwa Mtu na jamii katika kukabiliana na mazingira. "The challenge is how academic qualification is converted into practical application at a particular time".It is more of challenge in our country because we are being led by failures of academic system who have con the society to belive that they have academic qualification. Kujenga nyumba ni jambo la msingi hata Kama utaamua kutoitumia. Tanzania hatujajipanga kufuatana na uwezo na tuzo za kielimu. Tufanye hivyo kwanza kwa kuwapa WATU wenye elimu za kweli nafasi za kuonyesha uwezo wao na kuwatupa wote wenye tuzo za kimagumashi tuone. NAAMINI KWAMBA ELIMU NDIO MSINGI WA KUWEZA KUYAKABILI MAZINGIRA YA DUNIA TUNAYOISHI NA HAKUNA MBADALA. Home work yako ni Bill Gates na wengine walipata elimu gani bila kupata tuzo Kama degree,masters n.k?

Hakuna sehemu ambayo nimemwanisha mtu yoyote kuwa degrees sio kitu. Soma hoja yangu vizuri utaelewa,nimesema CV sio issue,issue ni nini umefanya aidha na hiyo CV au hata kama huna CV unaweza kudeliver? Read betwee lines and do not put words in my mouth
 
ni mbunge vitu maalum mkoa mpya geita sijui anawasaidiaje wa geita ndio la muhimu ila naona geita hawana wawakilishi sahihi si mliona itv siku zile yule mbunge max akizomewa tusubiri
 
CV ya mtu sio issue. Ila anaweza ku-deliver? Kwani Thomas Edison aliyevumbua bulb baada ya kufanya experiment mara elfu kumi( 10,000 x) alikuwa na masters ya nini? Bill Gates ambaye ni owner wa Microsoft(unatumia Windows PC?) ana degree? Tatizo la watu walio wengi Tanzania wanaangalia CV za watu kana kwamba CV ndio zinazoleta maendeleo ya nchi yetu. CV zenye PhD,masters lukuki zimejaa maofisi ya serikali lakini zainabakia kucheza karata tu,ufanisi hamna.

Tukokane na huu upuuzi wa kufikiri kuwa CV za watu ndio kielelezo sahihi cha kumthamini mtu na thamani ya kile ambacho mtu anaweza kufanya. CV ina umuhimu wake lakini muhimu zaidi ni "deliverables"

Bill Gates amechezea computer sana tangu umri mdogo. By 17 he was writing payroll programmes for companies.
 
Nadhani kuna vitu tunatakiwa kuwa wadadisi kidogo
kuna hisia zimetumika zaidi katika kujadili hiyo CV .
Ni vyema kila mtu akaukumiwa kwa HAKI hata kama ana makosa mengine.

Ukweli ni huu
kwa mtu mwenye
work experience miaka 5 (managerial ) na diploma (sometime bila Diploma ) kama una uzoefu wa kiuongozi vyuo vingi UK zinaweza kukubali kusoma Masters kwa mwaka mmoja.
Kwa maana hiyo sio kweli kwamba kusoma MASTERS lazima uwe na SHAHADA ya kwanza


Ndugu Vikwazo mchango wako umenileta katika swali jingine!
Je mfumo huo wa elimu unakubaliwa na Tume yetu ya Vyuo Vikuu?
Maana ,hata wenzetu wa Kenya hawana Elimu ya kidato cha Tano na Sita kama ilivyo hapa Tanzania.
Kwao, mtu akimaliza kidato cha Nne na kufaulu vema aweza jiunga Chuo Kikuu huko kwao na wanaruhusiwa kuja kusoma Vyuo Vikuu vya Tanzania.Lakini kwa Mtanzania hawezi kusoma shahada ya awali ama uzamili kwa kutumia matokeo ya kidato cha Nne pekee.
Ndugu mbunge wa viti maalumu aache kuhadaa watu.
 
mh, hyo Msc, noma, embu mnijuze namimi kama kuna namna nikapige kwani najua mimi itakua ni 6 months kwa vile nina Diploma since huyu mwenye cheti alipiga kwa 1 year
 
Mkuu shida ipo pale panapokuwa na harufu ya udanganyifu katika wasifu wa mtu, kama angekua mkweli na elimu yake hata kama ni std 7 watu wasingechonga hivi. Lakini pia lazima tufike mahali tukubali kuwa ili kwenda na kasi ya maendeleo na utandawazi na kuweza kung'amua mikataba mbalimbali na kuweza kuisimamia serikali, elimu ni muhimu mno

Nakubaliana na wewe kwa umuhimu wa elimu, ila pia ndani ya elimu tunayopata ina tatizo la kimsingi. Kwa kweli bila kujuwa huwa inatunyang'anya ule uwezo wetu wa asili wa kupigana na mazigira yetu ili kupata maendeleo ya kweli binafsi na ya Taifa. Mfano kwa kijana aliyemaliza degree ya kwanza ukiwa shs 50,000 kufungua genge la nyanya atakuona wewe wakuja kwelikweli. Yeye anataka apate white colar job pale serikali akae andike vocha ya shilingi 20,000/= hapo acheze kidogo aoneze zero iwe 200,000/= maisha yaende. Lakini hizi enterprize za magenge ndio zimewaletea watu wangi wenye elimu ya darasa la saba pale Kariakoo. Wana magorofa na biashara zinazofanya kazi vizuri tu. Mfano, The Tropical Hotel na Tropica wale wanuza vifaa vaya Electronics pale kariakoo. Hapana ubaya wa "to dream big" ila you dream big and at the same time be ralistic. Elimu ni muhimu lakini muhimu zaidi ni kile kinachozaliwa na ile elimu uliopata
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom