DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said ametoa rai kwa watumishi wa umma kubadilisha mtazamo kuhusu maisha, akisisitiza kuwa kazi, elimu na ndoa ni Ibada na hivyo vinahitaji kutekelezwa kwa moyo, weledi na nidhamu.
Mhandisi Zena ametoa kauli hiyo katika mkutano wa mwaka wa Wataalamu wa Rasilimali Watu na Utawala katika Utumishi wa Umma, unaoendelea kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).
“Kazi ni ibada, elimu ni ibada, ndoa ni ibada (...) Ibada ni kila kitu tunachokifanya ambacho kinamfuraisha Mwenyenzi Mungu, msiende kuonesha ufundi kwenye michepuko, mnaingia kwenye dhambi,” amesema Mhandisi Zena Ahmed Said
Amesema utumishi wa umma unahitaji mtazamo mpya unaozingatia maadili, heshima na uwajibikaji si tu kazini bali hata katika maisha binafsi, ikiwemo ndoa.