Mhe. Ummy sare uleta usawa shule za serikali, mzazi anayekosa unifomu nivigumu Kupata nguo mbadala za mwanaye: Tupunguze free lunch Kwa wananchi

Mhe. Ummy sare uleta usawa shule za serikali, mzazi anayekosa unifomu nivigumu Kupata nguo mbadala za mwanaye: Tupunguze free lunch Kwa wananchi

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Aliyeanzisha uniform au sare shuleni naamini alilenga kuweka usawa baina ya maskini na tajiri lakini pia alitofautisha Kati ya Mwanafunzi na watu watoto wengine. Tunaposema asiye na sare aende shule tunakosea, tulipaswa kuwabaini wasio na unifomu mapema Tena kwa kujiandikisha ikiwemo kuweka vigezo na masharti.

Hoja ya pili nadhani tunaweza tukawa tunawalemaza sana Watanzania pale tunapotoa free lunch kwenye kila eneo kisiasa. Ifike mahalo tuwalazimishe wazazi wawajibe Kwa watoto wao. Tutumie principle ya TASAF kuwabainisha wale wanaostahili msaada na SIYO kutoa general statement. Tuwaonee huruma watoto w maskini kama tunavyowaonea huruma wakwetu.

Kutovaa uniform kunaweza kuchangia majanga Kwa kizazi chetu ikiwemo kuongezeka Kwa mimba za utotoni.

Kaya maskini zinatambulika Nchi nzima, tutumie data za mradi wa Tasaf kufanya- analysis ya ukubwa wa tatizo na kuweka Suluhu yakimfumo SIYO tamko la kisiasa.

Tamko la watoto wasio na sare wapokelewe Lina miaka kadhaa na alitekelezeki na halina msingi wa kisera wala Sheria.
 
Hilo tamko kama lilikuwepo na halikutekelezeka bado naona this time linaweza kutekelezeka.

Najiuliza, huko mashuleni patakuwa na muonekano wa aina gani? hii ni vurugu nyingine Ummy anaitengeneza.

Mavazi ya ndugu zetu huko vijijini yanajulikana kwa uchakavu, kama mtoto hana uniform basi hata nguo za kushindia nyumbani nazo kuna uwezekano mkubwa hali yake isiwe nzuri.

Hili lisipoangaliwa mapema linaweza kutengeneza precedence pakawepo na watoto wengi wasio na uniform mashuleni mbele ya safari.

Hata kama wakiweka sheria au sera, bado kwa muda uliobaki naona ni mfupi sana watoto kurejea mashuleni, sijui kwanini serikali isitafute namna ya kuwasaidia hao watoto kupata uniform wakisaidiana na wafadhili ili kuondokana kabisa na hii haya matamko.
 
Tuache nchi iende inavyoenda hata tukisema hawatasikia,wao watoto wao wanasoma shule zenye sare na utaratibu unaoeleweka,shule za serikali ndo waache walimu washindwe kutofautisha wanafunzi na vibaka! Huruma zingine ni za kipuuzi!
 
Waache watoto wasome hata kama wako uchi, sare hazina uhusiano wowote ule na Elimu!
 
Kabisa na uniform ziwe sketi za kijani mtoto anaambiwa alete masai ya purple ulishaiona wapi?
 
Naunga mkono hoja swala la sare ni la msingi sana kwa mwanafunzi hasa wa Shule ya Msingi.

Shule kwa mtoto ni pamoja na uniform, embu fikiri mtoto atajisikiaje endapo yeye peke yake darasani hana uniform. Hili jambo laweza kufanya shule kuwa chukizo kubwa sana kwa hawa watoto, shule itakuwa likitu linalodhalilisha sio kwa mtoto tu bali hata kwa wazazi.
Yapo mengi niishie hapa tu.
 
Watanzania wa kipato cha chini na kawaida wajitahidi wasizae watoto zaidi ya wawili.
 
Hawa mawaziri wanakurupuka Sana kutoa matamko ambayo hayana research bases! Aliwahi kuona wapi wanafunzi wa shule za chini na za Kati wanahudhuria shule bila uniform? Labda nchi zenye vita! Aambiwe ukweli ili atengue kauli zake zisizo na utafiti! Enzi zetu tumevaa uniform Hadi kwenye ngazi za diploma huko na hakukuwa na shida yoyote kwani watoto kutoka madaraja yote ya kitajiri na kifukara tulifanana through uniforms!
Hii dhana yake ya kukurupuka italeta shida kuu Kwa walimu na jamii kwani wengi wa watoto wasio waadilifu wataishia mitaani na kwenye magheto na watashindwa kubainika kirahisi shule wanazosoma ili kuwasaidia! Uniform humtambulisha mtoto shule asomayo na hata akipata madhara Kama ajali inakuwa rahisi taarifa kuwafikia wazazi wake!
Kiujumla huyu waziri kachemka parefu nausubiri kuona mabinti wa maeneo ya mjini wakihudhuria wakiwa wamevaa zile soksi zao za kubana makalio na vitop na wavulana wakiwa na vinjunga vyenye matundu na viraka vingi ndio atawajua vyema wanafunzi!
Kasahau umri wa Hawa adolescents ulivyo changamoto huko sekondari! Walimu jiandaeni TU kufundisha darasa la E.W.W!
 
Uniform ni kinga kwa mwanafumzi dhidi ya mafataki. Sasa mwanafumzi akivaa za nyumbani zile bodaboda za baiskeli zitawabeba huko shinyanga vijijini na kuishia kunako machaka
 
Back
Top Bottom