Mheshimiwa Diwani Haji Fundi Haji awakaribisha wawekezaji Kata ya Bondeni asema Bondeni ni salama

Mheshimiwa Diwani Haji Fundi Haji awakaribisha wawekezaji Kata ya Bondeni asema Bondeni ni salama

Ndagullachrles

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
256
Reaction score
259
Diwani wa Kata ya Bondeni Manispaa ya Moshi Mheshimiwa Haji Fundi Haji ametoa rai kwa wafanyabiashara na wawekezaji kuwekeza kwenye Kata ya Bondeni na kwamba Kata hiyo ni salama .

Ametoa rai hiyo hivi karibuni kwenye kilele cha siku ya usafi wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Bondeni .

Amesema Kata ya Bondeni inazofursa nzuri katika uwekezaji ikichagizwa na uwepo na masoko mawili makubwa ya nafaka likiwamo la Mbuyuni ambalo kwa Sasa limeboreshwa na kuwa na mwonekano mzuri pamoja na soko la Manyema.

"Sifa moja ya sisi waswahili ni watu wastaarabu sana hivyo nawakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kuja kuwekeza Bondeni ,Bondeni ni salama",alisema.
Kuhusu suala la usafi alisema usafi unajenga heshima na utu kwa wananchi wa Kata ya Bondeni.
IMG-20260920-WA0055.jpg
 

Attachments

  • IMG_20260123_121134_749.jpg
    IMG_20260123_121134_749.jpg
    1.5 MB · Views: 9
  • Mhe. haji fundi haji.mp4
    81 MB
Back
Top Bottom