Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu! Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!

Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu! Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!

Hamumjui Anne Makinda, muulizeni Mzee Six.

Ingawa sijakiona hicho mnacho kielezea lakini nna uhakika kama Tundu anafanya ujeuri kwa huyo mama basi aelewe kuwa anajigeuza pweza kujipalilia mkaa mwenyewe. Ataipatapata.

InshaAllah usiku ntatazama marudio kupitia Star TV halafu ntakuja kutoa mtazamo wangu.
 
Haki sawa ndio maana yake! ckwasababu ni mwanamke kwani hata anapo pendelea chama chake nikwasababu ya kuwa mwanamke. Gamba gamba tu!
 
Wanabodi,

Leo nimepata fursa ya kuliangalia bunge live asubuhi hii kupitia TBC-1,
Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda ameshindwa kabisa kuliendesha bunge!, amepwaya sana na ameendesha kika bila confidence kabisa na mwisho wa maelezo yake, akamtaja Mhe. Tundu Lissu kama ndiye mbunge anayeongoza kwa kuleta vurugu bungeni, na Lissu aliponyanyuka kuomba muongozo wa Spika, akamvurumishia tena Spika Makombora mazito, na kama angeendela kidogo tuu!, Spika Makinda ange break down kwa machozi!. (Naamini akifika ofisini kwake, atajifungia kidogo na kuimalizia hasira yake the same way wanawake wote wanamalizaga hasira zao!.

Kwa kuzingatia sifa kuu iliyomfanya Mhe. Mama Makinda kuchaguliwa kuwa spika, huku Mhe. Tundu Lissu akiujua fika uwezo wa Madam Spika, kwanini anaendelea kumsulubisha kila apatapo fursa?!. This is not fair!.

Kwa vile Mama Makinda amepewa uspika because she is a lady, kwa uzi huu, namuomba Mhe. Tundu Lissu na wabunge wengine wa Kambi ya Upinzani, wanapokuwa na hoja za msingi, wamuaddress Madam Spika with courtesy of addressing a lady, ili ku restore confidence yake kuliendesha bunge ambapo kwa sasa, ameshindwa kabisa, amezuia hoja zote binafsi, hivyo leo bunge limekutana asubuhi tuu kwa kipindi cha maswali na majibu na kuahirishwa, natumaini kesho na keshokutwa itakuwa vivyo hivyo!, huu ni ufujaji bure wa rasilimali za Taifa!.

Nawauliza wajameni, hivi hiki anachofanya Mhe. Lissu na wabunge wengine wa upinzani, kumsubulu Madam Spika ambaye ni mwanamke bila huruma, ni sawa kweli?!.

Kiafrika, wanawanake ni ni watu wa kubembelezwa na kuonewa huruma!, hivi hawa wabunge wa upinzani ni watu wa aina gani wasio hata na huruma kwa wanawake?!, leo ilibakia kidogo tuu madam spika angelia!, jee hiki wanachofanya ni sawa kweli?!. Ni haki?!.

Nawaombeni tumtendee haki Spika wetu aendesha bunge kwa haki na kujiamini!.

Pasco.

mh! kama vile nahisi kitu hapa.....ISIJEKUWA WANATAKA KUJA NA PROPAGANDA YA KUITANGAZA CHADEMA KUWA NI ADUI WA WANAWAKE!
 
Ila bora huyu mama kuliko lile janaume nafiki lenye akili za shetani! Lijob Ndugai
 
Upinzani c uadui japo bunge letu ni uhasama mtupu chama mbele utaifa nyuma na ndiyo matokeo yake hayo, Lissu anatumia facts kupanga hoja na spika anatumia uzoefu na jazba kujibu hoja
 
Wanabodi,

Leo nimepata fursa ya kuliangalia bunge live asubuhi hii kupitia TBC-1,
Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda ameshindwa kabisa kuliendesha bunge!, amepwaya sana na ameendesha kika bila confidence kabisa na mwisho wa maelezo yake, akamtaja Mhe. Tundu Lissu kama ndiye mbunge anayeongoza kwa kuleta vurugu bungeni, na Lissu aliponyanyuka kuomba muongozo wa Spika, akamvurumishia tena Spika Makombora mazito, na kama angeendela kidogo tuu!, Spika Makinda ange break down kwa machozi!. (Naamini akifika ofisini kwake, atajifungia kidogo na kuimalizia hasira yake the same way wanawake wote wanamalizaga hasira zao!.

Kwa kuzingatia sifa kuu iliyomfanya Mhe. Mama Makinda kuchaguliwa kuwa spika, huku Mhe. Tundu Lissu akiujua fika uwezo wa Madam Spika, kwanini anaendelea kumsulubisha kila apatapo fursa?!. This is not fair!.

Kwa vile Mama Makinda amepewa uspika because she is a lady, kwa uzi huu, namuomba Mhe. Tundu Lissu na wabunge wengine wa Kambi ya Upinzani, wanapokuwa na hoja za msingi, wamuaddress Madam Spika with courtesy of addressing a lady, ili ku restore confidence yake kuliendesha bunge ambapo kwa sasa, ameshindwa kabisa, amezuia hoja zote binafsi, hivyo leo bunge limekutana asubuhi tuu kwa kipindi cha maswali na majibu na kuahirishwa, natumaini kesho na keshokutwa itakuwa vivyo hivyo!, huu ni ufujaji bure wa rasilimali za Taifa!.

Nawauliza wajameni, hivi hiki anachofanya Mhe. Lissu na wabunge wengine wa upinzani, kumsubulu Madam Spika ambaye ni mwanamke bila huruma, ni sawa kweli?!.

Kiafrika, wanawanake ni ni watu wa kubembelezwa na kuonewa huruma!, hivi hawa wabunge wa upinzani ni watu wa aina gani wasio hata na huruma kwa wanawake?!, leo ilibakia kidogo tuu madam spika angelia!, jee hiki wanachofanya ni sawa kweli?!. Ni haki?!.

Nawaombeni tumtendee haki Spika wetu aendesha bunge kwa haki na kujiamini!.

Pasco.

Kinachomuumiza ni uzembe wake wa kutaka kuficha uozo wa serikali na atakufa kwa pressure, me siko yeye alidhani Sita alikuwa anafaidi. Mburura hawa mwaka huu lazima wakione unakumbuka CDM walishasema huu mwaka ndo wenyewe wa kuionesha serikali njia.
 
Uvivu wa kufikiri wa viongozi wakuu wa bunge ndiyo chanzo cha yote haya. Dua ya kuliombea bunge ina kipengele .. . haki itendeke... haki hiyo ni kwa CCM tu? Tafakari kama wameshindwa kuongoza bunge wajiuzulu kwani lazima?
 
It is pay back time for poor Anne Makinda; no remorse no regrets at what she is going thru' period.

Kupachikwa kwake uspika kulikuwa na lengo moja tu la kuhakikisha kwamba Mzee wa "Kasi na Viwango" harudi kwenye wadhifa huo ambao alionekana kutopenda kuvumilia mbinu na hoja za kuficha maovu. nia ilikuwa kumpata HANGMAN (nyonganyonga) wa hoja za wapinzani

Bunge la 9 liloongozwa na Samuel Sitta litakumbukwa sana na kila mwananchi na hasa kila mzalendo anayechukia ufisadi, rushwa na mpenda maendeleo kwa wananchi wetu wote

Agenda ya kumpachika Anne uspika katu haikuwa kuweka historia ya kupata spika wa kwanza mwanamke, la hasha! bali kupata spika "dodoki" la kufukia uozo wa serikali kwa kunyonga hoja za wapinzani hususani baada ya Edo kugaragazwa kwa nguvu ya hoja za wapinzani na kulamzimisha kuundwa kwa kamati teule ya kuchunguza ufisadi wa richmonduli.

Kwa kuwa Anne alikubali kutumika kama "dodoki teule la kihistoria", she has to weather the storm, anavuna alichopanda, asimame kidete afanye kazi aliyopachikwa uspika kuifanya na aifanye kwa kasi na viwango ili apate nishani ya kuangamiza taifa hili.

Kama alikubali kudanganywa na Yusufu Makamba ambaye by any standards he is intellectually gray; wakati yeye Anne is a CPA na mtumishi wa umma mwandamizi kabisa! au Anne kama hakufanya SWOT analysis kabla ya kukubali wadhifa huo akili yake ikayeyukia kwenye neema na utukufu wa ofisi ya uspika; basi atulie tuli anyolewe na kizazi kipya,

Ninachomoumbea tu kama binadamu Mungu ampe ujasiri wa kuhimili vishindo ili asipate msongo wa mawazo au kiharusi akatutoka. angalau familia yake bado inamuhitaji japo sisi wengine kama wananchi tunamuona kama msaliti wa umma na nyota iliyofifia
 
Pole sana mama Makinda.
Huko ndiko kutumika ulikokubali, sometimes you hv to pay the price, and it might be against yr will.

-Where is Andrew Chenge, when u need him deadly!

-Where is Rostam Aziz when u are starving to see him!

Jikaze mama, ukilia utaniliza.
Ulichoongea pakajimmy kina ukweli kwa asilimia 100, waliomwingiza huyo mama yetu kwenye hicho kiti cha moto wameingia mitini!! Sasa wamemwacha mama wa watu anasulubiwa vilivyo n'a kina Lissu n'a Mnyika, saizi yake aipate hiyo adhabu ya usaliti, n'a yeye aliwezaje kuwakubalia kina Rostam kuhusu mpango wao mwovu wa kumng'oa Sitta?!
 
Hamumjui Anne Makinda, muulizeni Mzee Six.

Ingawa sijakiona hicho mnacho kielezea lakini nna uhakika kama Tundu anafanya ujeuri kwa huyo mama basi aelewe kuwa anajigeuza pweza kujipalilia mkaa mwenyewe. Ataipatapata.

InshaAllah usiku ntatazama marudio kupitia Star TV halafu ntakuja kutoa mtazamo wangu.
Sasa ulikuwa na ulazima gani wa kuyaandika haya yote wakati hujui hata kinachojadiliwa hapa, kama si kujivunjia heshima mtu mzima ni kitu gani? tabia hizi za kijinga ndizo zinazowaponza Wabunge wa CCM yani wanaongea halafu ndio wanafikiri badala ya kufikiri kwanza halafu ndio waongee.
 
Pasco, kuwa mwanamke sio udhaifu ila ni maumbile tu kwa ajili ya kuendeleza kizazi. Kuwatizama kina mama kama viumbe dhaifu au watu wa kubebwa na kuonewa huruma ni kutowatendea haki. Wanafanya mambo mengi makubwa yasiyomilika. Kibinadamu wapo wanaume wanyonge na wenye nguvu, kadhalika wanawake pia.

Hivyo kuja na kisingizio cha madam Spika aonewe huruma ni kutowatendea haki Watanzania na Tanzania kwa ujumla wake. Kama walimbeba Mwanamke DHAIFU kwa maslahi yao, kamwe hatuko tayari kutoitendea haki nchi yetu na waTanzania kwa kisongizio cha jinsia ya kike.
 
Bibi kiroboto!!!!!!!!!!!!!! Chezea CDM wewe,utajiuzulu mwaka huu
 
Jamani bunge ni chombo muhimu sana katika mstakabari wa nchi. Kuna ngazi ambazo huwezi kuchezea. Huwezi kuweka mtu kwenye kitu kama hicho eti kwa sababu ni mwanamke. Hii inci inahitaji maendeleo na si bora kiongozi wa jinsia fulani. Hapa tulihitaji spika wa kuliongoza bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania. Lakini kinyume chake tukaingiza fitina na ushabiki katika kumpa spika.

Kinacho hitajika hapa ni spika kama Six na si vinginevyo.
 
Sasa ulikuwa na ulazima gani wa kuyaandika haya yote wakati hujui hata kinachojadiliwa hapa, kama si kujivunjia heshima mtu mzima ni kitu gani? tabia hizi za kijinga ndizo zinazowaponza Wabunge wa CCM yani wanaongea halafu ndio wanafikiri badala ya kufikiri kwanza halafu ndio waongee.

Kinachojadiliwa nnakijuwa kwa kukisoma hapa, nilichosema ni kuwa sijakiona. Una matatizo ya uweledi au ya kusoma?
 
Back
Top Bottom