Miongoni mwa mawaziri wachapakazi katika serikali ya awamu ya tano, William Lukuvi hana upinzani. Hata kuna wakati Fulani alifikiriwa kustahili kuwa mrithi wa Magufuli au hata uwaziri mkuu.
Katika Wizara ya Ardhi amesaidia kutatua matatizl na kero nyingi sana mfano: Migogoro ya ardhi, upatikanaji wa hati za viwanja, upimaji na urasimishaji viwanja na mashamba.
Jana katika ziara yake kwenye mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa vigunguti alidhihirisha udhaifu wa kutisha
1. Kitendo cha kumwambia msimamizi wa ujenzi amuandikie maelezo ya kuchelewesha ukamilishaji wa ujenzi ili ampelekee mheshimiwa Rais ni udhaifu mkubwa kwa sababu HC ambao ndio wajenzi wa huo mradi wako chini ya wizara ya ardhi hivyo ripoti ya ucheleweshaji wa mradi anapaswa kuifanyia kazi yeye ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua viongozi wa NHC.
Badala ya Mheshimiwa Lukuvi kufanya maamuzi, anamsukumia mheshimiwa Rais, huu ni udhaifu na kukwepa uwajibikaji
2. Kitendo cha Mheshimiwa Waziri kumuelekeza Mkurugenzi mkuu wa NHC kumpangia majukumu mengine Meneja wa Miliki kufuatia malalamiko ya wapangaji wa NHC kutozwa kodi ya sh 100,000 bila kupewa risiti wakati NHC inapokea sh 25,000 ni udhaifu pia.
Huo mchezo wa NHC kupangisha watu kwa kodi ndogo wakati hao wapangaji wakiwapangisha wenzao kwa kodi kubwa umekuwepo kwa siku nyingi. Mheshimiwa waziri alipaswa:
1. Kuwaagiza Takukuru kuwachunguza watuhumiwa wote wa wizi huo kisha kuwachukulia hatua
2. Meneja Miliki alipaswa kupisha uchunguzi
3. Uhakiki wa wapangaji wa NHC ulipaswa ufanyike nchi nzima
4. Waziri alipaswa kuagiza matumizi ya mfumo wa Kielektroniki katika ulipaji wa kodi za NHC
5. Waziri angewapa offer ya kulipa kodi ya sh 25,000 wale wapangaji wa NHC kwa mwaka mzima kwa kufichua wizi
6. Waziri alipaswa kuwapa kinga wale wapangaji kwa kutoindolewa katika fremu zile na kutobughudhiwa na watumishi wengine wa NHC.
Kwa kifupi Mheshimiwa Waziri alicheza chini ya Kiwango hivyo Mamlaka za juu zinaweza kuingilia kati.
Ndio maana nashangaa Mheshimiwa Jembe letu katika baraza la mawaziri, unakwama wapi ukwamuliwe?