Mheshimiwa Magufuli, ni lini utatutembelea Mbeya na Wilaya zake?

Mheshimiwa Magufuli, ni lini utatutembelea Mbeya na Wilaya zake?

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,870
Reaction score
15,068
1614334324220.png

Mara zote kutembelewa na mgeni ni baraka. Kutembelewa na Rais ni baraka zaidi.

Kutembelewa na Rais Magufuli ni baraka tele ambayo wananchi wa Mbeya tumekuwa tukisubiri bila kiu hiyo kusuuzwa kwa muda mrefu sana.

Kwa ziara za kamusudi kukagua maendeleo na kuhamasisha wananchi, Mkapa hakuwahi kutemebelea Mbeya, Kikwete hakuwahi kutembelea Mbeya na Magufuli hajawahi kutemebelea Mbeya.

Marais wote walifika Mbeya wakati wa Kampeni tu ya Urais.

Mheshimiwa Magufuli tunaomba ukate huu mzizi, wananchi wana hamu sana kukuona Mbeya.
 
Mbeya hatumtaki!kwani miradi mikubwa yote anaipeleka Dar,Dom Mwanza na Chato tu!
Mbeya tunadharauliwa sana,
Mpaka Leo uwanja wa SONGWE hauna taa za kuongozea taa usiku,huu si ni u..la?
Taa za kuongozea taa ni kitu gani hiko
 
Huku Lingusenguse hatajawahi kutembelewa na Rais yeyote toka nchi hii ipate uhuru wa bendera na miaka yote ya uchaguzi tunapigia kura chama dola,kwa hiyo mtoa hoja just relax mkuu
 
Nadhani umesahau mkuu, Rais Magufuli alishafanya ziara ya kikazi ya siku 8 mkoani Mbeya. Hii ilikua mwaka 2019.

 
Duuh yaani viongozi wote hao wamewakwepa??

Kuna tatizo mahali sio bure.

Nakumbuka Msafara wa JK uliwahi rushiwa mawe. Hatari sana.

Nadhani pia alishawahi tembelea huko,

Kama unakumbuka akaenda mpaka tunduma na walikutana na Rais wa Zambia Bwn . Lungu. Kama unakumbuka yule kiongozi wa Zambia aliyepokea fedha toka kwa Rais kwa kupiga magoti.
 
Back
Top Bottom