Mhandisi: Reli ya SGR mpya kuchukua miaka 15 kumalizika

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
February 5, 2020
Kilosa, Tanzania

Wahandisi : Reli ya kati ihamishwe toka eneo la mafuriko na pia SGR kuchukua miaka 15 kukamilisha

Wakati wa ukaguzi wa uharibifu wa njia ya reli ya kati sehemu za Gulwe na Kilosa, wataalamu wa ujenzi wa reli wamebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuitumia reli ya mkoloni kwa miaka zaidi ya 10 ijayo.


Pia Reli mpya ya SGR itachukua takriban miaka 15 kumalizwa kujengwa hilo limebainishwa ktk eneo la reli ya kati lililokumbwa na mafuriko yasiyo ya kawaida wakati jopo la wahandisi na mkurugenzi mkuu walipokuwa wanajadili athari za mafuriko na changamoto za reli ya mkoloni na reli mpya ya SGR.

Soma pia: Uzi mkuu unaoonesha yaliyojiri kwenye mradi wa SGR tangu kuanza kwake mpaka mradi ulipofikia hivi sasa

TRC inapoteza zaidi ya milioni 100 kwa siku kutokana na kusitisha safari reli ya kati. Na ili kukabiliana na mafuriko inabidi reli ya kati ihamishiwe mlimani na mlima huo unahitaji kuchongwa pia .

Uharibifu ktk eneo la mto Mkondoa ni mkubwa sana na ingawa eneo hilo la Gulwe Kilosa hakuna mvua lakini mvua kubwa zinazonyesha mikoa ya Iringa na Dodoma inaingiza kiasi kikubwa cha maji mto Mkondoa.

Source: TRC Reli TV
 
Injinia wetu mtanzania ametupa taarifa iliyoshiba kuhusu miradi yetu ya mitandao ya meter gauge MGR ya mkoloni na huu mradi wa reli mpya SGR.

Ni vizuri walipa kodi kupata taarifa muhimu kama hizi za miradi inayotumia fedha zetu za ndani za mlipa-kodi na matarajio yake lini itakamilika kabisa.

Shukrani kwa TRC Reli TV kwa kutuhusisha kwa kutupa taarifa muhimu juu ya mradi huu mkubwa kabisa wa reli.
 
Mkuu hata kakideo au kapicha kangesaidia sana kutuaminisha sisi matomaso.
 
Ninashauri, mahandaki ya SGR ambayo yameanza kuchorongwa sasa, 'tuyanunue' ili kupitisha reli ya kati, kisha Mturuki achoronge mahandaki mapya kwa ajili ya SGR.
 
Mkuu hata kakideo au kapicha kangesaidia sana kutuaminisha sisi matomaso

Isikilize hiyo clip ya video mhandisi mtanzania mwenzetu mzalendo kabisa mwenye utaalamu na mzoefu akifanya kazi pamoja na wahandisi toka Turkey na China , amerudia zaidi ya mara moja kuwa mradi wa SGR Reli Mpya mpaka ukamilike utachukua miaka hata 15 (kumi na tano).
 
Asante mkuu. Pamoja sana.
 
Nimeisikiliza zaidi ya mara moja.
Ni kweli SGR itakamilika kati ya miaka 10-15. Mhandisi amejiongeza namna ya kulisema hili.

Ameongelea namna MGR itakavyowasaidia wananchi temporarly hadi hapo mtandao wa SGR utakapokamilika. Ukisikiliza haraka huku unamfikiria bashite 😀 huwezi kuielewa implication ya anachokisema.
 
Inabidi jpm apambane sana kumuweka mtu wake ili aendeleze reli!lakini nikiingia mimi naipiga chini sitakagi ujinga kabisa!!!Stiglers wakati watu hawana maji wala umeme wa uhakika??
Stiglers wakati watu hawana maji wala umeme wa uhakika??

Umerudia kusoma ulichoandika kabla hujapost? Kwani Stiglers ni mradi wa kuzalisha nini? Sio umeme kumbe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…