Mhe. Ndejembi, Guterres wazungumzia mageuzi ya un na amani duniani

Mhe. Ndejembi, Guterres wazungumzia mageuzi ya un na amani duniani

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
IMG-20260927-WA0002.jpg


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. António Guterres, katika Makao Makuu ya Umoja huo jijini New York, Marekani, tarehe 25 Septemba 2026, ambapo amempongeza kwa uongozi wake na kusisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuunga mkono juhudi za mageuzi ndani ya Umoja wa Mataifa.

Kwa upande wake, Mhe. Guterres ameipongeza Tanzania kwa kuwa mshirika muhimu wa Umoja huo na kuthamini mchango wake katika amani na usalama duniani.

IMG-20260927-WA0000.jpg


Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, yakisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa Tanzania na Umoja wa Mataifa katika kuendeleza juhudi za mageuzi, amani, usalama na ushirikiano wa kimataifa.
 

Attachments

  • IMG-20260927-WA0001.jpg
    IMG-20260927-WA0001.jpg
    102 KB · Views: 15
Mimi sina any conflict na makamu ni mtu mwema sana.

Ila hiyo kichwa yake na masikio yalivyokaa ni mtu ambaye ahaminiki kabsa....

I know people na saikolojia zao kwa kuwaona...

I never saw Ndejembi..
Naamini akili yangu itanisaliti..
 
Back
Top Bottom