Wanabodi
Naendelea na zile mada zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambazo ni mada za uzalendo kutoka kwa mzalendo wa kweli wa taifa hili. Mada ya leo ni kujadili moja ya Idara zetu nyeti sana, hapa nchini kwetu, hii ni idara yetu ya Usalama wa Taifa, TISS.
Introduction ya Mada
Hii ni mada very serious and sensitive kwasababu inaijadili idara yetu nyeti ya TISS ambayo kutokana na unyeti wake issues za idara hii huwa hazijadiliwi hovyo hovyo, wazi wazi na openly na kwa uwazi, hivyo ukiona hadi watu tunaojinasibu humu kuwa ni wazalendo wa kweli wa taifa hili halafu tukajitokeza openly waziwazi humu kuijadili TISS huku tukitumia majina yetu halisi, huu ni uthibitisho kuwa tunaleta mjadala huu kwa nia njema kabisa kwa kusukumwa na uzalendo wa kulisaidia taifa letu pale idara yetu hii nyeti, inapochafuliwa kwa kusingiziwa tuhuma za uongo, bila uthibitisho wowote, lakini pia kama ni kweli TISS inahusika, na hawa 'wasiojulikana', then tukubaliane kuwa TISS itakuwa ni imechafuka na inahitaji kusafishwa, the sooner the better!.