Mheshimiwa Lukuvi unakwama wapi Rais Magufuli akusaidie?

Team JPM

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2018
Posts
1,197
Reaction score
1,826
Miongoni mwa mawaziri wachapakazi katika serikali ya awamu ya tano, William Lukuvi hana upinzani. Hata kuna wakati Fulani alifikiriwa kustahili kuwa mrithi wa Magufuli au hata uwaziri mkuu.

Katika Wizara ya Ardhi amesaidia kutatua matatizl na kero nyingi sana mfano: Migogoro ya ardhi, upatikanaji wa hati za viwanja, upimaji na urasimishaji viwanja na mashamba.

Jana katika ziara yake kwenye mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa vigunguti alidhihirisha udhaifu wa kutisha

1. Kitendo cha kumwambia msimamizi wa ujenzi amuandikie maelezo ya kuchelewesha ukamilishaji wa ujenzi ili ampelekee mheshimiwa Rais ni udhaifu mkubwa kwa sababu HC ambao ndio wajenzi wa huo mradi wako chini ya wizara ya ardhi hivyo ripoti ya ucheleweshaji wa mradi anapaswa kuifanyia kazi yeye ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua viongozi wa NHC.

Badala ya Mheshimiwa Lukuvi kufanya maamuzi, anamsukumia mheshimiwa Rais, huu ni udhaifu na kukwepa uwajibikaji

2. Kitendo cha Mheshimiwa Waziri kumuelekeza Mkurugenzi mkuu wa NHC kumpangia majukumu mengine Meneja wa Miliki kufuatia malalamiko ya wapangaji wa NHC kutozwa kodi ya sh 100,000 bila kupewa risiti wakati NHC inapokea sh 25,000 ni udhaifu pia.

Huo mchezo wa NHC kupangisha watu kwa kodi ndogo wakati hao wapangaji wakiwapangisha wenzao kwa kodi kubwa umekuwepo kwa siku nyingi. Mheshimiwa waziri alipaswa:

1. Kuwaagiza Takukuru kuwachunguza watuhumiwa wote wa wizi huo kisha kuwachukulia hatua

2. Meneja Miliki alipaswa kupisha uchunguzi

3. Uhakiki wa wapangaji wa NHC ulipaswa ufanyike nchi nzima

4. Waziri alipaswa kuagiza matumizi ya mfumo wa Kielektroniki katika ulipaji wa kodi za NHC

5. Waziri angewapa offer ya kulipa kodi ya sh 25,000 wale wapangaji wa NHC kwa mwaka mzima kwa kufichua wizi

6. Waziri alipaswa kuwapa kinga wale wapangaji kwa kutoindolewa katika fremu zile na kutobughudhiwa na watumishi wengine wa NHC.

Kwa kifupi Mheshimiwa Waziri alicheza chini ya Kiwango hivyo Mamlaka za juu zinaweza kuingilia kati.

Ndio maana nashangaa Mheshimiwa Jembe letu katika baraza la mawaziri, unakwama wapi ukwamuliwe?
 
Wafanyakazi wengi NHC ni wezi na hawafanyi kazi yoyote zaidi ya kuiba kodi. Kulipa kwa mfumo ndio suluhisho. Pia kupunguza wafanyakazi kwa kuoutsource huduma nyingi.
 
Lukuvi? Lukuvi! Ni kazi yetu wananchi kuwajadili wanasiasa wetu.
Ukiangalia vitendo vya nyuma vya mh. huyu kabla ya Magufuli, hutaiona sababu ni kwa nini bado ni waziri. Lukuvi hakutenganishwa na lolote baya wakati wa awamu ya 4. Hakuwa objective ktk utendaji wake. Kumbuka suala la Zanzibar akiwa kanisani.

Tunachokiona sasa hivi ni kuigiza boss anachokitaka maana naamini hiyo siyo tabia yake. Ni kweli kwa upande wa ardhi amefanya mengi mazuri, lakini ni kwa kulazimika na siyo tabia au hisia zake za kweli. Sitaona ajabu kama itakuja fahamika baadaye kwamba anamiliki viwanja 100 ndani ya mipaka yetu.
 
Hayo matatizo ya NHC ni madogo sana na kama Waziri William Lukuvi angeyashughulikia angejishushia heshima yake, kwanza namshauri aachane na uchafu wa Mchechu Nehemia km aliweza kumtoa inatosha
Kodi niliskia pale Shekilango ni 125,000/ sasa leo waliotoa siri wapange 25,000 badala ya Laki ni kichekesho
huko kuna bifu lenu au wivu
Wazyri ana mambo mengi ya kushughulikia Ardhi ya Tanzania yenye Mashamba, Viwanda, Majumba sasa akaceze na NHC
HEBU INGIA HAPA Waziri Lukuvi awasimamisha maafisa ardhi 183 kupisha uchunguzi
 
Nyie mnajua utendaji wa waziri kwenye baadhi ya mambo unaishia wapi?
 
Hayo matatizo ya NHC ni madogo sana na kama Waziri William Lukuvi angeyashughulikia angejishushia heshima yake, kwanza namshauri aachane na uchafu wa Mchechu Nehemia km aliweza kumtoa inatosha
Kodi niliskia pale Shekilango ni 125,000/ sasa leo waliotoa siri wapange 25,000 badala ya Laki ni kichekesho
huko kuna bifu lenu au wivu
Wazyri ana mambo mengi ya kushughulikia Ardhi ya Tanzania yenye Mashamba, Viwanda, Majumba sasa akaceze na NHC
HEBU INGIA HAPA Waziri Lukuvi awasimamisha maafisa ardhi 183 kupisha uchunguzi
Alipowasimamisha maafisa Ardhi kupisha uchunguzi, nini kiliendelea?, Uchunguzi utaisha lini?.
 
Huenda ametuma ujumbe bila wewe/sisi kuelewa, huenda ameagizwa na mkuu kuwa apelekewe hiyo barua/taarifa.
Awamu ya tano hili linawezekana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miongoni mwa mawaziri wachapakazi katika serikali ya awamu ya tano, William Lukuvi hana upinzani. Hata kuna wakati Fulani alifikiriwa kustahili kuwa mrithi wa Magufuli au hata uwaziri mkuu.

Katika Wizara ya Ardhi amesaidia kutatua matatizl na kero nyingi sana mfano: Migogoro ya ardhi, upatikanaji wa hati za viwanja, upimaji na urasimishaji viwanja na mashamba.

Jana katika ziara yake kwenye mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa vigunguti alidhihirisha udhaifu wa kutisha

1. Kitendo cha kumwambia msimamizi wa ujenzi amuandikie maelezo ya kuchelewesha ukamilishaji wa ujenzi ili ampelekee mheshimiwa Rais ni udhaifu mkubwa kwa sababu HC ambao ndio wajenzi wa huo mradi wako chini ya wizara ya ardhi hivyo ripoti ya ucheleweshaji wa mradi anapaswa kuifanyia kazi yeye ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua viongozi wa NHC.

Badala ya Mheshimiwa Lukuvi kufanya maamuzi, anamsukumia mheshimiwa Rais, huu ni udhaifu na kukwepa uwajibikaji

2. Kitendo cha Mheshimiwa Waziri kumuelekeza Mkurugenzi mkuu wa NHC kumpangia majukumu mengine Meneja wa Miliki kufuatia malalamiko ya wapangaji wa NHC kutozwa kodi ya sh 100,000 bila kupewa risiti wakati NHC inapokea sh 25,000 ni udhaifu pia.

Huo mchezo wa NHC kupangisha watu kwa kodi ndogo wakati hao wapangaji wakiwapangisha wenzao kwa kodi kubwa umekuwepo kwa siku nyingi. Mheshimiwa waziri alipaswa:

1. Kuwaagiza Takukuru kuwachunguza watuhumiwa wote wa wizi huo kisha kuwachukulia hatua

2. Meneja Miliki alipaswa kupisha uchunguzi

3. Uhakiki wa wapangaji wa NHC ulipaswa ufanyike nchi nzima

4. Waziri alipaswa kuagiza matumizi ya mfumo wa Kielektroniki katika ulipaji wa kodi za NHC

5. Waziri angewapa offer ya kulipa kodi ya sh 25,000 wale wapangaji wa NHC kwa mwaka mzima kwa kufichua wizi

6. Waziri alipaswa kuwapa kinga wale wapangaji kwa kutoindolewa katika fremu zile na kutobughudhiwa na watumishi wengine wa NHC.

Kwa kifupi Mheshimiwa Waziri alicheza chini ya Kiwango hivyo Mamlaka za juu zinaweza kuingilia kati.

Ndio maana nashangaa Mheshimiwa Jembe letu katika baraza la mawaziri, unakwama wapi ukwamuliwe?
Naona kwa mbali ukinyemelea nafasi ya Waziri wa Ardhi ya Mh: Lukuvi
 
Alipowasimamisha maafisa Ardhi kupisha uchunguzi, nini kiliendelea?, Uchunguzi utaisha lini?.
kuendelea na nini tena? Ajira hakuna na ni sawa na wale waliofoji vyeti vya F4
wwunakuta kiwanja kikubwa cha Taasisi kinadaiwa 23M kwa miaka karibu mi4 unaambiwa toa 1M tukufutie Deni, na kweli wanashusha hadi 7M
Saver ni ya Serikali ipo mpaka kwa Mkuu bado inasoma 23M ww nyumbani unarudi unakiuza 17M aliyenunua akalipe 7M wewe akuachie 10M ndio kule yakabumbuluka mbona figure zinapishana?
sasa hapo kuna upelelezi gani mnasubiri wa Afisa Ardhi kurudishwa
au Waziri Lukuvi analo jingine?
 
Kitendo cha kumwambia msimamizi wa ujenzi amuandikie maelezo ya kuchelewesha ukamilishaji wa ujenzi ili ampelekee mheshimiwa Rais ni udhaifu mkubwa kwa sababu HC ambao ndio wajenzi wa huo mradi wako chini ya wizara ya ardhi hivyo ripoti ya ucheleweshaji wa mradi anapaswa kuifanyia kazi yeye ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua viongozi wa NHC.

Kumbuka kwenye hilo sekeseke yupo Gavana wa jiji, Lukuvi ni very technical and bright, anajua anachokifanya huwa hakurupuki
 
Back
Top Bottom