Baada ya kusoma hayo, sasa naanza kuunganisha dots, Ni ubalozi wa Canada ndio main sponsors kwa study tour za abroad kwa Media Council.
Nilibahatika kuingia kwenye moja ya selecting panel ya kuchagua waandishi wa kwenda study nje ya nchi, kwanza hao Wacanada wakalazimisha lazima hiyo sponsorship ipitie MCT, MCT wakaleta majina ya wale wazee wao, mimi hili nililipinga kwa nguvu zangu zote nikisisitiza wapewe nafasi waandishi vijana ambao ni active kwenye media, niliwablend hao wazee wa MCT kuwa ni 'spent force', Wacanada wakang'ang'ana na wazee wale, sasa ndio naanza kupata picha!
Ile sherehe ya siku ya uhuru wa habari ya Mwaka juzi, iliyofanyika pale hoteli moja pale Mnazi Mmoja, main sposor ni ubalozi wa Canada na alikuja balozi mwenyewe!. Sponsor wa pili ni mzee wetu mkarimu mmiliki wa media house kubwa nchini. Nilipopata wasaa kuchangia, niliwabamiza MCT wao kama regulator, kwanini wafadhiliwe na media house moja, nikaorodhesha baadhi ya madudu ya hiyo media mbele ya mmiliki, nikazimiwa kipaza sauti na kuambiwa, kauli zangu zitaonyesha ukosefu wa shukrani kwa waliotoa fedha zao. Wakati wa kupata vinywaji balozi wa Canada alizungumza nani kujua kwa nini naiblast MCT, nilimweleza.
Mwaka huu katikati, nilikuwa approched na Ubalozi wa Canada wakanipa offer ya kuwa Political Advisor na kuahidi kunilipa pesa yoyote, very unfortunately I refused thier offer because I had other plans of my own, sisi wengine, tutajifia masikini na patriotic pride kwa taifa letu, nikiangalia kumbe mambo yenyewe ni haya, sijutii kuikataa job offer yao, najisikia heri kubaki masikini jeuri kuliko kuuza utu na utaifa wetu kwa shibe ya siku moja!.
Binafsi Zitto namuaminia sana, na pia niliamini yuko bold enough to stand any test in time, aliposhambuliwa mwaka jana kuhusu abrupt personal gain ya jumba masaki, hammuer, vogue na vx kadhaa, aliorodhesha income zake ku justfy ila pia akaisusa rasmi jf, nikamsisitia kwa boldness yake, hakuwa na sababu ya kususa, alisema bado hutembelea sana jf as a guest na atachangia pale tuu, patakapobidi sana.
Wakati tukiendelea kusubiri majibu ya Zitto, wana jf, naomba tukubali, kwenye mapambano, ukijiona huwezi kuwashinda adui zako, ama una surrender, ama una retreat. Ile formular ya no retreat no surrender, ni fomuler ya kupigana mpaka risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limemwagika but at the end of the day, utasifiwa umekufa kishujaa but you are dead!. Inawezekana Zitto baada ya kujua hawezi kuwashinda, alitumia ile option ya "if you can't beat them, join them" tumpe benefit of doubt kuwa amekubali ili kuwainua wanaKogoma kielimu hivyo sasa Kigoma hawadanganyiki tena ndio maana CCM imepata kipigo, hivyo kujustify kupokea chochote kitu cha Barrick watoto wasome!.