Mheshimiwa Rais sidhani kama kupenda Kwako kila mara ' Kumtajataja ' hadharani TISS DG Dkt. Kipilimba ni sawa Kiuweledi

Kwa mujibu wa sheria ya usalama wa taifa, DG wa taasisi hiyo ndiye mtumish pekee anayetakiwa kutajwa na kujulikana... mtumsh mwingine yeyote yule kutajwa hadharan n kosa la jinai
 
USA trump sio tu kumtaja bali hata hudiriki kumpinga au kupishana na mkurugenzi wa C.I.A .

Wewe sema lako jambo usizunguke mbuyu.
Wenye akili tumekuelewa unachotaka kutuaminisha.

All in all!
Anapoteuliwa kuwa mkurugenzi wa TISS huwa anatangazwa hadharani hivyo yeye si siri bali taasisi yake ndio siri kiutendaji.
Acha hizooo[emoji1787]
 
Amtaje au asimtaje hadharani, watu wakihitaji kumjua watamjua tu. Ifikie wakati tuamini integrity ya watu wetu. Hata hivyo TISS ni chombo halali cha serikali kwahiyo hakuna ubaya mkuu wao kufahamika. Kazi zao kua siri ni sawa ila sio executives.
Mkuu huyu mleta mada anazunguka mbuyu tu ila hana hoja hapa.
Huyu mkurugenzi wa TISS yeye kama yeye uteuzi wake hutangazwa hadharani, so yeye sio siri bali taasisi yake na watendaji wake pamoja na shughuli zao.
 
Hakuna tatizo mkuu Gentamycine. Ni jambo la kawaida kabisa.

Lakini si jambo la kawaida kila mara kwenye mikutano ya halaiki, kumuamuru asimame na umati wote umuone aonekanaje, wajihi wake na kadhalika.
 
Unaweza kuwa unawapa sifa nyingi na heshima kubwa kuliko uwezo wao halisi. Acha watajwe tu.
 
Lakini si jambo la kawaida kila mara kwenye mikutano ya halaiki, kumuamuru asimame na umati wote umwone anaonekanaje, wajihi wake na kadhalika.
Katika dunia ya leo bado ni kawaida sana.
 
Nipe mfano nchi gani mkurugenzi mkuu wa idara ya usalama wa taifa katika dunia hii ya leo, atajwa hadharani na anaambiwa asimame na watu wamuone.
Hakuna ulazima wa kufanya hivyo kwakufuatisha nchi nyingine
Jambo la muhimu ni Athari za kitendo hicho kiusalama.
 
Hakuna ulazima wa kufanya hivyo kwakufuatisha nchi nyingine
Jambo la muhimu ni Athari za kitendo hicho kiusalama.

Basi kama ni hivyo ungesema kwamba "kwa Tanzania ya leo" na sio kusema, "kwa dunia ya leo".

Na hata ukisema kwa Tanzania ya leo, bado unaungana na mleta mada ambae anasema hiyo haijawahi kutokea huko nyuma.

Na kwa dunia ya leo hakuna nchi kiongozi wa taasisi kama hii ya kwetu anatajwatajwa hadharani na kusimamishwasimamishwa ili umati wa watu umuone.
 
Mwacheni Magufuli afanye kazi, kila siku yeye tu.
Hivi huwa hamna kazi ninyi, ndiyo maana tumechelewa kimaendeleo kama taifa.

We' re glad to have a ' NEW CERTIFIED FOOL ' on board. You're welcome!
 

Ndiyo Mkuu nilimsikia alivyonijibu leo pale UDSM na kuamini kuwa kumbe uwepo Wetu hapa JamiiForums huwa hatupotezi tu muda Wetu bali kumbe huwa tuna ' impact ' kubwa tu maeneo mbalimbali ya Kijamii hapa nchini. Nakupongeza pia kwa Wewe kuwa na ' Jicho ' la tatu la kuona hili tatizo ambalo nimeliibua hapa kwamba si jambo jema. Bado Wahusika ( hasa Watendaji wake Bwana Mkubwa ) hawajachelewa Kumrekebisha katika hili kwani sioni kama lina tija / mantiki kivile.
 
Wee Jamaa una Maneno mengi sana...ila una "Kaujiniazi" fulani hivi....Rekebisha baadhi ya Mapungufu yako ya "wazi" utakuwa Mtu smart sana kwa mahitaji ya Taifa. GENTAMYCINE

Noted na Wewe siyo wa Kwanza Kunikongole / Kunisifia hivi kwa uwezo wangu ( hapa Jamvini na hata katika Jamii niliyopo ) ila labda nikuambie tu kuwa hata Mimi napenda na nahitaji sana niwe ambavyo Wewe na wengineo humu / hapa Jamvini mnataka niwe ila kumbukeni tu ya kwamba hata katika ' Saikolojia ' imethibitika kuwa Watu wenye ' Uwerevu / Ujiniazi ' huwa pia wana ' Kasoro ' fulani ambazo hata ufanyeje haziwezi Kurekebishika labda mpaka dunia ikigeuka.

Ninachokuomba tu Mkuu Wewe chukua tu yale mema yangu hapa ila yale yangu ya ' Kipopoma ' nakuomba nianchie mwenyewe kwani sidhani kama nitakuja kubadilika. Wapitie Watu wengine ambao unawajua wako vizuri Kichwani / Kiakili / Kifikra kisha utagundua ya kwamba pamoja na kupewa ' Zawadi ' hiyo na Maulana / Mola ila wana ' Mapungufu ' fulani fulani pia ya hapa na pale.

Kikubwa tuvumiliane tu Mkuu au vipi?
 

Wewe ni Mmoja wa ' Genius Members ' wa JamiiForums ambao huwa nawakubali sana Mkuu. Naomba leo nikuambie hili na utembee Kifua mbele kabisa kuwa uko vizuri Kichwani. Kuna Watu wanadhani huu ' Uzi ' nimeuanzisha tu kama vile Kucheza ' makida makida ' ila wangetumia ' Jicho ' la Tatu katika kuona mbali zaidi nadhani wangekubali kwamba anachokifanya Mheshimiwa Rais kwa huyu TISS DG siyo sahihi kabisa ( hasa Kiuweledi wa Kazi / Jukumu husika ) na nahisi hata wana TISS wenyewe hili hawakubaliani nalo sema tu labda wanashindwa Kumrekebisha ' Bwana Mkubwa ' au pengine wameshamwambia lakini ' mwambiwaji ' nae akawa ni wale wale akina ' SIKIO LA KUFA '.......naomba niishie hapa tafadhali.
 
mzee wa porojo Nyingi Genta..

Ila zinazosikika, kufuatiliwa, kujadiliwa hadi kufanyiwa Kazi na IKULU yako ya Magogoni na hatimaye nakuja kujibiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mkuu wako wa nchi.
 
Huyu anampenda sana maana ndiye aliyemsaidia wizi ka kura mpaka akaukwaa urais, hivyo anajipendekeza sana ili isije siku moja siri ikavuja. Nchi nyingine zina tume huru za uchaguzi

Mmmmh....makubwa Mkuu Mimi simo!!!!!!!!
 

Huwa napenda na nafurahi sana kukutana na ' Majiniazi ' wachache wa mfano wako hapa Jamvini JamiiForums. Nimekukubali mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…