Mhandisi Ezra Chiwelesa Amesema Bunge Tanzania Kuiuzia China Gesi Asilia Kupitia Mradi wa LNG

Mhandisi Ezra Chiwelesa Amesema Bunge Tanzania Kuiuzia China Gesi Asilia Kupitia Mradi wa LNG

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
ENG. EZRA CHIWELESA - TANZANIA ITAIUZIA CHINA GESI ASILIA KUPITIA MRADI WA LNG

Mgodi wa Biharamulo StamiGold tumepokea Umeme na hasara ya Mafuta zaidi ya billion 1.2 yaliyokuwa yanatumika mgodini tuna umeme tayari, ni hatua kubwa na Mapinduzi katika Wilaya ya Biharamulo. Nina hakika Mgodi ule kwasababu ulikuwa unajiendesha kwa hasara sasa wataanza kufanya kazi kwa faida na hatimaye CSR tunaweza kuipata" - Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa, Mbunge wa Jimbo la Biharamulo

"Nawashukuru Mgodi wa STAMIGOLD wamejenga Shule ya Sekondari Mavota, wamejenga vyumba viwili vya madarasa, Ofisi na Vyoo. Nina hakika baada ya kupata umeme watafanya vingine vikubwa zaidi ili Biharamulo iweze kusonga mbele kwa kasi sawa na Maendeleo mengine" - Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa, Mbunge wa Jimbo la Biharamulo

"Biharamulo nina Vijiji 25 ila ni Vijiji 7 tu vimeunganishwa na Umeme, kasi ya uunganishaji ni ndogo sana. Kila mwananchi anataka apate umeme kwenye Kijiji chake kwa sababu Umeme ni hitaji la kila mtu kwenye kila kijiji cha Biharamulo" - Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa, Mbunge wa Jimbo la Biharamulo

"Kumpa mkandarasi mmoja Mkoa mzima kwa mradi wa REA ni kosa kubwa sana, ni mzigo mzito mno. Tafuteni mkandarasi kwa kila Wilaya maana wananchi wamechoka kusubiri wanataka waone Umeme" - Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa, Mbunge wa Jimbo la Biharamulo

"Waziri wa Nishati andaa program Maalum ya Kupeleka Umeme kwenye Taasisi. Biharamulo kuna Shule ya Sekondari Ruziba, Rusaunga, Nyakanazi, ni Shule kubwa lakini hazina Umeme. Vitu kama vituo vya afya na Shule za Sekondari ziandaliwe program yake uwapelekee umeme pekee yao tofauti na kwenye Vijiji" - Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa, Mbunge wa Jimbo la Biharamulo

"China 🇨🇳 kwa Mara ya kwanza tutaanza kumsambazia gesi Asilia kwa sababu hana Liquefied Natural Gas (LNG) anaagiza. India 🇮🇳 hana LNG anaagiza. Mataifa makubwa yanayotumia LNG kwa wingi yanaagiza. China wana nchi zaidi ya 20 ambapo wanaagiza LNG" - Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa, Mbunge wa Jimbo la Biharamulo

"China 🇨🇳, Tani moja ya LNG inauzwa kwa Dollar 💵 808. Baada ya Uwekezaji kwenye LNG Taifa litapata Umeme wa kutosha kusambaza viwandani, Ajira za kutosha, Gesi Asilia ya kusambaza kwenye Magari maana tunaelekea kwenye Nishati Safi" - Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa, Mbunge wa Jimbo la Biharamulo

"LNG inapochomwa kwenye Gari ina chini ya Asilimia 40 ya Carbonidioxide kuliko Diseli au Petroli, LNG ina kiwango chini ya 35% ya Sulfurdioxide ambazo ni gesi mbaya na zinaua. Reserve ya gesi tuliyonayo ni ya miaka 105 tunaweza kuitumia. LNG ni mradi mkubwa sana" - Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa, Mbunge wa Jimbo la Biharamulo

"Nampongeza Rais Samia kwa kuwekeza Trilioni 4.42 kwa ajili ya kuimarisha Gridi ya Taifa. Ukiunganisha na mradi wa Julius Nyerere Hydro Power Project mnaliweka Taifa sehemu nzuri na Wawekezaji wataweza kuja na kufanya kazi" - Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa, Mbunge wa Jimbo la Biharamulo

"Ilikuwa ni aibu, Mwekezaji anakuja kuwekeza na matrilioni lakini lazima aje na Genereta la Megawati moja au mbili. Tunapofanya uimalishwaji wa Gridi ya Taifa tunafanya kukatika kwa Umeme haitakuwepo" - Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa, Mbunge wa Jimbo la Biharamulo

"Mwekezaji anapokuja anachokiwaza ni kufanya biashara, kuzalisha, kupata faida na hatimaye aweze kuajiri Watanzania walio wengi. Siyo anakuja anaanza kuwaza genereta linakula mafuta" - Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa, Mbunge wa Jimbo la Biharamulo
WhatsApp Image 2023-05-31 at 19.54.24.jpeg
 
Back
Top Bottom