Mhe. Rais: Vunja Baraza na Bunge!

Mhe. Rais: Vunja Baraza na Bunge!

what troubles me is that JK is being considered as smart, clean, hardworker and many other positive compliments while the facts is absolute opposite
 
Mtoto,
Pengine mimi ndio sikuelewa kifungu cha sheria ulichoweka lakini inaposema hivi:- Rais hatakuwa na uwezo wa kulivunja Bunge wakati wowote, isipokuwa tu- blaaa blaa blaaa!

Nimeelewa kwamba kama moja ya kifungu hicho ipo basi rais anaweza fanya hivyo WAKATI WOWOTE. Hili neno wakati wowote linabeba uzito mkubwa zaidi kuonyesha kwamba hakuna sababu wala kusubiri maamuzi ya mahakama. Sijaona kifungu kinachomtaka raios apeleke mashtaka au malalamiko yake kwanza mahakamani inapotokea au anapoona ulazima wa kuvunja bunge kutokana na vifungu hivyo.
Ndivyo nilivyoelewa mimi, na pengine ndivyo marais wengi huvunja bunge pasipo kusubiri mahakama..Ikiwa nimeelewa vibaya naomba somo mkuu wangu.

Ni kweli kuwa anaweza kuvunja wakati wowote, kama anatimiza masharti yaliyowekwa katika hivyo vifungu. Lakini kama atavunja hayo masharti na mtu ukaona kuwa amekosea, basi una uhuru wa kwenda mahakamani kutafuta haki. Mahakama ina uwezo wa ku-stay (kuweka pause) proceedings hizo za kuvunja bunge na kusikiliza kesi. Maana kisheria, mahakama ndo mwamuzi wa mwisho wa sheria. Hivyo unaweza ku-challenge decision inayofanyika chini ya sheria. Ndo maana kuna area ya sheria ijulikanayo kama Judicial Review. Hii inakuwezesha kumpeleka mtu yeyote anayeshika public office mahakamani kama utahisi amevuka mipaka ya nguvu zake alizowekewa kisheria. Ni area iliyo interesting sana, na nadhani kwa Tanzania haitumiki kwa wingi. Since nguvu za rais zipo chini ya sheria, mwananchi yeyote ana haki ya ku-challenge maauzi ya rais pale anapodhani yamevuka mpaka. Nadhani siku rais akiamua kuvunja bunge kiholela holela, utaona kina Dr Slaa watakavyo-chakarika. Maana yeye yupo shapu sana kwenye haya maeneo ya Administration/Public Law.

Kwa kuangalia Katiba chap-chap, kama ulivyosema mwanzo ingekuwa kweli, yani rais anauweza wa kuvipa vifungu vya 91(2)(c) na (d) maana apendayo, basi nadhani kifungu cha 46A kitakuwa hakina nguvu. Kifungu hichi kinaruhusu bunge kupitisha azimio la kumuondoa rais. Kwa hiyo, kama rais atashtukia process hiyo inaendelea, basi kwa kupitia hivi vifungu vya 91 angeweza kulivunja bunge na hivyo kujiokoa. Umenipata hapo? Hivyo ni lazima kwa kupitia mahakama, tu-balance matumizi ya nguvu walizopewa kikatiba.

Ni muhimu kutofautisha kati ya policy decisions - ambazo kwa kawaida mahakama haiwezi kuziangalia, na discretion ya kumake hizo policy decision iliyowekwa na sheria - ambayo mahakama inaweza kuaangalia. Mfano mzuri ni mahakama haiwezi kuaangalia kwa nini rais kamchagua mtu fulani kuwa PM - hiyo ni discretion yake. Lakini kama mtu huyo hana sifa ya kuwa PM, chini ya sifa zilizowekwa kisheria, basi hapo unaweza ku-challenge. Kwa hiyo huwezi ku-challenge jina la mtu, bali sifa za mtu. Hii ni kwa sababu jina la mtu - ni uamuzi binafsi wa rais afanyao (discretion), lakini sifa za mtu ziko chini ya sheria. Na hivyo mahakama inaweza kuangalia kama rais amefuata sheria. Hii ndo Public Law haswa.
 
what troubles me is that JK is being considered as smart, clean, hardworker and many other positive compliments while the facts is absolute opposite

hawa wote wanasifia kwa vile yuko madarakani sasa, lakini atakapotoka utashangaa!!!
 
nadhani baraza jipya linapangwa sasa; kikao kijacho cha bunge kinaweza kuwa na baraza la mawaziri jipya.
 
nimecheka saana kwenye red hapo



Ah! unamaanisha Baraza la Mawaziri na Bunge tukufu? au yeye anatakiwa Avae sura ya mwenye maamuzi yasiyorudi nyuma na asiwe mtu wa kutetea tuuu? Au kuna ishu mimi naifikiria nitatuma thread tuijadili kama inafaa maana mimi langu jichooooooo
 
Back
Top Bottom