Bwana Mapesa,mimi ni mwoga sana kuzungumzia hoja za ukabila,ukanda na udini,historia inaonyesha hoja hizi zimeleta maafa mengi duniani.Hayo tuyaache turudi kwenye hoja ya msingi...Katiba.Hapo kwenye blue unauliza wakati nachukua fomu sikujua kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa katiba? let me refresh your memory,Novemba 29 mwaka jana TFF walipotoa barua yenye azimio la kubadili katiba kwa njia ya waraka mkoa wa Kagera ambao mimi ni Mwenyekiti wake ulipinga utaratibu huu kwa madai kuwa unakiuka katiba ya TFF,katiba ya TFF ibara ya 22(1) iko wazi inasema katiba itabadilishwa kupitia mkutano mkuu
TU (General assembly) na si vinginevyo. Msimamo wangu huu pamoja na hoja ya uzoefu ndivyo vilisababisha Kamati ya rufaa chini ya ya Bw Iddi Mtiginjola ikate jina langu.Kama mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF ninawajibika kuilinda katiba ya TFF,ninaamini hata wewe ungekuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF ungeniunga mkono katika hili.