Wa chato haukukosewahizi ni janjajanja maana uwanja wa ndege mwanza ni karibu na mbuga ya serengeti hivyo huko mbele ingepunguza shughuli za uwanja wa Kia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wa chato haukukosewahizi ni janjajanja maana uwanja wa ndege mwanza ni karibu na mbuga ya serengeti hivyo huko mbele ingepunguza shughuli za uwanja wa Kia
Miradi babu ya wazalendo. Wazee wa legacyTOKA MAKTABA
Rais Magufuli apeleka bilioni 9 Mwanza
MONDAY , 30TH OCT , 2017
NA GERALD KITALIMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kuamuagiza Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano profesa Makame Mbarawa kupeleka bilioni 9 Mwanza katika ujenzi wa Uwanja wa ndege.
![]()
Rais Magufuli ameagiza hilo leo Oktoba 30, 2017 akiwa jijini Mwanza wilayani Ilemela katika uzinduzi wa daraja la waenda kwa miguu la Furahisha ambapo ametaka fedha zaidi ya bilioni 9 zipelekwe Mwanza katika upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza ili uwe uwanja wa kimataifa.
"Nimesikia kuwa mkandarasi anadai zaidi ya bilioni tisa, sasa Waziri naagiza mwambie huyo mkandarasi kuwa wiki hii atapata hizo fedha zote bilioni tisa kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza, nataka uwanja huu uwe uwanja wa kimataifa akamilishe uwanja huu kabla sijamaliza muda wangu, kwani asipokamilisha ndani ya muda huo hapo atalala lele, nataka wafanyabishara wa samaki wasiende nchi zingine kwa ajili ya kusafarisha samaki zao' alisisitiza Rais Magufuli.
Mbali na hilo Rais Magufuli amesema serikali yake imekusudia kujenga meli kubwa itakayobeba watu 1200, na tani za kutosha na magari katika ziwa Victoria.
Rais Magufuli yupo jijini Mwanza katika ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo ziara hiyo imelenga kuzindua daraja la Furahisha ambalo tayari limeshazinduliwa na baadaye atazindua kiwanda
Ndani ya serengeti kuna uwanja wa ndege kubwa una lami na taa watu wenye hela wanatua moja kwa moja.hizi ni janjajanja maana uwanja wa ndege mwanza ni karibu na mbuga ya serengeti hivyo huko mbele ingepunguza shughuli za uwanja wa Kia
Nyie watu wa Arusha na Dar ndio mnatatufanyia figisu, kila mwaka ni ngonjera watajenga watajenga, matamko kila siku ni mengi vitendo hakuna, kuna nini nyuma ya pazia, huu uwanja kwanini unapigwa vita?Ndugu Kitombile hii ni aibu jiji la pili kukosa international Airport hii ni fedheha kwa taifa kutozingatia vipaumbele
Nafikiri unakosea kulaumu laumu anaejenga serikali sio watu wa Arusha wala dar hahahaha 😆 tena Arusha hamna international Airport wala hakuna mpango wa kujenga??!Nyie watu wa Arusha na Dar ndio mnatatufanyia figisu, kila mwaka ni ngonjera watajenga watajenga, matamko kila siku ni mengi vitendo hakuna, kuna nini nyuma ya pazia, huu uwanja kwanini unapigwa vita?
Bora yenu mmepata hata hilo banda la kufugia kuku, sisi hata kumaliziwa godown letu wanazingua.Nafikiri unakosea kulaumu laumu anaejenga serikali sio watu wa Arusha wala dar hahahaha 😆 tena Arusha hamna international Airport wala hakuna mpango wa kujenga??!
Mkuu chato mna international Airport Mungu awape nini zaidi??Bora yenu mmepata hata hilo banda la kufugia kuku, sisi hata kumaliziwa godown letu wanazingua.
MHANDISI - UWANJA WA NDEGE MWANZA UMEKOSEWA, VIGEZO HAVIKUZINGATIWA UWE WA KIMATAIFA
Hayo yameelezwa na mhandisi wakati mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Amos Makala alipofika kuangalia ujenzi unaoendelea.
Mhandisi huyo anafafanua kuwa maelekezo ya mwanzo waliyopewa wakati wa uanzishwaji wa mradi yamebainika kuwa yana mapungufu mengi kimataifa .
Mwanzoni ujenzi ulikuwa wa kuweza kupokea abiria 150 lakini ili uwanja utambulike ni wa kimataifa unatakiwa uwe na vigezo vya kupokea abiria 300 na kuendelea kwa wakati mmoja.
View attachment 2646002
Majengo yaliyopo ndege ikishusha abiria wengi wengine watabaki nje wakipigwa na jua au mvua kwa kuwa hakuna nafasi ya kutosha na hilo ni pungufu mojawapo la vigezo uwanja wa kimataifa
Mkuu wa mkoa, CPA Amos Makala ahoji hata kama ilikuwa maelekezo ya wakati huo kwanini utekelezaji wa mradi haukuzingatia vigezo vya kimataifa huku kuna wataalamu pia kwanini mkoa haukushirikisha wadau kama TAA, ICAO, mashirika ya ndege, wahudumu wa abiria n.k
Bilioni 16 za ziada inatakiwa ili kubadilisha mradi jengo la abiria toka bajeti ya awali ya bilioni 13 hivyo jumla kubwa kuwa bilioni 29 kutokana na makosa yaliyofanyika awali.
Mkuu wa mkoa, CPA Amos Makala aagiza sasa mamlaka ya viwanja vya ndege na wadau wengi muhimu kitaifa na kimataifa wahusishwe na kazi hiyo iondolewe toka manispaa Halmashauri ya Ilemela Mwanza ambayo haina ujuzi na kuwa mikononi mwa taasisi na mamlaka zitakazowezesha mradi huo ukamilike kwa viwango vya kimataifa .
HISTORIA TOKA MAKTABA :
20 September 2019
Mradi wa uwanja ulianza 2019
AHADI YA RAIS MAGUFULI UJENZI WA JENGO LA ABIRIA UWANJA WA NDEGE MWANZA SASA RASMI YAANZA KUFANYIWA
Utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyotoa mnamo tarehe 15 ya Mwezi July 2019, kuiagiza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutoa Sh 2.2 bilioni na Manispaa ya Ilemela itoe Sh 1.8 bilioni na kufanya jumla Sh4 bilioni kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Hatimaye agizo hilo limeanza kutekelezwa, kwani maandalizi ya awali kuelekea ujenzi wa jengo hilo umeanza mapema hii leo.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ametembelea eneo lililotengwa kwaajili ya ujenzi wa jengo hilo la abiria kujiridhisha kwamba kazi imeanza au laa.
Chato sio Mwanza.
Mkuu chato mna international Airport Mungu awape nini zaidi??
Utawalaumu hao TAA, hapo kuna shida na hujuma zinaanzia juu huko serikali kuu, na huo uwanja hutokuja kujengwa labda tusubiri hawamu nyingine na kama ukijengwa litajengwa kama kibanda umiza cha kuangalizia mpira.February 2024 mkataba kusainiwa sasa hivi ni Machi 2024 huyu TAA na Uchukuzi wana dharau sana,hata kwa Rais na Mkuu wa Mkoa,waendelee tu hatimaye watavuna wanachotaka
😂😂😂😂😂Hivi kuna utashi wa kisiasa kweli kujenga uwanja huu,mbona Songwe na Arusha vitu vikubwa vimeteremshwa hapo. safari hii CCM na Serikali vitaumbuka kwa huu uwanja wa ndege wa Mwanza.