Mhandisi: Uwanja wa ndege Mwanza umekosewa, vigezo havikuzingatiwa

Maagizo ya engineer Magufuli kila wakati yameleta hasara kubwa ngoja tutasikia mengi.
 
Hili nalo litapita, bil 9 + bil 4 = bil 13, kiuhalisia hilo jengo lililokosewa, ambapo cha kushangaza linasimamiwa na halmashauri, badala ya TAA, litakuwa limetumia kiasi kidogo, nyingine zimegawanywa kuanzia juu hadi chini.
CAG analijua hili?
 
Nilitegemea enzi za JPM angewekeza zaidi kwenye huu uwanja kuliko kule Chato. Kwa geografia yetu tayr kaskazini Kuna uwanja wa kimataifa, Kanda ya pwani upo Dar, Kanda ya kusini Songwe. Ilibidi Kanda ya kati kwa maana ya Dodoma na maono yake ya kufanya kuwa makao makuu na angemalizia na Kanda ya Ziwa ambayo tayari Mwanza palishaanza kuonekana.
 
Watatuwekea zile ngazi zinazo seleleka? Mungu wangu miguu yetu! Nawaza nikiwa ukerewe
 
Jengo hili lilikosewa tangu Mwanzo baada ya kuwabagua makusudi TAA, ICAO na wataalam wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi,nadhani hatua ya haraka Bw Amos Makala akabidhi mradi kwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, isiishie kwenye maneno kwa vile hili la kukabidhi tumeliskia kuanzia wakati wa Adam Malima,tunataka utekelezaji haraka,tuache siasa. Lakini pia nashauri wataalam wizara ya ujenzi/uchukuzi wawe na mchoro wao maridadi unaokidhi mahitaji na viwango vya kimataifa bila kuingiliwa na serikali ya mkoa tena. Waliisha chemsha hawana jipya. zaidi ya kuendekeza upigaji.
 
Miradi babu ya wazalendo. Wazee wa legacy
 
issue ya uwanja wa ndege wa Mwanza umeishinda serikali ni bora ku declare wazi taifa lijue kuwa imeshindikana, kuna hujuma kubwa kwenye uwanja huu. Awamu zote 6 zimeshindwa kweli haya ni maajabu.
 
hizi ni janjajanja maana uwanja wa ndege mwanza ni karibu na mbuga ya serengeti hivyo huko mbele ingepunguza shughuli za uwanja wa Kia
Ndani ya serengeti kuna uwanja wa ndege kubwa una lami na taa watu wenye hela wanatua moja kwa moja.
Wala shida sio KIA na kama hujui kia una operate under capacity hadi sasa. Pili watalii wetu wengi wanashukia kenya na kuvuka na magari. Upo hapo?? Tunahitaji maboresho mengi
 
Ndugu Kitombile hii ni aibu jiji la pili kukosa international Airport hii ni fedheha kwa taifa kutozingatia vipaumbele
Nyie watu wa Arusha na Dar ndio mnatatufanyia figisu, kila mwaka ni ngonjera watajenga watajenga, matamko kila siku ni mengi vitendo hakuna, kuna nini nyuma ya pazia, huu uwanja kwanini unapigwa vita?
 
Nafikiri unakosea kulaumu laumu anaejenga serikali sio watu wa Arusha wala dar hahahaha πŸ˜† tena Arusha hamna international Airport wala hakuna mpango wa kujenga??!
 
Nafikiri unakosea kulaumu laumu anaejenga serikali sio watu wa Arusha wala dar hahahaha πŸ˜† tena Arusha hamna international Airport wala hakuna mpango wa kujenga??!
Bora yenu mmepata hata hilo banda la kufugia kuku, sisi hata kumaliziwa godown letu wanazingua.
 
Hizo nyingine ni bwebwe tu kinachotakiwa hapo ni hizo bi. 16 kuna watu wanamgao wao hapo..
Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake
 
February 2024 mkataba kusainiwa sasa hivi ni Machi 2024 huyu TAA na Uchukuzi wana dharau sana,hata kwa Rais na Mkuu wa Mkoa,waendelee tu hatimaye watavuna wanachotaka
 
February 2024 mkataba kusainiwa sasa hivi ni Machi 2024 huyu TAA na Uchukuzi wana dharau sana,hata kwa Rais na Mkuu wa Mkoa,waendelee tu hatimaye watavuna wanachotaka
Utawalaumu hao TAA, hapo kuna shida na hujuma zinaanzia juu huko serikali kuu, na huo uwanja hutokuja kujengwa labda tusubiri hawamu nyingine na kama ukijengwa litajengwa kama kibanda umiza cha kuangalizia mpira.
 
Hivi kuna utashi wa kisiasa kweli kujenga uwanja huu,mbona Songwe na Arusha vitu vikubwa vimeteremshwa hapo. safari hii CCM na Serikali vitaumbuka kwa huu uwanja wa ndege wa Mwanza.
 
Hivi kuna utashi wa kisiasa kweli kujenga uwanja huu,mbona Songwe na Arusha vitu vikubwa vimeteremshwa hapo. safari hii CCM na Serikali vitaumbuka kwa huu uwanja wa ndege wa Mwanza.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…