Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu! Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!

Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu! Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!

Hata ya sasa inasema hivyo na hata madam spika alichaguliwa kwa kishindo na haohao wabunge akimbwaga Mabere Marando wa chadema kwa mbali.Labda kuna kitu kingine ulikuwa unamaanisha?

Mkuu nilikuwa na maana kwamba ninachokiona hapo bungeni ni kwamba spika wa bunge anafanya kazi ya kuitetea serikali na chama tawala moja kwa moja bila kuona haya. Mimi ni CCM, lakini hatuwezi kujenga taifa makini kwa kuendesha bunge namna hii. Kama ni hivyo basi tuamue moja kwamba hakuna haja ya kuwa na vyama vingi. ukweli nimesikitishwa sana na huyu Makinda.
 
Makinda alitaka the big Apple kabite sasa cant chew....

Tindu Lissu kashamjua huyu mama na anamkomesha mpaka ahakikishe she breaks down. It seems Mama cant work vizuri under so much pressure and thats what Tindu Lisu is doing.
 
Asome alama za nyakati ajiuzuru wadhifa huo alio nao itamjengea heshima kwa jamii.
 
Pole sana mama Makinda.
Huko ndiko kutumika ulikokubali, sometimes you hv to pay the price, and it might be against yr will.

-Where is Andrew Chenge, when u need him deadly!

-Where is Rostam Aziz when u are starving to see him!

Jikaze mama, ukilia utaniliza.
 
Pasco siasa mchezo mchafu! Jioni utawakuta hivi!

IMG_4291.JPG
 
Na bado hadi ajiuzuru mwenyewe bila Shinikizo.:target:
 
Kama kashindwa kazi si aache? Anang'ang'ania nini?
 
kiti kile kinahitaji maombi ya toba kabla ya kukikalia kwani kuna dhambi ya dhuluma na kutokutenda haki inakinyemelea sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Wanabodi,

Leo nimepata fursa ya kuliangalia bunge live asubuhi hii kupitia TBC-1,
Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda ameshindwa kabisa kuliendesha bunge!, amepwaya sana na ameendesha kika bila confidence kabisa na mwisho wa maelezo yake, akamtaja Mhe. Tundu Lissu kama ndiye mbunge anayeongoza kwa kuleta vurugu bungeni, na Lissu aliponyanyuka kuomba muongozo wa Spika, akamvurumishia tena Spika Makombora mazito, na kama angeendela kidogo tuu!, Spika Makinda ange break down kwa machozi!. (Naamini akifika ofisini kwake, atajifungia kidogo na kuimalizia hasira yake the same way wanawake wote wanamalizaga hasira zao!.

Kwa kuzingatia sifa kuu iliyomfanya Mhe. Mama Makinda kuchaguliwa kuwa spika, huku Mhe. Tundu Lissu akiujua fika uwezo wa Madam Spika, kwanini anaendelea kumsulubisha kila apatapo fursa?!. This is not fair!.

Kwa vile Mama Makinda amepewa uspika because she is a lady, kwa uzi huu, namuomba Mhe. Tundu Lissu na wabunge wengine wa Kambi ya Upinzani, wanapokuwa na hoja za msingi, wamuaddress Madam Spika with courtesy of addressing a lady, ili ku restore confidence yake kuliendesha bunge ambapo kwa sasa, ameshindwa kabisa, amezuia hoja zote binafsi, hivyo leo bunge limekutana asubuhi tuu kwa kipindi cha maswali na majibu na kuahirishwa, natumaini kesho na keshokutwa itakuwa vivyo hivyo!, huu ni ufujaji bure wa rasilimali za Taifa!.

Nawauliza wajameni, hivi hiki anachofanya Mhe. Lissu na wabunge wengine wa upinzani, kumsubulu Madam Spika ambaye ni mwanamke bila huruma, ni sawa kweli?!.

Kiafrika, wanawanake ni ni watu wa kubembelezwa na kuonewa huruma!, hivi hawa wabunge wa upinzani ni watu wa aina gani wasio hata na huruma kwa wanawake?!, leo ilibakia kidogo tuu madam spika angelia!, jee hiki wanachofanya ni sawa kweli?!. Ni haki?!.

Nawaombeni tumtendee haki Spika wetu aendesha bunge kwa haki na kujiamini!.

Pasco.

Pasco,

Si wakati wa kuremba sasa, we should call a spade a spade. The time for Madame Speaker for doing the blunders and run the parliamentary proceedings in the way she wants has to come to an end. VIVA Chadema, VIVA Tundu Antipas Mughwai Lissu and other opposition MPs
 
Mkuu nilikuwa na maana kwamba ninachokiona hapo bungeni ni kwamba spika wa bunge anafanya kazi ya kuitetea serikali na chama tawala moja kwa moja bila kuona haya. Mimi ni CCM, lakini hatuwezi kujenga taifa makini kwa kuendesha bunge namna hii. Kama ni hivyo basi tuamue moja kwamba hakuna haja ya kuwa na vyama vingi. ukweli nimesikitishwa sana na huyu Makinda.

Kuzuia hilo mkuu ni spika kutokuwa mbunge na mwanachama wa chama chochote cha siasa.Ili asiingie kwenye kamati wala caucus ya chama chochote.Bila hivyo tutaendelea kulaumu kila siku.
 
Wanabodi,

Kiafrika, wanawanake ni ni watu wa kubembelezwa na kuonewa huruma!, hivi hawa wabunge wa upinzani ni watu wa aina gani wasio hata na huruma kwa wanawake?!, leo ilibakia kidogo tuu madam spika angelia!, jee hiki wanachofanya ni sawa kweli?!. Ni haki?!.

Nawaombeni tumtendee haki Spika wetu aendesha bunge kwa haki na kujiamini!.

Pasco.

Hapo kwenye red, nadhani hii huduma uwa inapatikana kwa mwanamume ambaye ni mume wa mwanamke husika. Kama kazi imemshinda akatafute kazi nyingine, kuachia ngazi si jambo la ajabu. Makinda sio kupwaya tu, bali kiatu kimemvaa badala yeye kuvaa kiatu. Kwa kifupi hatufai.
 
Pole sana mama Makinda.
Huko ndiko kutumika ulikokubali, sometimes you hv to pay the price, and it might be against yr will.

-Where is Andrew Chenge, when u need him deadly!

-Where is Rostam Aziz when u are starving to see him!

Jikaze mama, ukilia utaniliza.

Hivi hapa tuko jukwaa la jokes au mie ndiye nimepotea?
 
Kuna kazi nyingine ambazo mtu yeyote anaweza kuzifanya ila sio SHERIA. Kaka yangu Lissu anachofanya ni kumvuruga akili Spika, matokeo yake anajikuta amepwaya na kutoka nje ya mstari kabisa. Hii inaweza mwathiri mwanamke akajikuta ameingia P...od bila kutarajia.
 
Back
Top Bottom