MHANDISI - UWANJA WA NDEGE MWANZA UMEKOSEWA, VIGEZO HAVIKUZINGATIWA UWE WA KIMATAIFA
Hayo yameelezwa na mhandisi wakati mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Amos Makala alipofika kuangalia ujenzi unaoendelea.
Mhandisi huyo anafafanua kuwa maelekezo ya mwanzo waliyopewa wakati wa uanzishwaji wa mradi yamebainika kuwa yana mapungufu mengi kimataifa .
Mwanzoni ujenzi ulikuwa wa kuweza kupokea abiria 150 lakini ili uwanja utambulike ni wa kimataifa unatakiwa uwe na vigezo vya kupokea abiria 300 na kuendelea kwa wakati mmoja.
Majengo yaliyopo ndege ikishusha abiria wengi wengine watabaki nje wakipigwa na jua au mvua kwa kuwa hakuna nafasi ya kutosha na hilo ni pungufu mojawapo la vigezo uwanja wa kimataifa
Mkuu wa mkoa, CPA Amos Makala ahoji hata kama ilikuwa maelekezo ya wakati huo kwanini utekelezaji wa mradi haukuzingatia vigezo vya kimataifa huku kuna wataalamu pia kwanini mkoa haukushirikisha wadau kama TAA, ICAO, mashirika ya ndege, wahudumu wa abiria n.k
Bilioni 16 za ziada inatakiwa ili kubadilisha mradi jengo la abiria toka bajeti ya awali ya bilioni 13 hivyo jumla kubwa kuwa bilioni 29 kutokana na makosa yaliyofanyika awali.
Mkuu wa mkoa, CPA Amos Makala aagiza sasa mamlaka ya viwanja vya ndege na wadau wengi muhimu kitaifa na kimataifa wahusishwe na kazi hiyo iondolewe toka manispaa Halmashauri ya Ilemela Mwanza ambayo haina ujuzi na kuwa mikononi mwa taasisi na mamlaka zitakazowezesha mradi huo ukamilike kwa viwango vya kimataifa .
HISTORIA TOKA MAKTABA :
20 September 2019
Mradi wa uwanja ulianza 2019
AHADI YA RAIS MAGUFULI UJENZI WA JENGO LA ABIRIA UWANJA WA NDEGE MWANZA SASA RASMI YAANZA KUFANYIWA
Utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyotoa mnamo tarehe 15 ya Mwezi July 2019, kuiagiza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutoa Sh 2.2 bilioni na Manispaa ya Ilemela itoe Sh 1.8 bilioni na kufanya jumla Sh4 bilioni kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Hatimaye agizo hilo limeanza kutekelezwa, kwani maandalizi ya awali kuelekea ujenzi wa jengo hilo umeanza mapema hii leo.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ametembelea eneo lililotengwa kwaajili ya ujenzi wa jengo hilo la abiria kujiridhisha kwamba kazi imeanza au laa.