Mitambo ya Dowans ina miaka mitatu tangu iletwe TZ na si tangu ianze kutumika. Ilitumika kwa zaidi ya miaka 10 huko ilikotoka kabla ya kuletwa TZ. Ilikarabatiwa na kupigwa rangi tu. Unajua bei ya umeme ambayo Tanesco hulipa kampuni binafsi, hutegemea kiasi kilichowekezwa. Aliyewekeza zaidi hulipwa bei ya juu. Hivyo kampuni iki-inflate bei ya mitambo na hivyo ku-inflate gharama halisi za uwekezaji, hudai bei ya juu kuliko hali halisi. Na hii ndiyo inayosababisha bei ya umeme TZ kuwa juu sana, Hiki cha juu ndicho wakubwa wanagawana. Milipaji halisi ni mtumiaji wa umeme na mtumiaji wa bidhaa zinazozalishwa kwa kutumia umeme huo.
Tatizo lingine la mitambo hiyo ni kuwa bei wanayotaka kununulia ni kubwa mno kuliko hata kununua mitambo mipya kabisa. Maana yake ni kwamba kuna cha juu hapa wakubwa wanataka kugawana kwa kisingizio cha dharura. Noungana na wale wanaotaka Dk. Idriss ajiuzulu maana baada ya kutangaza kuwa Tanesco imeachana na mipango ya kununua mitambo ya dowans na kutaka shirika lisilaumiwe ikiwa taifa litaingia gizani, hakuna juhudi zozote anazofanya kuanza mchakato wa kuagiza mitambo mipya. Amekaa nasubiri taifa liingie gizani halafu aseme, si niliwaambia?
Taifa haliatingia gizani bali lintaingizwa kimaksudi gizani. Sasa hivi tayari giza limeanza wakati mabwawa yamejaa maji! Huu si mchezo wa kitoto? Hapa ndipo tunasema 'mtu mzima ovyo'