Mheshimiwa Rais sidhani kama kupenda Kwako kila mara ' Kumtajataja ' hadharani TISS DG Dkt. Kipilimba ni sawa Kiuweledi

Mheshimiwa Rais sidhani kama kupenda Kwako kila mara ' Kumtajataja ' hadharani TISS DG Dkt. Kipilimba ni sawa Kiuweledi

ANGALIZO

Naomba kama unajijua kabisa kuwa uwezo wako wa kuona vitu vya umbali / unyeti / umuhimu wake basi katika huu ' Uzi ' kaa nao mbali kabisa na waachie wenye ' akili ' zao na ' Wachambuzi ' wa masuala haya ya Kijasusi ambao wapo ( tunao ) wengi humu na Sisi Mangumbaru na Mapopoma wengine tuwe watazamaji tu kuliko Kuchangia halafu ukajikuta umevapa / umekosea.

HOJA KUU

Nashukuru sana Mwenyezi Mungu kwamba karibia awamu zote za nchi hii nilikuwepo japo ya Hayati Baba wa Taifa ilinikutia nikiwa bado katika Ndoo ya Kuogea na nalilia Uji wa Buruga ( namaanisha nikiwa bado Kichanga kabisa ) ila kwa awamu ya Mzee Mwinyi niliishuhudia bila kusahau ya Mzee Mkapa na ya Mzee Kikwete na sasa nipo hii ya Mheshimiwa Dkt. Magufuli natiririka na naserereka nayo.

Katika Awamu zote hizo sikuwahi hata Siku moja kuwasikia hao Watangulizi wake Rais Dkt. Magufuli wakiwa na tabia ya kupenda ' Kumtajataja ' au hata kupenda kuonyesha kwamba Mkurugenzi Mkuu wa Idara Nyeti nchini ya Usalama wa Taifa ( TISS ) yupo eneo ambalo Wao wapo ila ilikuwa ni mpaka tu labda Mtu akutonye / akuambie.

Nimejuiuliza maswali mengi sana kwani Marais wote Wastaafu walikuwa hawapendi kuwatajataja Wakuregenzi wao Usalama wa Taifa ( TISS DG ) lakini kwa Awamu hii ya Gwala / Tano Rais Dkt. Magufuli anapenda mno ' Kumtaja ' na hata kupenda ' Kumuinua ' Kitini Mkurugenzi wa sasa Dkt. Modestus Kipilimba na bado sijapata jawabu / jibu ila najua kupitia ' Majiniasi ' waliotukuka wa Jamvi hili la JamiiForums leo nitayapata.

Sikuishia tu hapo kama kawaida yangu huwa napenda kwenda ' deep ' zaidi kufanya ' references ' na Mataifa mengine mbalimbali kuanzia na haya Jirani ( tunaofanana kwa Vingi ) kisha hupenda pia kuangalia na yale Mataifa makubwa ambayo yana uwezo mkubwa wa Kuanzia Uchumi, Kijeshi na Kiusalama kuliko Tanzania yetu hii na sijaona mahala ambapo Marais wao huwa wanawataja hovyo tena hadharani Wakurugenzi Wakuu wa Idara zao ' Nyeti ' za Usalama wa Taifa ila kwa Tanzania naona hii tabia inaanza Kuzoeleka.

Kwa maoni au mtazamo wangu mdogo tu ( mnaojua zaidi mtanisaidia ) kwa asili ya hizi nchi zetu tena ambazo zina ' Majaribu ' na ' Matatizo ' mengi ya Kimsingi huku kukiwa na ' Maadui ' wengi wa ndani na nje sidhani na siafiki kabisa tena kwa 100% kwa Wakurugenzi wetu hawa wa hii Idara / Taasisi muhimu kama si nyeti ya Usalama wa Taifa ( TISS ) kutajwatajwa hovyo kwa Watu na hata kujulikana kwakuwa Tanzania ya sasa imejaa Watu wa ajabu ajabu wenye ' maslahi ' yao ' hasi ' na nchi hii hivyo kuna uwezekano na Wao wakaanza Kumjua na Kumzoea kisha hali ikaja kuwa mbaya zaidi huko mbeleni.

Na sidhani pia kama hata ' Kiuweledi ' hivi anavyofanya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. Magufuli la kupenda ' Kumtajataja ' Mkurugenzi Mkuu wa Idara / Taasisi ya Usalama wa Taifa ( TISS DG ) Dkt. Kipilimba ni sahihi na kama itapendeza nadhani Watu wa ' Itifaki ' ambao nina uhakika kuwa wengi wenu tunatiririka na kuserereka pamoja 24/7 hapa JamiiForums hili mtaliangalia kwa hayo mapana yake ili utaratibu ule ule uliozoeleka wa zamani wa hawa Wakurugenzi kutojulikana sana au kutajwatajwa hovyo uendelee kwani Kwangu Mimi kwa ' Mazingira ' ya nchi yetu ulikuwa ni utaratibu murua / mujarab / sahihi kabisa kuliko huu wa sasa aliouanzisha Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dkt. Magufuli.

Huu ulikuwa ni mtizamo wangu Mimi kama GENTAMYCINE ila nitashukuru na Watu wengine nao wakija hapa wakichangia huku wale ambao ' watanikosoa ' basi wanikosoe ha ' Hoja ' nzito nzito kwani hata Mimi nataka Kujifunza jambo hapa kutokana na kwamba yawezekana huu utaratibu wa sasa ukawa ndiyo sahihi kuliko ule ambalo nimeukariri / nimeuzoea. Nia na madhamuni tupate afya ya Kimjadala na ya Kimantiki juu ya hili ' Suala ' kusudi mwisho wa Siku wote tupate ' maarifa ' na ' ufahamu ' zaidi.

Karibuni!

Nawasilisha.
Kwa mujibu wa sheria ya usalama wa taifa, DG wa taasisi hiyo ndiye mtumish pekee anayetakiwa kutajwa na kujulikana... mtumsh mwingine yeyote yule kutajwa hadharan n kosa la jinai
 
Sijawahi Kuanzisha ' Threads ' fupi hapa JamiiForums Mkuu ( pitia threads zangu zote za mambo sensitive zilivyo ) na nashukuru zote zimekuwa zikisomwa na kupata mrejesho wake hivyo labda hili ni tatizo lako tu. Hata hivyo asante kwa kuja na kuchangia hivyo nikuombe tu kaa pembeni waachie ' Great Thinkers ' waje waweze kunipa ' Madini ' tafadhali.
USA trump sio tu kumtaja bali hata hudiriki kumpinga au kupishana na mkurugenzi wa C.I.A .

Wewe sema lako jambo usizunguke mbuyu.
Wenye akili tumekuelewa unachotaka kutuaminisha.

All in all!
Anapoteuliwa kuwa mkurugenzi wa TISS huwa anatangazwa hadharani hivyo yeye si siri bali taasisi yake ndio siri kiutendaji.
Acha hizooo[emoji1787]
 
Amtaje au asimtaje hadharani, watu wakihitaji kumjua watamjua tu. Ifikie wakati tuamini integrity ya watu wetu. Hata hivyo TISS ni chombo halali cha serikali kwahiyo hakuna ubaya mkuu wao kufahamika. Kazi zao kua siri ni sawa ila sio executives.
Mkuu huyu mleta mada anazunguka mbuyu tu ila hana hoja hapa.
Huyu mkurugenzi wa TISS yeye kama yeye uteuzi wake hutangazwa hadharani, so yeye sio siri bali taasisi yake na watendaji wake pamoja na shughuli zao.
 
Hakuna tatizo mkuu Gentamycine. Ni jambo la kawaida kabisa.

Lakini si jambo la kawaida kila mara kwenye mikutano ya halaiki, kumuamuru asimame na umati wote umuone aonekanaje, wajihi wake na kadhalika.
 
Unaweza kuwa unawapa sifa nyingi na heshima kubwa kuliko uwezo wao halisi. Acha watajwe tu.
 
Lakini si jambo la kawaida kila mara kwenye mikutano ya halaiki, kumuamuru asimame na umati wote umwone anaonekanaje, wajihi wake na kadhalika.
Katika dunia ya leo bado ni kawaida sana.
 
Nipe mfano nchi gani mkurugenzi mkuu wa idara ya usalama wa taifa katika dunia hii ya leo, atajwa hadharani na anaambiwa asimame na watu wamuone.
Hakuna ulazima wa kufanya hivyo kwakufuatisha nchi nyingine
Jambo la muhimu ni Athari za kitendo hicho kiusalama.
 
Hakuna ulazima wa kufanya hivyo kwakufuatisha nchi nyingine
Jambo la muhimu ni Athari za kitendo hicho kiusalama.

Basi kama ni hivyo ungesema kwamba "kwa Tanzania ya leo" na sio kusema, "kwa dunia ya leo".

Na hata ukisema kwa Tanzania ya leo, bado unaungana na mleta mada ambae anasema hiyo haijawahi kutokea huko nyuma.

Na kwa dunia ya leo hakuna nchi kiongozi wa taasisi kama hii ya kwetu anatajwatajwa hadharani na kusimamishwasimamishwa ili umati wa watu umuone.
 
Mwacheni Magufuli afanye kazi, kila siku yeye tu.
Hivi huwa hamna kazi ninyi, ndiyo maana tumechelewa kimaendeleo kama taifa.

We' re glad to have a ' NEW CERTIFIED FOOL ' on board. You're welcome!
 
Mkuu mleta mada GENTAMYCINE upo sahihi asilimia 100% ndy maana hata ujumbe/ushauri wako wa upendeleo wa mkuu wetu (kupendelea UDSM kama hamna vyuo vingine) umefika na kupokelewa kwa mikono yote (Nafikiri utakuwa umemsikia mkuu wa kaya)

Hii tunasema ni defense mechanism anavyosema kuwa wakuu wa vyombo vya usalama na mkuu wa Usalama wa Taifa ( TISS ),sasa kwa hali tuliyonayo hapa Tanzania kwa sasa haitakiwi kutajwa kabisa yeye aendeleee na kuwataja wengine lakini aachane kabisa na vyombo vya ulinzi na Usalama wa Taifa ( TISS ).

Hawa wote ni watu ambao hawatakiwi kuzoeleka machoni pa jamii japo wanajulikana lakini siyo kutajwa kwenye public.

Nafikiri ujumbe huu utamfikia kupitia mtiririko huu wa hapa jamvi la jamiiForum

Ndiyo Mkuu nilimsikia alivyonijibu leo pale UDSM na kuamini kuwa kumbe uwepo Wetu hapa JamiiForums huwa hatupotezi tu muda Wetu bali kumbe huwa tuna ' impact ' kubwa tu maeneo mbalimbali ya Kijamii hapa nchini. Nakupongeza pia kwa Wewe kuwa na ' Jicho ' la tatu la kuona hili tatizo ambalo nimeliibua hapa kwamba si jambo jema. Bado Wahusika ( hasa Watendaji wake Bwana Mkubwa ) hawajachelewa Kumrekebisha katika hili kwani sioni kama lina tija / mantiki kivile.
 
Wee Jamaa una Maneno mengi sana...ila una "Kaujiniazi" fulani hivi....Rekebisha baadhi ya Mapungufu yako ya "wazi" utakuwa Mtu smart sana kwa mahitaji ya Taifa. GENTAMYCINE

Noted na Wewe siyo wa Kwanza Kunikongole / Kunisifia hivi kwa uwezo wangu ( hapa Jamvini na hata katika Jamii niliyopo ) ila labda nikuambie tu kuwa hata Mimi napenda na nahitaji sana niwe ambavyo Wewe na wengineo humu / hapa Jamvini mnataka niwe ila kumbukeni tu ya kwamba hata katika ' Saikolojia ' imethibitika kuwa Watu wenye ' Uwerevu / Ujiniazi ' huwa pia wana ' Kasoro ' fulani ambazo hata ufanyeje haziwezi Kurekebishika labda mpaka dunia ikigeuka.

Ninachokuomba tu Mkuu Wewe chukua tu yale mema yangu hapa ila yale yangu ya ' Kipopoma ' nakuomba nianchie mwenyewe kwani sidhani kama nitakuja kubadilika. Wapitie Watu wengine ambao unawajua wako vizuri Kichwani / Kiakili / Kifikra kisha utagundua ya kwamba pamoja na kupewa ' Zawadi ' hiyo na Maulana / Mola ila wana ' Mapungufu ' fulani fulani pia ya hapa na pale.

Kikubwa tuvumiliane tu Mkuu au vipi?
 
Katika mataifa yote makini huwezi kusikia mission yoyote ikihusishwa na usalama wa taifa. Usalama wa taifa hufanya mission nyinging sana lakini mwisho wake utasikia "Jeshi la Polisi limekamata, au TANESCO Imegundua, au wasamaria wema wawataja waharifu/majambazi, au wanafunzi wa chuo fulani waibua maduxu, au ofisi ya mlaguzi mkuu wa serikali yai ua madudu, au Speaker wabunge atoa utaratibu mpya, au Benki kuu yagundua au T.R.A yagundua mianya inayotumiwa na wafanyabiashara kukwepa kodi au Rais amtumbua kiongozi fulani au amteua fulani.
Ukiangalia, asilimia karibu 80 ya hayo yote hufanywa na idara ya Usalama wa taifa lakini hutumia mamlaka tofauti kuelezea kazi zao, wao si kazi yao kujieleza, wao hufanya lakini mwisho huiunganisha mamlaka husika bila mamlaka hiyo kujua kuwa unafanya kazi ya idara ya usalama. Idara huendelea kufanya kazi zake kwa ukimwa na usiri kama vile haipo. Mkuu wa Idara si mtu wa kuonekana onekana hata kwenye misafara ya rais.
Kitendo anachokifanya rais Magufuli kinaifanya idara ya usalama isomeke sana, wataalamu inawawia rahisi sana kuunganisha dots.

Wewe ni Mmoja wa ' Genius Members ' wa JamiiForums ambao huwa nawakubali sana Mkuu. Naomba leo nikuambie hili na utembee Kifua mbele kabisa kuwa uko vizuri Kichwani. Kuna Watu wanadhani huu ' Uzi ' nimeuanzisha tu kama vile Kucheza ' makida makida ' ila wangetumia ' Jicho ' la Tatu katika kuona mbali zaidi nadhani wangekubali kwamba anachokifanya Mheshimiwa Rais kwa huyu TISS DG siyo sahihi kabisa ( hasa Kiuweledi wa Kazi / Jukumu husika ) na nahisi hata wana TISS wenyewe hili hawakubaliani nalo sema tu labda wanashindwa Kumrekebisha ' Bwana Mkubwa ' au pengine wameshamwambia lakini ' mwambiwaji ' nae akawa ni wale wale akina ' SIKIO LA KUFA '.......naomba niishie hapa tafadhali.
 
mzee wa porojo Nyingi Genta..

Ila zinazosikika, kufuatiliwa, kujadiliwa hadi kufanyiwa Kazi na IKULU yako ya Magogoni na hatimaye nakuja kujibiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mkuu wako wa nchi.
 
Huyu anampenda sana maana ndiye aliyemsaidia wizi ka kura mpaka akaukwaa urais, hivyo anajipendekeza sana ili isije siku moja siri ikavuja. Nchi nyingine zina tume huru za uchaguzi

Mmmmh....makubwa Mkuu Mimi simo!!!!!!!!
 
Mimi nina haya machache kutokana na uwezo wangu mdogo katika mambo haya,

Kwanza niseme awamu zote nimekuwepo awamu ya kwanza nilikuwa shule na zilizofuata na hii hapa ya Tano kwanza haikuwa Rahisi kujua Mkurugenzi wa TISS au kuwajua watumishi wao hata pale walipotaka kusafirisha mkurugenzi wao usingeweza kujua ila sasa mavimurimuri wanawazidi hata Traffic hili nikosa maana kwa sasa na wao wanataka watambulike kuwa wao ndo TISS hivyo naona utofauti mkubwa sana,na wakati wakumpata mkurugenzi wao kulikuwa na vetting ya Directories RSO,DSO,etc ya TISS na ya kamati kuu za ulinzi na usalama anapelekewa Rais anateua katika majina aliyopewa,tofauti na sasa anachagua kutokana na matakwa yake hata wakuu wa majeshi as well.Naomba mchukulie haya maelezo kama binafsi.

Huwa napenda na nafurahi sana kukutana na ' Majiniazi ' wachache wa mfano wako hapa Jamvini JamiiForums. Nimekukubali mno.
 
Back
Top Bottom