- Thread starter
- #541
21 March 2026
Kisumu, Kenya
UZINDUZI WA UJENZI WA RELI MPYA YA SGR KENYA NA UGANDA
View: https://m.youtube.com/watch?v=6pGLInavAOw
Rais William Ruto na mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni, siku ya leo wameshiriki kwa pamoja uzinduzi wa Awamu ya 2C ya Reli ya Standard Gauge (SGR).
Mradi huu ni miundombinu muhimu unaotarajiwa kuleta zaidi kuimarishwa kwa muunganisho wa kikanda na kibiashara ndani ya Afrika Mashariki.
Mradi huo, utakaoanzia Kisumu hadi Malaba , ulianza rasmi Kibos katika Kaunti ya Kisumu siku ya Jumamosi, 21 March 2026 ukiashiria hatua muhimu katika mpango wa Kenya wa kupanua reli hiyo hadi mpakani na hatimaye kuiunganisha na mtandao wa reli wa Uganda.
Viongozi, wadau, na umma walikusanyika katika eneo la uzinduzi ili kushuhudia kuwekwa kwa boliti na nati ya mfano ktk taruma la reli la SGR na viongozi hao wawili.
Hatua hiyo inaashiria kuanza kwa kazi za ujenzi kwa ajili ya mradi wa miundombinu wa reli ya SGR uliokuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu.
Sherehe hiyo ilisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kikanda katika kuendeleza usafiri na maendeleo ya kiuchumi kote Afrika Mashariki.
Kiongozi wa Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) Oburu Odinga alikuwa miongoni mwa viongozi waliokuwepo na kumpokea Rais Ruto wakati wa kikao cha uzinduzi. Hii ni kuashiria kuwa mradi huu wa SGR ni mradi wa kitaifa siyo wa chana fulani cha kisiasa, hivyo unakubaliwa kwa pamoja na waKenya wote
View: https://m.youtube.com/watch?v=r_ASx8wq-Ro
Reli ya Kisumu-Malaba SGR inatarajiwa kutumika kama lango la fursa kwa Ukanda wa Magharibi, Kanda ya Ziwa, na Jumuiya pana ya Afrika Mashariki kwa kuimarisha usafirishaji wa bidhaa na abiria.
Mara tu reli hiyo itakapokamilika, inatarajiwa kurahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka bandari ya Mombasa hadi Uganda na nchi zingine zisizo na bandari, kupunguza gharama za usafiri, na kuongeza ukuaji wa biashara na viwanda kando ya ukanda huo.
Uzinduzi huo unakuja saa chache tu baada ya Rais Ruto kufanya mkutano na viongozi na wataalamu kutoka eneo la Nyanza katika State Lodge huko Kisumu, ambapo aliwafahamisha kuhusu maendeleo ya mipango ya maendeleo ya serikali.
Ushiriki huo ulikuwa sehemu ya maandalizi ya ziara yake ya siku nne ya maendeleo katika eneo hilo yenye lengo la kuharakisha miradi ya miundombinu, kiuchumi, na kijamii.
Itakapokamilika, Rais mapema Alhamisi alisema itaanzisha njia ya reli inayoendelea ya karibu kilomita 1,000 kutoka Mombasa hadi Malaba, njia ambayo haitasafirisha tu bidhaa bali pia itahakikisha nafasi ya Kenya kama kitovu cha biashara ya bara la Afrika.
"Kwa kupanua reli hii hadi Kisumu na hatimaye hadi Malaba, tunaimarisha jukumu la Kenya kama uti wa mgongo wa usafirishaji kwa nchi za kanda hii ya Afrika Mashariki na Kati," Rais alisema huko Narok siku ya Alhamisi katika kijiji cha Emurtoto, Kaunti ya Narok.
Mkuu wa nchi aliongeza kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilisha maono (visheni) ya pamoja kitaifa; maono ya kuunganisha Kenya kwa kuongeza ufanisi zaidi, kupunguza gharama ya kufanya biashara na kuiweka nchi hiyo katikati ya biashara katika eneo la Maziwa Makuu na kote barani Afrika.
Alielezea sehemu ya Narok-Kisumu yenye urefu wa kilomita 262.3, Awamu ya 2B ya mtandao wa SGR, si tu ugani, bali pia uingiliaji kati wa kushirikisha jamii pana katika uchumi wa kimkakati nchi.
Ruto alisema, njia hii ya reli ya SGR ina uwezo mkubwa wa kiuchumi, akielezea kuwa magharibi mwa Kenya huzalisha mazao ya chai, mahindi, sukari na mpunga, pia itasaidia sekta ya uvuvi yenye nguvu katika eneo la Ziwa Victoria, na huzalusha mazao ghafi muhimu kwa ajili ya usindikaji wa mazao hayo ya kilimo viwandani.

Museveni : The Problem in Africa is having Sleepy Leaders ! Wake up and lead Africa !!