Mhandisi Bwire: Tunairudisha DAWASA iwe ya wananchi tukishirikiana kupitia Wenyeviti wa mitaa changamoto zitaisha

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA Mhandisi Mkama Bwire amesema wanakusudia kurejesha Mamlaka hiyo kwa wananchi ili kutoa fursa na na nafasi ya kufikisha mrejesho wa huduma na kutatua changamoto za Maji ili kusaidiwa kwa haraka.

Mhandisi Bwire ameyasema hayo leo Februari 20, 2025 wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi kati ya DAWASA na Wenyeviti wa mitaa wa wilaya ya Temeke na kusema kuwa hiyo ndio agenda ya Mamlaka katika utendaji kazi wao

“Tunekusudia turudishe DAWASA iwe ni ya wananchi tunaamini tukishirikiana pamoja changamoto za kihuduna kupitia Wenyeviti wa mitaa zitaisha” alisisitiza Mhandisi Bwire

Mhandisi Bwire amesema kupitia kikao hicho watajadili changamoto za maji zilizopo katika maeneo ya Temeke kupokea mawazo na maoni ya wenyeviti juu ya suluhisho lakini kujenga mahusiano yatakayosaidia kuweza kuwa karibu baina ya DAWASA na viongozi hao.

“Lazima tuwe na mambo ambayo tunataka kushirikiana na kujenga uelewa wa pamoja tunapoenda kwa Wananchi kile anachozungumza Mwenyekiti na DAWASA azungumze hivyo” alisisitiza

Aidha Mhandisi Bwire ameongeza kuwa mamlaka hiyo imetambua umuhimu wa wenyeviti na kuelewa nafasi yao katika kurahisisha ufikishaji wa huduma kwa Wananchi na kutatua changamoto zilizopo

Pamoja na hayo Mhandisi Bwire amekiri uwepo wa changamoto mbalimbali katika Manispaa ya Temeke lakini amesema anaamini sasa itakuwa rahisi kutatua changamoto hizo kutokana na uwepo wa uhusiano mzuri baina yao.

Chanzo: Jambo TV
 
Duh naandika nafuta yaani DAWASA hii hii ambayo wamerudisha tena vioski vya maji mtaani ama wanamfungulia mteja mmoja tu maji ili auze wachukue commission ama ni DAWASA nyingine? napata tabu sana na siasa kwenye mambo ya msingi. Tuendelee tu lakini na ujinga wetu mana ndio tulichoamua.
 
Hatuna huduma ya maji wiki ya tatu sasa Bunju DAWASA
Sasa nyie huko si afadhari hata mabomba mnayo mmetandaziwa huko Chanika mpaka Kisarawe Pwani hata maji hayajafika hakuna hata mabomba ya maji watu wanahaha kutafuta maji kila kukicha na wapo Dar,
 
Back
Top Bottom