Mhe. Rais: Vunja Baraza na Bunge!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Ili uwafunge goli wabaya wako. Tuanze upya kwani sasa unajua urais ni zaidi ya ving'ora na saluti.
 
Kwanza sijakuelewa!

Ujumbe ume-hang hewani na kama nimekuelewa,hili bunge unaloshauri livunjwe na baraza la mawaziri ndio wafadhili wake wamo humo.

Changanya mafisadi na wema wote sasa hata kama JK ni mpuuzi, sidhani kama anaweza ku-scoop that low otherwise he will break his backbone!
 
Fukuza hao mawaziri/manaibu na awashitaki mahakamani kama wale wa Benki Kuu walivyo fanyiwa - and those were mere clerks, at least most of them.

Fanya kweli, raisi, fanya kweli!!
 
akivunja bunge na kufukuza mawaziri sina kumbukumbu ya haraka hapa ila nahisi maana yake kikatiba tunafanya uchaguzi tena, itamfanya aitishe uchaguzi....
 
hii iko hewani kweli....ila lazima tucalculate risks na costs za uamuzi unaopendekeza mzee, kwa wakati kama huu sio busara kufanya hivyo, wapo wachache ambao kama JK ataamua kuvaa sura ya simba itamsaidia sana yeye binafsi na chama kwa ujumla...
 
Hivi kwani hii nchi ina Baraza (la Mawaziri) na Bunge (la Jamuhuri ya Muugano wa Tanzania)?

Mimi nadhani tuna Chama Tawala ambacho ndiyo Baraza na Bunge.
 
Ili uwafunge goli wabaya wako. Tuanze upya kwani sasa unajua urais ni zaidi ya ving'ora na saluti.


Unamwongelea JK huyu huyu au mwingine, "a born again President JK"? Kwa maamuzi yapi aliyofanya kwenye historia yake yanakushawishi kumpatia huu ushauri? Mimi naona unamtumia pongezi kwamba mambo yake mazuri sana kwa njia ya kuzunguka. Vinginevyo uteme mate chini!
 
Kwa sasa atafumba macho akijuaa kuwa atawabeba hadi apate second term ale vzr kwa kukomba...atoke...hana jipya masha ameharibu kazi vitambulisho amekaliaa.,.....hatoi kitu sababu kampuni yake haimo.....anakwamisha mambo yote ya watu mil 40...sababu ujinga wake bado anamchekeaa......muache aendelee kucheka cheka...ck moja akiwa kisutu tutamtaka acheke cheke nae muace akitoka labd a aondoke tz
 
nimecheka saana kwenye red hapo
 
Ili uwafunge goli wabaya wako. Tuanze upya kwani sasa unajua urais ni zaidi ya ving'ora na saluti.
Nimeipenda hii statement. Hii miaka minne ya utawala wa JK imekuwa migumu sana maana kashfa zimepamba karibu kila safu ya uongozi.Na kwa bahati mbaya karibu wengi waliokuwa karibu nae wakawa wahusishwa kwa namna mbalimbali. Kwa kiongozi kwenye mazingira yale kuchukua u-turn imekuwa ngumu sana. Kama anaonyesha nia ya kuthubutu, twamuombea kila la kheri.Yote yanawezekana kama nia ipo
 
Ili uwafunge goli wabaya wako. Tuanze upya kwani sasa unajua urais ni zaidi ya ving'ora na saluti.
Akifanya hivyo goli atafungwa yeye kwa sababu huko nje hajajipanga sawasawa na anajua adui zake are very flexible
 
JK amekuwa mwoga maana kwa sasa nguvu aliyonayo ni ya kikatiba tu ambapo kwa mfumo wa chama chake nguvu ni ya hela, hivyo ni powerless. Akivunja chochote sasa hivi, inabidi akae karibu na wenzie (wanajeshi) la sivyo anawezakupata ya Honduros
 

Kama Ngeleja alivyochaguliwa kwa kuangalia sura,si haba hata huyu masha ni sura iliangaliwa ndio maana anachekewa mpaka leo!
 
tatizo la serikali ya JK na yeye mwenyewe ni kuwa katumia muda mwingi kufukua vimeo vya Mkapa na wenzake akashahau kuwa 5 years sio nyingi sasa akivunja baraza ndo kabisaaaaaaaaaaaa anajipalia makaa ya moto..he is not strong enough to withstand the shocks
 

Jamani ataanguka tena bure. Mwacheni nkuu apunzike
 
Hivi kwani hii nchi ina Baraza (la Mawaziri) na Bunge (la Jamuhuri ya Muugano wa Tanzania)?

Mimi nadhani tuna Chama Tawala ambacho ndiyo Baraza na Bunge.

Baraza la mawaziri ni makada wa chama! Bunge limejaa chama! Hivyo akivunja vyote maana yake amekosa kudhibiti yote mawili.Hana ushawishi tena. Hivyo avunjapo maana yake anakiri kosa. Kwamba hawezi nchi, kwamba ameshindwa, kwamba na chama chake kimeshindwa. Huyu nimjuae mimi, HAWEZI!!!!!!!!!!!!
 
Akifanya hivyo goli atafungwa yeye kwa sababu huko nje hajajipanga sawasawa na anajua adui zake are very flexible

Mh Mpitanjia;
Mkuu wa kaya hawezi hata kidogo kujaribu jambo hilo. Yeye mwenyewe ni product ya hao tunaodhani anaweza kuwatimua. Mkuu, huwezi katia tawi ulilokalia mwenyewe otherwise utakuwa zuzu
 
Kama Ngeleja alivyochaguliwa kwa kuangalia sura,si haba hata huyu masha ni sura iliangaliwa ndio maana anachekewa mpaka leo!


kama ni sura tuu wapo wengi.. .
Sema ushemeji, urafiki, umtandao, ushule moja, u- national service pamoja, ndo unaharibu kazi! at last unakuta wote wanaokuzunguka wanajua siri zako mpaka rangi na aina za boxer unazopendelea kuvaa. utakoromaje hapo? utamkoromea vipi waziri ambae unamchukua mwanae kwa siri, ama mkurugenzi flani ambae binti yake anachumbiwa na mwanao? na vipi utamtimua kazi waziri aliyempa ajira mwanao?
 

Akivunja vyote ategemee kurudisha watu gani wakati wenye chama na fweza zao ndo hao hao? Ingekuwa enzi zile za chama cha wakulima na wafanyakazi ningesema kuwa Universal set yake ni kubwa na kwa hiyo anaweza kupata watu wengine. Ila kwa sasa Chama ni mali ya wafanyabiashara na baadhi ya makuwadi wanja wanja wachache basi. Hata ikibidi uchaguzi mpya ufanyike, pesa atazitoa wapi? Hujasikia kuwa Kigoda wakati akiwa treasurer wa CCM alienda kuchukua mafweza toka Malaysia kwa wezi wa IPTL? JK is powerless, mwache ajipe raha kwa kucheka cheka kidogo. Labda itampunguzia matukio ya kuzimika zimika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…