Mheshimiwa Rais, kabla ya watoto kurudi shule, wewe toka kwanza nyumbani kwako Chato rudi ofisini Ikulu

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Kwa mujibu wa sheria za nchi ofisi rasmi ya raisi ni Ikulu, Ikulu zozote zilizo ndani ya nchi na wala siyo nyumbani kwake.

Kwa sasa zaidi ya siku 50 Rais anafanyia kazi za nchi ndani ya nyumba yake huko Chato, sijajua yale mafaili confidential ya nchi anayaweka sebuleni kwake au dining room, hili hakuna anayelijua.

Hata hivyo raisi juzi kwenye hotuba ya kisiasa aliyoitoa akiwa madhabahuni alisikika akisema kuwa anakusudia kufungua vyuo maana anaamini nchini mambo ni shwari korona siyo tishio sana.

Mimi ningependa kumwambia ndugu rais kwamba, kabla ya kufungua vyuo rudi kwanza ofisini. Wakati akiwataka maelfu ya watumishi ambao ni waalimu warudi mashuleni kuchapa kazi basi ni muhimu naye akarudi katika ofisi ambayo kisheria ndiyo anayopaswa kufanyia shughuli za kiofisi.

Nyumba ya rais huko Chato siyo ya kwake peke yake, ni yake na mkewe. Mkewe ana haki ya kuchagua mtu gani aingie ndani ya nyumba hiyo, hata hivyo Ikulu siyo yake na mkewe kwa hiyo hawana haki ya kumkatalia mtu yeyote kwenda kupata huduma ya raisi au taasisi ya uraisi yenye ofisi zake Ikulu.

Kitendo cha raisi kufanyia kazi za nchi kwenye nyumba yake binafsi kinawanyima haki ya kupata huduma za kiofisi wananchi wengi wenye kutaka kupata huduma za kiofisi za raisi.

Kitu kingine ni kwamba nyumba ya raisi huko Chato haikujengwa makhsusi kuwa na hadhi ya Uraisi, haikuwekewa vifaa vyote vya ulinzi stahiki wa mtu anayekalia kiti cha rais, kwa hiyo ni security risk kwa rais kuendelea kukaa kwenye nyumba hiyo binafsi.

Kama rais anadhani Korona ipo under control atoke huko Chato kwenye nyumba ya mama yetu mama Janet aje kwenye nyumba ambayo wananchi wamemuweka afanye kazi zetu.

Ndugu rais uko nje ya ofisi kwa muda mrefu sasa, rudi ofisini!
 
Kuna wadau humu waliobobea kwenye masuala ya kisiasa na kiintelijensia kama Pascal Mayalla, walitoa ufafanuzi wa kina ya kwamba Rais anaweza akafanya shughuli zake za kiofisi huku akiwa mahali popote pale ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Hivyo mkuu mtoa mada, usiwe na hofu yoyote ile juu ya hilo. Mwezi ujao (wa sita) tunamtegemea aende Dodoma kulihutubia na pia kulivunja Bunge letu. Baada ya hapo, nina imani atarejea Ikulu ya Dar au atabaki kwenye ile Ikulu ya Chamwino.
 
Na confidential reports/documents zitatunzwa master bedroom kwake au?
 
Kwa mujibu wa sheria za nchi ofisi rasmi ya raisi ni Ikulu, Ikulu zozote zilizo ndani ya nchi na wala siyo nyumbani kwake.

Kwa sasa zaidi ya siku 50 Rais anafanyia kazi za nchi ndani ya nyumba yake huko Chato, sijajua yale mafaili confidential ya nchi anayaweka sebuleni kwake au dining room, hili hakuna anayelijua.

Hata hivyo raisi juzi kwenye hotuba ya kisiasa aliyoitoa akiwa madhabahuni alisikika akisema kuwa anakusudia kufungua vyuo maana anaamini nchini mambo ni shwari korona siyo tishio sana.

Mimi ningependa kumwambia ndugu rais kwamba, kabla ya kufungua vyuo rudi kwanza ofisini. Wakati akiwataka maelfu ya watumishi ambao ni waalimu warudi mashuleni kuchapa kazi basi ni muhimu naye akarudi katika ofisi ambayo kisheria ndiyo anayopaswa kufanyia shughuli za kiofisi.

Nyumba ya rais huko Chato siyo ya kwake peke yake, ni yake na mkewe. Mkewe ana haki ya kuchagua mtu gani aingie ndani ya nyumba hiyo, hata hivyo Ikulu siyo yake na mkewe kwa hiyo hawana haki ya kumkatalia mtu yeyote kwenda kupata huduma ya raisi au taasisi ya uraisi yenye ofisi zake Ikulu.

Kitendo cha raisi kufanyia kazi za nchi kwenye nyumba yake binafsi kinawanyima haki ya kupata huduma za kiofisi wananchi wengi wenye kutaka kupata huduma za kiofisi za raisi.

Kitu kingine ni kwamba nyumba ya raisi huko Chato haikujengwa makhsusi kuwa na hadhi ya Uraisi, haikuwekewa vifaa vyote vya ulinzi stahiki wa mtu anayekalia kiti cha rais, kwa hiyo ni security risk kwa rais kuendelea kukaa kwenye nyumba hiyo binafsi.

Kama rais anadhani Korona ipo under control atoke huko Chato kwenye nyumba ya mama yetu mama Janet aje kwenye nyumba ambayo wananchi wamemuweka afanye kazi zetu.

Ndugu rais uko nje ya ofisi kwa muda mrefu sasa, rudi ofisini!
Hao kina Bashite na JIWE wanatuambia tufanye kazi na tupige kazi kama kawaida huku tukichua tahadhari wakati wao wenyewe wamejificha,mimi mpaka nione wao kwanza wakifanya ziara kama awali na jiwe akirudi kula upepo wa bahari,kwenda kwenye vijiwe,kwenda kanisani kila jumapili kama ilivyo ada yake,bashite na yeye kuzunguka na convoy yake mitaa yote ya Dar,wakifanya hivyo ndio nitaamini wanachomaanisha ila wakiendelea kujificha ficha press conference au kuonekana kwenye TV kila baada ya wiki mbili nitazidi kuchanganya na zangu akili za kuambiwa.
 
Back
Top Bottom