Kumekuwa na malalamiko lukuki kuhusu kodi na ushuru mbalimbali kwa Wafanyabiashara wa hapa nchini. Mshauri wako mkuu ni Waziri wa Fedha ambaye kwa ushauri wake anawaumiza wafanyabiashara na hii imefanya wafanyabiashara kugoma hasa pale Kariakoo. Ninavyoona mgomo huu utaenea nchi nzima kama hatua za haraka hazitachukuliwa kurekebisha kodi mbalimbali. Mhe. Rais anayekuangusha ni Waziri wa Fedha ni vema ukaanza naye kwa kumuajibisha.